JamiiTalks Tutumie taarifa za Rushwa ya Ngono na Unyanyasaji sehemu ulipo, ili Mamlaka za Serikali zizifanyie kazi

Ahsante kwa kujioambanuwa mkuu.
Ebu naomba utuweke wazi kwa muda wa miaka kumi ukiwa kwenye kitengo cha utawala, Je hizi tuhuma ni kweli zipo?
Na kama zipo, ninyi kama utawala mmefanya juhudi zipi ili kuhakikisha mnakomesha ama kutokomeza rushwa ya ngono?
Na Je, ninyi kama wazazi mlifanya bidii zipi pamoja na kukusanya ushahidi wa kimazingira, pamoja na kulinda usiri wa shahidi/mkosewaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia wasituchanganye sisi tunaokula "matunda" kimasihara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee..... kama ndio hivi basi hao waomba,rushwa watakoma...Maana kwa kasi hii ya mabadiliko ya technology..hakiyanani tena Jela watakwenda wengi....Wakati una muomba mtu rushwa kumbe mwenzio ana record maongezi yenu iwe kwa,njia ya sauti.video.au text......

Aisee yajayo yana furahisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee.... hao police wahesabu kwamba kazi hawana tena... hii taarifa ikimfikia kangi kugola wameisha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,

Salaam. Watu kama nyie ni muhimu sana katika nchi hii.

Tunaomba haya maelezo uyapost kwenye hii thread hapa chini ili yaweze fanyiwa kazi na Serikali kuu. Umefanya vizuri sana kuongelea hili swala.

Hapa tunaomba taarifa za Rushwa ya Ngono na unyanyasaji kijinsia.

Karibu karibu sana.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo sio kuripoti,tatzo ni usalama wa aliyetoa ripoti au fununu

nijuavyo afrika hakunaga siri ,utawala wa sheria haufuatwi na wenye mamlaka, sasa kama hili halipo usalama wa mtu pia upo hatarini...
 
Hivi kweli kuna rushwa za maana za ngono, au ni kwaajli ya kukomoana tu?

Tuchukulie juzi yule mzee alikuwa rector wa cho gani sijui!

Kategeshewa kasichana kanafunzi kake, kisha kuishia kuaibishwa na mauzee yote hayo.

Hizi rushwa za ngono za kulengeshewa sheria ziangaliwe upya, mtatumaliza wanaume.

Maana mtu hauna hili wala lile, unakuta mwanamke anajilengesha kumbe katumwa ili akunase uingie kwenye mtego wa simba!

Na kukiwa na kuogopana kati ya mwanamke na mwanaume, dunia hii itakuwa ni tambara bovu ambalo halifai hata kwa kupigia deki siwafichi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tahadhari ichukuliwe katika kufanyia kazi hizi cases ili tuseje tukasababisha madaktari wakawa frustrated kisa watoto wenyewe ambao wanatumia papuchi kama kinga yao ya kupata upendeleo katika kila kitu na kila huduma. Wahadhiri na madaktari ni watu muhimu sana. Siyo vizuri kukurupuka katika kuyashughikia cases na tuhuma Kama hizi. Umakini unahitajika ili kuepuka kubomoa badala ya kujenga. Mimi naona wizara ya afya iendelee kusisitiza matumizi ya kinga.
Mwanamke aruhisiwe kufungua kumshitaki mwanaume atakayekataa kutumia kinga.
BTW penzi la kulazimisha halinogi. Inawezekana hao wadada wanakubali mambo, then wasipotimiziwa ahadi zao wanaamua kuwaumbua wadeni wao.
Wanawake ni wengi jamani huku Mbeya. Sio vizuri kumlazimisha mmoja asiyekutaka au kuomba Rushwa ya ngono. Halafu wanawake wa Mbeya sio wagumu kiasi ya madaktari kuwa na ukame wa papuchi kiasi hicho.

Haya mambo huwa yananichanganya.
 
tatizo sio kuripoti,tatzo ni usalama wa aliyetoa ripoti au fununu

nijuavyo afrika hakunaga siri ,utawala wa sheria haufuatwi na wenye mamlaka, sasa kama hili halipo usalama wa mtu pia upo hatarini...
Hapana mkuu, ndo maana tukaomba tutumiwe sisi JamiiForums. Ni rahisi kifuatilia na kumpa mrejesho mhusika. Mambo yamebadilika. Usiwe na hofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni mwanaume kuendelea kuwa king'ang'anizi, mwanamke akikukataa mwache na sio kumtishia kuharibu maisha yake.
 
Dah,aisee pole sana Mkuu
Mke wangu anakwamishwa sana na lecturers wanamnyima marks 1 ili kuvuka grade hivyo husababisha arudie mara ya 3 sasa toka 2016 sijui wanataka nini hao walimu maana huwa ni marks 1 tu hata akifanya appeals hapiti

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using my 6x6 bed.
 
Mkuu uwezo mdogo wa binti isiwe sababu ya kumnyanyasa kingono ama kijinsia.Kuna watu mmezoea sana kutumia fursa kama hizi kunyanyasa mabinti mnaodhani hawana uwezo.

Utakuta unamdhalilisha hadharani,kwa matusi na dhihaka ili ajisalimishe kwako.Badala ya kumtia moyo afanye vizuri ,kitendo cha kumshusha na kumfanyia psychological torture,humfanya azidi kukata tamaa.

Ndio maana naamini wakufunzi wanaofanya hivi hawastahili kabisa kuwepo sio tu chuoni,hata duniani.Wakati mwingine mtu anaweza kuwa na uwezo mdogo darasani kutokana na mambo mengi ya kijamii yanayomkabili.Utakuta nyumbani anaishi na mama na wadogo zake tu na wakati yeye yuko Chuo huenda nyumbani ni wagonjwa na hawana pesa ya kujitibu.

Wewe kama mwalimu unamuhukumu kwa kumdhalilisha.Hii tabia haivumiliki
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo siyo ukame,shida ni tatizo la kisaikolojia mtu kuona yeye msomi kwa nini akataliwe na kiumbe yoyote!
Anajiuliza mtu kama diamond hakuna mwanamke anamkataa kwa nini yeye akataliwe,ndo ubabe unapoanza Midimay,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…