Tutie bidii kujifunza Kingereza, lakini tusikidharau Kiswahili chetu

Tutie bidii kujifunza Kingereza, lakini tusikidharau Kiswahili chetu

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Inawezekana idadi ya Waganda wanaojua Kingereza ni kubwa kuliko idadi ya Watanzania wanaojua Kimalkia, lakini si kila Mganda anajua Kizungu. Nililijua hili kwa mara ya kwanza mwaka Jana baada ya kufika Kampala kwa muda mfupi, lakini safari hii nimepata uzoefu mpana zaidi.

Japo kuna boda boda na mama lishe wanaojua Kizungu, lakini siyo kila Mganda anaifahamu hiyo lugha.

Pamoja na kuwa idadi kubwa ya Waganda wanaweza wakawa wanakifahamu Kizungu, hawakishiboei kivile. Karibia kila utakakopita utakutana na Kiganda!

Katika mizunguko yangu ya hapa na pale, nimekutana na Waganda wasioongea Kizungu kabisa. Kuna ambao wanakisikia lakini hawawezi kujibu kwa Kizungu, na kuna wasioelewa kabisa.

Mfano:
1. Nilipanda daladala (kwa huku huita taxi), na nilipohisi nimefika ninakopaswa kushuka, nilipomeuliza konda kama tumetoka, yeye alichoweza kusema ni kauli moja tu:"My money, My money...) huku akiwa amenibyooshea mkono ishara ya kutaka kupokea kitu

2. Nilipokuwa ninakuja Kampala, nililazimika kulala nje ya mji wa Kampala kesho yake ndiyo nikaenda hadi Kampala Mjini. Nilipoenda kutafuta gesti ya kulala siku hiyo, nilikuta mhudumu anayehusika na vyumba hajui kabisa English. Ilibidi nimwite mhudumu wa upande wa vinywaji ili awe mkalimani.

Hiyo changamoto nimekutana nayo pia kwa boda boda wa Kampala. Baadhi hawelewi kabisa Kizungu.

Kwa hiyo:
1. Tuendelee kutoa bidii kujifunza Kizungu

2. Tusikidhobokee Kizungu, hasa kama unanifahamu

3. Ukisikia watu wanasema Watanzania hawajui English, usiwaamini. Kuna Watanzania wanaojua Kizungu na kuna wasiojua, kama ilivyo kwa nchi zingine kama Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Kwa ufupi, ijulikane kuwa tunakijua Kizungu ili hatukishobei kwa sababu tunaipenda lugha yetu ya Taifa.
 
kizungu ni lugha tu kama kisukuma,kikurya, kijaluo, kijita ni ukienda kwa wajita jifunze kijita ili uwasiliane nao vizuri, mbona wazungu wanalazimika kujifunza kiswahili ili waweze kuelewana na sisi, sasa hapa nadhani na kaushamba kamo kamo huwa yunaamini anayeweza kizungu ndio msomi
 
Mtanzania akiongeleshwa kizungu kwa dakika 15 mfululizo anaweza kuzimia
Upo sawa. Ila kwanza uanze kueleza kizungu ni lugha gani. Je ni kifaransa? Español? Dutch? German? Denish?

Vizungu vipo vingi ila kama ni kiingereza tu wabongo wengi wanajua hata kuomba maji.
 
Back
Top Bottom