Imalamawazo
JF-Expert Member
- Jul 27, 2021
- 1,343
- 3,269
1. Utangulizi
Inawezekanaje tutumie vyuo vikuu kukabiliana na tatizo la ajira ikiwa wahitimu wa vyuo hivyo ndilo kundi linaloongoza kwa kusota mitaani bila ajira?
Japo ni kweli kuwa tatizo la ukosefu wa ajira nchini linadhihirika zaidi miongoni mwa wahitimu wa vyuo vikuu, ni vyema tukataraji pia kuwa suluhisho la ajira kwa vijana hawa litapatikana vyuo vikuu.
Taraja yetu inatokana na utayari wa wahitimu wengi kutosubiri ajira kwenye fani walizozisomea badala yake wanapambana kusaka ujuzi mbadadala nje ya fani zao. Tumekuwa tukishuhudia wahitimu walijitokeza kuomba nafasi za mafunzo ya ufundi stadi (VETA) yanayogharamiwa serikali. Lakini pia wapo wahitimu wanaojifunza mitaani ufundi makenika, mbinu za kilimo, ufugaji wa kisasa, usafirishaji n.k kutoka kwa wenzao wasio na elimu ya juu.
Taswira kubwa tunayopata hapa ni kuwa wahitimu hao wanahangaika kujifunza upya stadi ambazo walipaswa kuwa wamejifunza katika safari yao ya kielimu. Lakini pia wakishatatua chngamoto ya ujuzi wanakumbana na changamoto nyingine hasa hasa ukosefu mitaji. Makala hii inapendekeza mkakati wa kukabiliana na ombwe la stadi na mitaji kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu kwa kuhusisha vyuo vyenyewe na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
2. Vyuo vikuu vifanye nini cha ziada?
Chuo kikuu ni sehemu ya kupata maarifa na ujuzi wa kila namna kupitia mifumo na taratibu zilizowekwa. Taratibu hizo kwa namna moja au nyingine zinarahisisha mwanafunzi apate maarifa nje ya shahada aliyodahiliwa kwayo, mhitimu anapata shahada yake pamoja na kitu kingine cha nyongeza. Kutokana na urahisi huo makala hii inapendekeza mkakati maalumu utakao vifanya vyuo vikuu kuanza kutoa shahada na stadi flani ya nyongeza kwa wanafunzi wake, kwa urahisi tuuite, Shahada++.
Vyuo vikuu vinazo fursa za kutekeleza miradi kama hii bila kuathiri mitaala yake wala pasipo kuhitaji kurekebisha mitaala na mifumo ya elimu za msingi na sekondari. Mfano, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na taasisi ya Empower inaendesha program ya Generation Empower inayolenga kuwajengea wahitimu maarifa yanayohitajika karne ya 21 ili waweze kuajiriwa au kujiajiri (Generation Empower, 2020 Generation Empower Media Press Release | Empower imepatikana 27 Julai, 2021). Kumbe hata utekelezaji wa mkakati wa Shahada++ hautaonekana kuwa ni jambo geni katika uwanda wa kitaaluma nchini na duniani kote. Kupitia mkakati wa Shahada++ mhitimu atapata shahada aliyodahiliwa kwayo lakini pia atapata nafasi ya kujifunza stadi flani flani za nyongeza kulingana na hobi zake au fursa zinazopatikana maeneo yake.
3. Je, vyuo vikuu havitageuka vyuo vya kati?
Hapana: Mkakati wa shahada++ hautaingiliana na mafunzo yanayotolewa na vyuo vya chini au chini kwani mafunzo yatakayotolewa yatawalenga wanafunzi wa vyuo vikuu tu. Lakini pia mkakati huu unaweza kutekelezwa sambamba na program za vyuo vikuu pasipo kushusha ubora wa elimu ya vyuo husika. Katika kutekeleza mkakati huu, vyuo vikuu vitatakiwa kushirikiana na wadau kuandaa mitaala ya mafunzo ya stadi zinazotakiwa katika sekta ambazo zinazalisha ajira nyingi au sekta zitakazowawezesha wahitimu kujiajiri.
Mfano wa sekta hizo ni pamoja na ufundi stadi, kilimo, uongezaji wa thamani wa mazao ya kilimo, ufugaji, uchakataji wa malighafi kwa ajili ya viwanda, stadi za TEHAMA, mbinu za ujasiriamali, michezo, sanaa na kadhalika. Kwa hiyo wanafunzi watachagua stadi wazipendazo miongoni mwa stadi za ziada zinazotolewa chuoni kwao kuzingatia hobi zao na fursa zinazowazunguka katika mazingira yao. Kupitia Shahada++ vyuo vitazalisha wahitimu ambao wanajua stadi nyingi zitakayomwezesha kujiajiri na kuajiri wengine.
4. HESLB iwafikie wahitimu wanaotaka kujiajiri
Ili kuufanya mpango wa Shahada++ ulete matokeo tarajiwa ni lazima uambatanishwe na upatikananji wa mitaji. Lakini sehemu kubwa ya wahitimu wa elimu ya juu hawana mitaji wala dhamana zinazokubalika na taasisi za fedha. Katika huo mtanziko wa upatikanaji wa mitaji tunatambua kuwa HESLB ndiyo taasisi pekee itayokuwa ikiwadai wahitimu wa elimu ya juu pesa nyingi.
Isitoshe, HESLB ndiyo taasisi pekee ya kifedha inayoweza kuwaamini wanafunzi na kuwakopesha pesa bila dhamana. Hivyo basi HESLB haipaswi kuondoa imani kwa wanafunzi hao pindi wanapohitimu masomo na kuanza kupambana kupata kujiingizia kipato ambacho pia kitasaidia wahitimu hao kurejesha deni wanalodaiwa. Aidha, ni bora HESLB ikashiriki pia kuwajengea uwezo wa kiuchumi ili kukabiliana na changamoto ya ajira ili waweze kurejesha pesa hizo kwa wakati.
Kwa hiyo inapendekezwa, HESLB itoe fursa ya wahitimu wanaopenda kujiajiri kuomba mkopo usiopungua pesa yao ya boom ya mwaka wa mwisho wa masomo yao ili kuwafanya wahitimu hao waanze safari yao ya kujiajiri kwa kujiamini.
6. Ni nani anaweza kuanzisha utekelezaji wa Shahada++?
Mamlaka za vyuo vikuu, wadau wa elimu na serikali wanaweza kushawishi utekelezaji wa mkakati wa Shahada++. Mfano, serikali inaweza kuamua kutenga pesa kiasi kutokana na zile pesa ambazo zinapelekwa vyuo vya ufundi ikazipeleka pale chuo cha uhandisi pale Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuwataka waandae mafunzo ya ufundi mafupi kwa wanachuo wa shahada zisizo za uhandisi. Lakini pia serikali inaweza kuvipa fursa vyuo vingine vipendekeze mafunzo stadi ambazo zitagharimikiwa na serikali kutokana na maeneo yao ya umahiri kama ujasiriamali, sanaa, uandaaji picha na kadhalika.
Lakini pia wadau wa elimu wanaweza kushawishi taasisi mbalimbali ikiwemo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na kupeleka pendekezo la Shahada++ vyuoni kama namna ya kuvipa changamoto vyuo vikuu ili viweze kubuni njia za kuwasaidia wahitimu kukabiliana na changamoto ya soko la ajira. Hata serikali za wanafunzi zenyewe zinaweza kushirikiana na mashirika kama shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kuanza utekelezaji wa shahada++ kama mpango wa muda mfupi.
Hata hivyo, katika utekelezaji wa Shahada++ ni vema kutofautisha mkakati wa Shahada++ na zile kozi fupi mithili ya zile za Microsoft office zinazotolewa kwenye baadhi ya vyuo kwa wanafunzi nyakati za likizo fupi. Shahada++ inayopendekezwa inatakiwa irasimishwe na ngazi zinazo rasimisha mitaala vyuoni. Pia mwanafunzi asilazimike kulipa tozo ya ziada ili kupata mafunzo hayo ya ziada. Kwa hiyo kumbe siyo kila mtu anaweza kuwafanya hao wazee wa vyuo vikuu wakune vichwa vyao bali ni wadau wa elimu ya juu.
7. Hitimisho
Mkakati wa Shahada++ unaopendekezwa utatuwezesha kujaziliza ombwe la stadi kwa wahitimu pasipo kulazimika kufumua na kusuka upya mitaala ya shule za msingi na sekondari. Pia mkakati huu utawasaidia wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaodai kuwa wahitimu wa darasa la saba ni bora kuliko wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu nchini. Hivyo utaongeza hamu ya watu kupata elimu ya chuo kikuu, itapanua wigo wa wahitimu kujiajiri, itaongeza tija kwenye sekta za uzalishaji mali kama kilimo, ufugaji, usafirishaji, tehema na uzalishaji wa bidhaa.
Mwisho kabisa Shahada++ pia utasidia kujenga urafiki kati ya wahitimu na HESLB hivyo kuongeza ufanisi katika ukukusanyaji madeni.

Upvote
14