SoC03 Tutumie digitali ili kukuza idadi ya watu kushiriki Uchaguzi Mkuu

Stories of Change - 2023 Competition

Mdudu Mende

Member
Joined
Mar 31, 2021
Posts
78
Reaction score
120
Kutokana na Sensa ya mwaka 2022, Zaidi ya watanzania milioni 40 wana umri wa kushiriki kuchagua kiongozi, yaani kupiga kura. Kutokana na namna chaguzi zinavyoendesha miaka yote tumekuwa na idadi ndogo ya wanaojiandikisha kupiga kura, na katika wanaojiandikisha kupiga kura ni wachache kati yao ambao hupiga kura.

Hili ni tatizo limekuweo kwa muda mrefu. Unaweza kuangalia baadhi ya taarifa za upigaji kura kwa miaka ya nyuma kwa taarifa rasmi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mathalani hadi sasa wanaotambulika kama wapiga kura ni 29,188,347 tu kati ya watu Zaidi ya milioni 40 wanaostahili kupiga kura.

1689240234579.png

https://www.nec.go.tz/uploads/docum...A TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020.pdf

Kwa takwimu hizi, ni takriban 50% ya watu hawajitokezi kupiga kura. Hali ilikuwa mbaya Zaidi kwa mwaka 2010 na mwaka 2020. Inaonekana kabla ya mwaka 2005 watu walikuwa na muamko sana wa kushiriki mchakato wa uchaguzi kwa kupiga kura.

Tatizo lipo wapi? Kwanini hawaji kupiga kura?

Sitii mashaka kuwa watu wanaenda kupiga kura, ila hali za maisha mara nyingine zinaathiri ushiriki wa watu hawa. Mathalani, watu wengi wameajiriwa kwenye sekta isiyorasmi, na hata walio kwenye mfumo rasmi, mara nyingine huwa mbali na vituo walivyojiandikisha au kuhuisha taarifa zao za kupiga kura. Mimi nikitaja mahali nilipo na mahali nilipojiandikisha ni umbali wa siku mbili kwa basi. Hata hivyo kuna wengine wana kazi ambazo ni ngumu kumsubirisha mtu, chukulia mfano dereva wa mabasi makubwa au wengine wasioweza kuhudhuria kwenye vituo vya kura. Kuna watu wengine hupata maradhi, hivyo siku za uchaguzi huwa wamelazwa hospitalini hawezi kuja kwenye kituo au kusimama. Kwa hakika ni ukatili kufanya mzee au mtu mwenye ulemavu asimame kwenye foleni kuja kupiga kura wakati tunaweza kumpunguzia adha zote hizi.

Japo hizi zinaweza zisiwe sababu za moja kwa moja, lakini ni muhimu kuzingatia kuwa zinaweza kuwa zinasababisha watu kushindwa kushiriki tukio hili muhimu la kuchagua kiongozi wanayemtaka. Hivyo, badala ya tume kujikita kwenye elimu kwa umma pekee inabidi wachukue njia nyingine ambazo zinazingatia suala la mtu kuweza kushiriki kwa dharura zote.

Digitali kama suluhu ya tatizo

Pamoja na kuongeza elimu kwa umma lakini bila kuhakikisha zoezi linakuwa rafiki kwa kila mmoja bado tutakumbana na suala hili la watu kutoshiriki katika uchaguzi. Hivyo ni muhimu kuhakikisha watu wanatumia digitali katika kupiga kura. Hadi sasa idadi ya watanzania wenye simu ni kubwa sana hali inayotupa uhakika kuwa wengi wanaweza kushiriki kwa simu zao kupiga kura popote walipo bila kuhitaji kwenda kwenye kituo cha kupiga kura.

Hii itafanyika kama ifuatavyo, tunaweza kuwa na USSD code ya serikali ambayo mtu ataipiga, atachagua huduma za kiserikali, atachagua kupiga kura, ataweka namba yake ya mpiga kura ili imtambue mahali alipotokea kisha atapiga kura kwa watu anaowataka. Baada ya kupiga kura, taarifa iende kwa msimamizi wa kituo kuwa namba ya mpiga kura fulani imeshapiga kura, ili ikitokea akataka kupiga kura mara mbili isiwe rahisi, kwa maana kuwa taarifa zitakuwa zimeshafika kwa msimamizi wa kituo kuwa namba hiyo imeshatumika.

Hii itarahisisha kwa mtu yoyote, ambapo, hata kama mtu hana simu anaweza kuchukua simu ya jirani yake na kutumia kupiga kura, kwa kuwa namba zao za wapiga kura hazifanani. Hii itasaidia sana kufanya raia washiriki mchakato huu muhimu wa kukuza uwajibikaji na demokrasia nchini.

Pamoja na SSID code, tuwe na app na website ya kusaidia kupokea kura online, na mchakato uwe rafiki ili mtu asipate shida ya kurudiarudia taarifa. Link ya kuweza kupiga kura inaweza kutumwa kwa kila mtanzania, kama ambavyo mlitusumbua na zoezi la sensa kutukumbusha kujiandaa.

Hivyo, kama tunaenda kidigitali, tuhakikishe mfumo unaweza kuhudumia watu zaidi ya milioni 100 kwa wakati mmoja ili kusiwe na mikwamo mikwama ya ”try again”. Maana kuna udhaifu kwa uwekezaji wa kidigitali nchini, ambapo mara nyingine nchi imekuwa haiweki mfumo kuwa na uwezo wa kuhudumia watu wengi kwa wakati mmoja. Nikitoa mfano wa ajira za Walimu/watu wa afya nchini huwa na usumbufu wa mfumo kushindwa kutokana na uchache wa bandwidths na mfumo kutokuwa tayari. Hivyo ni muhimu kuujaribu mfumo huu mwaka mmoja kabla, hivi tuna uchaguzi 2025 basi mfumo unafanyiwa majaribio 2024 ili kuhakikisha kila kitu kitafanya kazi vizuri siku ya uchaguzi.

Digitali ni namna rafiki hata wakati wa majanga ya magonjwa ya mlipuko

Njia hii itapunguza msongamano kwenye vituo vya wapiga kura na hivyo kwa wale watakaoenda watakuwa na muda mchache wa kusubiri ili kupiga kura. Mfumo huu unafanyakazi vyema hata wakati wa majanga kama COVID19 ambayo yanahitaji kuwekeana umbali au kuzuia mikusanyiko. Hivyo serikali ikiwekeza vya kutosha kwenye digitali tutakuwa na uwezo mkubwa wa kuendelea na masiha yetu hata wakati wa majanga makubwa.

Pia, suala la viongozi kuhofia masuala ya ghasia katika vituo yanatatuliwa vyema na digitali. Hapa, viongozi hawatakuwa na hofu ya kuwa raia watajazana nje ya vituo na kuhofia fujo na ugomvi wakati wa kutangaza matokeo. Hii, ni zaidi ya kupata watu tu wa kupiga kura bali pia ni muhimu kwa kupunguza ghasia ambazo mara nyingi hutokea wakati wa uchaguzi mkuu.

Tuwekeze kidigitali.
 
Upvote 2
Kutokana na Sensa ya mwaka 2022, Zaidi ya watanzania milioni 40 wana umri wa kushiriki kuchagua kiongozi, yaani kupiga kura. Kutokana na namna chaguzi zinavyoendesha miaka yote tumekuwa na idadi ndogo ya wanaojiandikisha kupiga kura, na katika wanaojiandikisha kupiga kura ni wachache kati yao ambao hupiga kura.

Hili ni tatizo limekuweo kwa muda mrefu. Unaweza kuangalia baadhi ya taarifa za upigaji kura kwa miaka ya nyuma kwa taarifa rasmi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mathalani hadi sasa wanaotambulika kama wapiga kura ni 29,188,347 tu kati ya watu Zaidi ya milioni 40 wanaostahili kupiga kura.

View attachment 2686590

https://www.nec.go.tz/uploads/documents/sw/1637761579-MPYA TAARIFA YA TATHMINI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020.pdf

Kwa takwimu hizi, ni takriban 50% ya watu hawajitokezi kupiga kura. Hali ilikuwa mbaya Zaidi kwa mwaka 2010 na mwaka 2020. Inaonekana kabla ya mwaka 2005 watu walikuwa na muamko sana wa kushiriki mchakato wa uchaguzi kwa kupiga kura.

Tatizo lipo wapi? Kwanini hawaji kupiga kura?

Sitii mashaka kuwa watu wanaenda kupiga kura, ila hali za maisha mara nyingine zinaathiri ushiriki wa watu hawa. Mathalani, watu wengi wameajiriwa kwenye sekta isiyorasmi, na hata walio kwenye mfumo rasmi, mara nyingine huwa mbali na vituo walivyojiandikisha au kuhuisha taarifa zao za kupiga kura. Mimi nikitaja mahali nilipo na mahali nilipojiandikisha ni umbali wa siku mbili kwa basi. Hata hivyo kuna wengine wana kazi ambazo ni ngumu kumsubirisha mtu, chukulia mfano dereva wa mabasi makubwa au wengine wasioweza kuhudhuria kwenye vituo vya kura. Kuna watu wengine hupata maradhi, hivyo siku za uchaguzi huwa wamelazwa hospitalini hawezi kuja kwenye kituo au kusimama. Kwa hakika ni ukatili kufanya mzee au mtu mwenye ulemavu asimame kwenye foleni kuja kupiga kura wakati tunaweza kumpunguzia adha zote hizi.

Japo hizi zinaweza zisiwe sababu za moja kwa moja, lakini ni muhimu kuzingatia kuwa zinaweza kuwa zinasababisha watu kushindwa kushiriki tukio hili muhimu la kuchagua kiongozi wanayemtaka. Hivyo, badala ya tume kujikita kwenye elimu kwa umma pekee inabidi wachukue njia nyingine ambazo zinazingatia suala la mtu kuweza kushiriki kwa dharura zote.

Digitali kama suluhu ya tatizo

Pamoja na kuongeza elimu kwa umma lakini bila kuhakikisha zoezi linakuwa rafiki kwa kila mmoja bado tutakumbana na suala hili la watu kutoshiriki katika uchaguzi. Hivyo ni muhimu kuhakikisha watu wanatumia digitali katika kupiga kura. Hadi sasa idadi ya watanzania wenye simu ni kubwa sana hali inayotupa uhakika kuwa wengi wanaweza kushiriki kwa simu zao kupiga kura popote walipo bila kuhitaji kwenda kwenye kituo cha kupiga kura.

Hii itafanyika kama ifuatavyo, tunaweza kuwa na SSID code ya serikali ambayo mtu ataipiga, atachagua huduma za kiserikali, atachagua kupiga kura, ataweka namba yake ya mpiga kura ili imtambue mahali alipotokea kisha atapiga kura kwa watu anaowataka. Baada ya kupiga kura, taarifa iende kwa msimamizi wa kituo kuwa namba ya mpiga kura fulani imeshapiga kura, ili ikitokea akataka kupiga kura mara mbili isiwe rahisi, kwa maana kuwa taarifa zitakuwa zimeshafika kwa msimamizi wa kituo kuwa namba hiyo imeshatumika.

Hii itarahisisha kwa mtu yoyote, ambapo, hata kama mtu hana simu anaweza kuchukua simu ya jirani yake na kutumia kupiga kura, kwa kuwa namba zao za wapiga kura hazifanani. Hii itasaidia sana kufanya raia washiriki mchakato huu muhimu wa kukuza uwajibikaji na demokrasia nchini.

Pamoja na SSID code, tuwe na app na website ya kusaidia kupokea kura online, na mchakato uwe rafiki ili mtu asipate shida ya kurudiarudia taarifa. Link ya kuweza kupiga kura inaweza kutumwa kwa kila mtanzania, kama ambavyo mlitusumbua na zoezi la sensa kutukumbusha kujiandaa.

Hivyo, kama tunaenda kidigitali, tuhakikishe mfumo unaweza kuhudumia watu zaidi ya milioni 100 kwa wakati mmoja ili kusiwe na mikwamo mikwama ya ”try again”. Maana kuna udhaifu kwa uwekezaji wa kidigitali nchini, ambapo mara nyingine nchi imekuwa haiweki mfumo kuwa na uwezo wa kuhudumia watu wengi kwa wakati mmoja. Nikitoa mfano wa ajira za Walimu/watu wa afya nchini huwa na usumbufu wa mfumo kushindwa kutokana na uchache wa bandwidths na mfumo kutokuwa tayari. Hivyo ni muhimu kuujaribu mfumo huu mwaka mmoja kabla, hivi tuna uchaguzi 2025 basi mfumo unafanyiwa majaribio 2024 ili kuhakikisha kila kitu kitafanya kazi vizuri siku ya uchaguzi.

Digitali ni namna rafiki hata wakati wa majanga ya magonjwa ya mlipuko

Njia hii itapunguza msongamano kwenye vituo vya wapiga kura na hivyo kwa wale watakaoenda watakuwa na muda mchache wa kusubiri ili kupiga kura. Mfumo huu unafanyakazi vyema hata wakati wa majanga kama COVID19 ambayo yanahitaji kuwekeana umbali au kuzuia mikusanyiko. Hivyo serikali ikiwekeza vya kutosha kwenye digitali tutakuwa na uwezo mkubwa wa kuendelea na masiha yetu hata wakati wa majanga makubwa.

Pia, suala la viongozi kuhofia masuala ya ghasia katika vituo yanatatuliwa vyema na digitali. Hapa, viongozi hawatakuwa na hofu ya kuwa raia watajazana nje ya vituo na kuhofia fujo na ugomvi wakati wa kutangaza matokeo. Hii, ni zaidi ya kupata watu tu wa kupiga kura bali pia ni muhimu kwa kupunguza ghasia ambazo mara nyingi hutokea wakati wa uchaguzi mkuu.

Tuwekeze kidigitali.
Wazo zuri sana naunga hoja.
 
Back
Top Bottom