JamiiTalks Tutumie taarifa za Rushwa ya Ngono na Unyanyasaji sehemu ulipo, ili Mamlaka za Serikali zizifanyie kazi

Wachunguzi wa hizi kesi usikute nao walipata ajira kwa njia hizo hizo

Rushwa ya Ngono haina tofauti na Ubakaji,sii Ridhaa ya mhusika (mfanywaji) ,ni jambo baya kwa wale wanao Heshimu Utu wao.
 
Midimay,
Nimesomea vyuo vya Medicine, masomo ya Medicine ni magumu kwa wanafunzi wa Jinsia zote. wanafunzi wa kiume wakikamatwa hawana kisingizio, lakini wanafunzi wa kike wakikamatwa wanasingizia kuwa kufeilishwa kwao kunasababishwa na walimu kutaka rushwa ya ngono. Je, wanafunzi wa kiume wakifeli mwalimu anataka rushwa ya nini?
 
Mtoa tuhuma za rushwa ya ngono Mbeya, Alitengeneza tuhuma za kuchafua na kuwakomoa walimu kwa kuwataja majina yao kwa hisia tu. Kwani hakutoa uthibitisho kuwa amewahi kutoa rushwa ya ngono.

Kwenye tuhuma zake anamtuhumu Mkurugenzi wa Hospitali ya rufaa ya Kanda Mbeya, lakini pia bila uthibitisho wowote kuwa Mkurugenzi amewahi kupelekewa malalamiko hayo.

Ni vema angejitokeza kutoa maelezo yasio acha mashaka ya kukomoana hasa kwenye Serikali hii ambayo inapenda kutoa maamzi yanayolenga kuifurahisha hadhala bila kujua ukweli.
 

Isiishie hapo tu, hata zile rushwa za uchaguzi ili ccm wapite bila kupingwa uwekwe wazi. Haya mambo yako wazi na huwa tunasema, ila kwakuwa viongozi waandamizi wanafaidika na hizo rushwa wanakaa kimya, na takukuru ikifika hapo wanajificha au wanatumia nguvu ndogo kuzuia hilo.
 

Mfumo wa mahakama sio rafiki kwa raia wa kawaida. Kuna changamoto kubwa kwenye mfumo wa kupata haki ndani ya mahakama zetu. Ukitaka kuamini nenda magereza ukaone utitiri wa mahabusu, na kikwazo ni mfumo mzima wa kupata haki.
 
Tatizo ni mwanaume kuendelea kuwa king'ang'anizi, mwanamke akikukataa mwache na sio kumtishia kuharibu maisha yake.
Mkuu kweli wanaume tumetofautiana! Anikatae mwanamke halafu nimtishie!
Dah! Sasa huo ndiyo ubazazi kamili!

Penzi linatishiwa! Sasa hiyo furaha inayotafutwa kwenye penzi, itapatikanaje hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JamiiForums, Tatizo whistle blowers wengi wanaishia kupata matatizo.

Kwanini msifanye kazi kama FBI, ukipata tip unaifanyia kazi kimyakimya.

Wengine wamejaribu hata kupiga picha maeneo wanaishia kusikojulikana na kesi kibao.
true
 
Wilaya ya same mkoa wa Kilimanjaro kwenye kata moja huko milimani kuna shule moja team ya waalimu wa kiume wamewageuza wanafunzi wa kike mateka wa kimapenzi. Sio mwanafunzi mmoja au wawili. Nikiwa kwenye mood ntaandika
 
Kwenu JF. Kuna tukio la mfanyabiashara mmoja Bwana Noa mkazi wa huko Orkasmet Simanjiro anatuhumiwa kufanya ulawiti wa mtoto wake wa kumzaa mwenye umri usiozidi miaka 5.
Taarifa zinabainisha kwamba Bwana Noa alikuwa akimuingilia mtoto wake pindi mama yake akienda kwenye shughuli za mgahawa alfajiri. Taarifa pia zinadai baada ya mama wa mtoto kubaini unyama huo usioweza kuvumilika kwa mtoto wake aliripoti polisi Simanjiro na kufungua jalada. Baada ya kufungua / Kuripoti tukio hilo mtuhumiwa inadaiwa alikimbia na kumekuwa na juhudi za pande zote mbili za wazazi kutaka kesi hii imalizwe kifamilia ilihali mtoto ameharibiwa vibaya kutokana na ripoti za daktari aliyemfanyia uchunguzi. Kutokana na mama wa mtoto kutokubaliana na upande wa wazazi alifukuzwa nyumbani na yeye kuendelea kufuatilia haki ya mtoto wake kisheria. Jitihada za mama wa mtoto mnamo tarehe 06.01.2020 zilizaa matunda kwa mtuhumiwa kukamatwa huko Makao mapya Arusha na kufikishwa kituo kikuu cha polisi Arusha. Taarifa hizi nadhani zitasaidia kufanya haki ipatikane kwa mama na mtoto kwa inaonekana kuna juhudi za kutumia pesa kukwepesha ukweli. Taarifa zaidi zikipatikana zitawekwa kwani hili jambo linaumiza mno kwa kulisikiliza tu maana mtoto sasa hivi inadaiwa anataka kufanyiwa kama baba yake alivyokuwa anamfanyia na pia inaelezwa mtoto kwa sasa ameharibika sehemu zake za haja kubwa. CC. JamiiForums
 
Yule Mwalimu wa shule ya msingi ya ST. FROLENCE ya mikocheni mjini DSM aliyetuhumiwa Kubaka wanafunzi waliokuwa wame kwenda safari ya kishule, kesi yake imeishia wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…