JamiiTalks Tutumie taarifa za Rushwa ya Ngono na Unyanyasaji sehemu ulipo, ili Mamlaka za Serikali zizifanyie kazi

Mimi nina kesi Geita mtoto wa mdogo wangu alibakwa usiku kucha na mshtakiwa akakubali lakini polisi waligeuza kibao.

Mtoto mpaka sasa anaumwa ana matatizo ya kisikolojia na hataki tena kusikia jina mwanamme. Alikuwa anamfanyia kibarua kama mjenzi yeye ni kibarua wake. Alipoenda kumsaidia kupeleka maji nyumbani akambaka. Tulienda bali lakini wakasema alishafikisha miaka 18 kesi haina maana.

Mtoto ameathirika kisaikolojia na hataki kitu chochote kuhusu mapenzi. Aliachiwa gono akatibu angalau siyo UKIMWI. Mimi mwenyewe nilihusisha mahakimu, askari na kila mtu lakini kesi ikabuma tangu 2014. Geita Geita Geita.
 
Asante kwa Taarifa na pole kwa Matatizo.

Tunaomba kuwasiliana na wewe ili tupate maelezo ya kina juu ya hili. Ili tujue imefanyika Mwaka gani na Wahusika wote na vielelezo kama unavyo.

Tutumie PM au email ili iweze kufanyiwa kazi haraka sana.

Asante kwa kupaza sauti.
 
Haya mambo yasikieni tu. Siku moja binamu yangu ananipigia simu usiku wa manane analia vibaya mno, mwalimu wake anadai bila mapenzi hakuna kuchomoa.

Imagine, huyu binti by the tiime anafikisha miaka 8 alishapoteza wazazi wote. Amepambana sana kusoma, Alifanya vizuri sana form 4 mpaka akapambata scholarship A Level hapa hapa Tanzania. Yuko mwaka wa 5 medicine, pumbavu mmoja anataka kumkwamisha. Long story short tulishughulika na mwalimu, binti akamaliza chuo leo anatibu watoto. Lakini nikawaza kitu kimoja, huyu ana bahati ya kuwa na na watu wa karibu wenye uwezo wa kumpambania, vipi watu wengine?

Mimi mwenyewe wakati niko chuo kidogo nipate matatizo, kisa na-date na mwanafunzi anayetakwa na mwalimu. Mwalimu anampa tabu demu wangu, kisa anamfundisha, mimi ananipa tabu kupitia walimu wenzake, kwa sababu alikuwa hanifundishi. Kilichosaidia ni mwalimu alisimamishwa kwa kesi nyingine ya kudai rushwa ya ngono.

Hili jambo ni janga kubwa sana, hasa hasa elimu za juu. Yule Lecturer Vicensia Shule alipotaka kulivalia njuga, wakawahi kumziba mdomo. Inashangaza sana, waziri wa elimu mwanamke tena mwalimu wa chuo, she should know haya mambo, maana sio siri, walimu washenzi wanajulikana. Waziri wa maendeleo ya jamii mwanamke, mnafanya nini kulinda haki za wadogo zetu wa kike.

Serikali inapaswa kutangaza Rushwa ya ngono vyuoni kuwa ni janga, waunde tume ikusanye taarifa kuhusu hili jambo, zifanyike survey za siri za kutosha tujue ukubwa wa tatizo; then tuone nini kifanyike. But we have a big problem.
 
Mkuu, unaweza kutusaidie kumfikia huyu mtendewa? Tushikamane kutokomeza rushwa ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia.

Karibu PM mkuu, Tutashukuru sana.
 
Hizi rushwa za ngono vyuoni ndio sababu inayochochea wanaume wengi kuoa walioishia sekondari, Chuoni lecturer anageuka kuwa mungu mtu, dem akikataa kumpa kitumbua lecturer anampa supp kama trailer na movie inaanza dem akiendelea kukataa unapewa carry na hatimae anadisko.

Naombeni tujulishane wale ma lecturer waliokamatwa kwa rushwa ya ngono wapo wapi kwa sasa, isije ikawa bado wanaendelea na kazi hii kunyanyasa wanafunzi.

Iwekwe sheria lecturer akiomba rushwa ya ngono ihesabike kwamba AMEBAKA ale mvua ya miaka 30 jela....uhakika tabia hii itapungua kwa kazi ya ajabu
 
Pole sana. Hapo rushwa ilitembea kwasababu ubakaji hauna umri. Kubaka ni kumuingilia msichana au mwanamke bila ridhaa yake. Jaribu kufufua kesi upya, kama mshitakiwa yupo hai basi atashitakiwa. Inasikitisha sana
 
Daaahh, pole sana mama.
Inasikitisha sana, hapo rushwa ilishatumika hadi haki ikakosekana
 
Yupo sawa 5W +H kila Mkoa na Wilaya PCCB wapo Sasa ishu ya Mbeya ina haja gani kufanyiwa uchunguzi na PCCB-HQ? Ulipo wapo
 
Pole sana. Hapo rushwa ilitembea kwasababu ubakaji hauna umri. Kubaka ni kumuingilia msichana au mwanamke bila ridhaa yake. Jaribu kufufua kesi upya, kama mshitakiwa yupo hai basi atashitakiwa. Inasikitisha sana
Tatizo nipo maporini ila nashukuru hili dirisha limefunguliwa tuone tutafika wapi. Mwanangu kaambukizwa, tumetibia kapona lakini jeraha la moyo haliponi.
 
MtamaMchungu,
Ni mwaka wa kumi nafanya kazi za utawala katika elimu ya juu. Shida kubwa hizi kesi zinapotaka kushughulikiwa, wanafunzi huwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa hofu ya kwamba huko mbeleni atakwamishwa. Lakini in reality hakuna mtu anaweza kukukwamisha kwasababu tu ulimreport. Kuna haja kubwa kwa wanafunzi na jamii kujengewa uwezo na kujiamini ili kutoa taarifa za matukio kama haya.
 
hii scenerio mm pia ilinikuta chuo flani, mbaya zaidi nilikua na mahusiano na bint ambaye tupo same class na fani moja. Aisee walimu walinisumbua sana ila nilihakikisha nasoma sana ili kama wakinifelisha iwe ni kwa dhamira yao.

Yule dada (ambae sasa ni mke wangu) wakati tunamaliza chuo last semester lecturer akamkamata makusudi ili akirudi kufanya supplimentary amdake (maana wakati tukiwa bado chuo nilikua simuachi yule bint sababu nilijua anything kikitokea kwake nitakua responsible.) So ulipofika muda wa kufanya supp. nikampiga kizinga mzee nikapata nauli plus matumizi nikaibuka chuoni kumsaidia bint kusoma kwa ajili ya supp.

Lecturer alipomuona bint akamuita akamwambia amtafute apewe pepa ili aisome kabla ya mtihani. Bint akanifikishia taarifa mzee nikaambatana nae jamaa kutuona tupo pamoja akatoa udhuru then akapotea mazima. Thanks God bint alifaulu na now tunalea familia.
 
Katika kijiji cha Tella Mande kilichopo wilaya moshi vijijini kata ya old moshi, kaskazini mwa mji mdogo wa Kiboriloni upo mradi wa maji wa 900m ambao umesimama kwa hujuma ya mkandarasi na wahandisi wa maji. Walitandika mabomba undersize na wananchi walipopiga kelele wakayatoa na hawajaleta mengine na site hawaonekani.
Ofisi ya mradi iliyotarajiwa kugharimu 50m kama ilivyo kwenye andiko ndio kichekesho kama inavyoonekana hapa.
Wahusika wooote. Kimyaaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angepeleka huko PCCB wangemuomba rushwa ya ngono pia ili wayashughulikie madai yake, bora alivyosambaza kwenye mitandao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…