JamiiTalks Tutumie taarifa za Rushwa ya Ngono na Unyanyasaji sehemu ulipo, ili Mamlaka za Serikali zizifanyie kazi

Midimay,
Kiongozi ni kweli wenda mbeya kuna wanawake wengi ambao pia unadai sio wagum ila ijulikane kua ipo tabia binadam akisha jijengea hawezi acha thats unakuta mtu mzima na akili yake anabaka mtoto wamiaka mitano na hapo ndo unajiuliza zaidi kwamba ni raha gani huyu mtu anapata na je ni kweli katika maeneo haishiyo kweli hakuna wanawake watu wazima wenzake.

Nafikili kwa sasa kwa hali ilivyo ni mda muafaka selikari kuja na mbinu muhafaka ambayo itaweza kulinda hadhi ya vijana wetu wasionewe kwa rushwa za ngono na wakati huo pia madactari wasionewe ila haki itendeke mfano hata ilo la mbeya naamini selikari kwa kutumia vyombo vyake vya uchunguzi wataweza jua mambo mengi maana haiwezekani mtu from no where akaleta malalamiko kama yale bila kutomanisha kwa vyovyote vile anamanisha wala sio kichaa
 
Lecturers au walimu wa shule hawaruhusiwi kutongoza wanafunzi. Wao ni walezi wa wanafunzi hao kitaaluma na kijamii. Conflict of interest. Haja zako za kimwili kamalizie kwa wasiowanafunzi au deal na wafanyakazi wenzio.
 
Sakasaka Mao,
Rector alitakiwa astick kwenye maadili ya kazi yake hasa ukizingatia nafasi yake kama kiongozi wa chuo. Alipoona jambo hilo alitakiwa amkemee mtoto huyo kwa sauti ya mzazi. Huyo rector kujilegeza inaonesha ni mshenzi wa tabia wa siku nyingi tu, alikuwa anatafutiwa 40 yake.
 
Mwaka wa kumi ndio nyie mmetufikisha hapa. Hakuna mlichofanya. Pisheni wengine wapige kazi.

Eti watu hawajiamini Unaongea utumbo sana bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ni jambo gumu kidogo. Kuna kitu wenzetu wanaita "Power Dynamics in relationships". Unapokuwa na watu wawili wako kwenye taasis moja au shughuli zao zinaingiliana, na ikatokea mmoja ana nguvu kuhusu shughuli za mwenzake, mahusiano huwa hayakatazwi lakini hayashauriwi; not forbidden but not encouraged.

Shida inaanza hapa, wewe mwalimu ni kweli umempenda mwanafunzi kutoka moyoni, na inawezekana mwanafunzi naye kakupenda pia; lakini inawezekana mwanafunzi "kakupenda" sio kwa sababu ya mapenzi, lakini ni kwa sababu ameshaona wenzake waliowakataa walimu walivyopata shida. Kwahiyo akaona ni bora tu "nimpende" mwalimu. Ukakasi unakuja hapo, kwamba nguvu uliyonayo juu ya huyu mwanafunzi au secretary wako ni kubwa mno, kiasi kwamba hatuwezi kuwa na hakika; amekupenda kweli, au ameshakuwa mateka wako.

Kuna baadhi ya makampuni makubwa, yamekataza kabisa relationships kati ya subordinates, kwa kuogopa hili jambo. Anakupenda kweli, au ukimtongoza unatupia na "miaka mitano kwenye chuo ni mingi sana kupoteza" au "unajua mtaani kugumu sana". Ndio maana kunahitaji sera kuhusu haya mambo, kwa mfano vyuo vingekuwa na dawati la jinsia kama ilivyo polisi, binti kama yuko uncomfortable na kutongozwa na mwalimu na anashindwa kusema no kwa mwalimu; akaripoti huko. Chuo kimwambie ticha knock off

McDonald's boss Steve Easterbrook fired after dating employee

Intel chief Brian Krzanich resigns over relationship
 

Mkuu, tufanye nini ili utuamini?

JamiiForums ni mtandao wa kijamii maarufu zaidi nchini Tanzania ulioanzishwa rasmi mwaka 2006 mwezi Machi ikiwa na waanzilishi wawili, Maxence Melo na Mike Mushi
 
Kweli kunahitajika ushahidi maana watuhumiwa wanetajwa live wana famili ni wazi watakuwa wamefedheheka sana. Mtoa tuhuma ajitokeze na kutoa ushahidi vinginevyo ni udgalilishaji kwa watuhumiwa na familia zao. Fikiria mme, babako, ba mkwe, kaka, shemeji anaanikwa hadharani namna ile kuwa anaomba na kulazimisha rushwa ya ngono? So bad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ishu ni nzuri sana japokuwa uchunguzi nao usiachwe nyuma hata mimi wakati nasoma chuo kuna lecture alikuwa anamtesa mdada wa watu kwa kumpa ma sup kwa sababu ya kumdaka ili amuachie mzigo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Peleka ushahidi na umwambie huyo mdada ajitokeze tuhuma zote huchunguzwa hata kama ni za muda mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini mnanyamazia taarifa hizi? Bado huyo mwl anaweza kuchukuliwa hatua endapo huyo binti atajitokeza kutoa madai ya kudhalilishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kuna wanaochangia bila kuusoma huo uzi mngeuacha hewani wakuu waupitie ndipo wachangie vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya sasa wahusika hili nalo lifuatiliwe. Zinafunguliwa kesi za vita ya kwanza na ya pili itakuwa hii. Serikali ina macho makali na mikono mirefu hilo nalo lisiachwe likapita. Wengi wameumia sana lakini walikuwa hawana mahali pa kusemea. Jf ndipo mahali sahihi pa kulia kilio chako chote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana. Hakuna jiwe litaachwa bila kugeuzwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…