Tonytz
Senior Member
- Jul 18, 2022
- 159
- 1,142
UTANGULIZI
Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu kwa pumzi na uhai anaozidi kunikirimia katika maisha yangu yote. Pia nawaombea uzima na afya njema jopo zima la JF kwa kuweka jukwaa wazi kwa umma na hasa katika kuhaikikisha ajira kwetu Watanzania. Nawaombea afya njema na uzima waandishi wenzangu pamoja na wapiga kura wetu.
KWANINI YATUPASA KUWA WANYENYEKEVU KATIKA KUWAJIBIKA AU KUTUMIKIANA?
Hili ndilo swali muhimu sana linalobeba dhima ya Makala hii. Je kwa watumishi au watu wengine kuwa na unyenyekevu katika uwajibikaji kuna tija yoyote? Jibu ni jepesi kuwa ndiyo yatupasa kuwa wanyenyekevu katika kuwajibika kwetu kwenye nyanja zote za kiuchumi, kisiasa, kijamii na hata katika taasisi zote kwani ni kichocheo cha uadilifu na maendeleo na Amani ya Taifa.
Unaweza ukajiuliza kichwani kuwa unyenyekevu ni nini? Unyenyekevu ni hali ya kujishusha bila kujitazama binafsi(yaani bila kuwa mbinafsi). Unyenyekevu unamfanya mtu awe na tabia au mazoea ya kutenda mema kwake na kwa wengine bila kuweka mbele maslahi yake mapana. Tunapokosa unyenyekevu maana yake tunatawaliwa na ubinafsi katika maamuzi yetu ambapo hupelekea kuharibika kwa kazi na kuathiri mipango na malengo ya taasisi husika. Kukosekana kwa hekima, busara, uvumilivu, utii, kiasi, hofu ya Mungu katika maamuzi ya kiutendaji ni viashiria ya kutokuwepo kwa unyenyekevu kwa watu wengi hasa kwa waliopewa dhamana kutuongoza.
Watu wengi tumetawaliwa na ubinafsi katika maamuzi na hata katika utekelezaji wa miradi mbalimbali. Na mara nyingi ubinafsi ni pamoja na kutojijua, kutokukubali makosa na kuomba radhi au msamaha. Hii ina maana kuwa kujijua, kukubali makosa na kuomba msamaha ni ishara ya unyenyekevu katika kutumikiana kwetu. Kwa sasa siyo jambo la kushangaza kuona maofisini wafanyakazi wanaoneana chuki, wanasengenyana, wanatafutiana visa na wengine wapo mstari wa mbele kumfanya mfanyakazi mwenzake akutwe na tatizo na pengine kufukuzwa kazi, huu siyo uwajibikaji bali ni ukosefu wa maadili na unyenyekevu katika utendaji na uwajibikaji wetu.
Kwa kukosa unyenyekevu kwa watu waliotuamini au kutuchagua ili tuwatumikie kunapelekea kudidimiza maendeleo na kukiuka viapo vyetu kwa watu waliokupa nafasi ya kuwaongoza. Sambamba na hiyo hupelekea machafuko na kukosa kuaminiana. Kuwepo na watumishi maofisini wenye majivuno, jeuri, chuki, kupenda rushwa katika utoaji wa huduma, wizi au ufisadi na mengineyo yenye kufanana na hayo ni ishara ya uozo wa maadili ya kitumishi ambapo misingi yake ni kutokana na kukosa unyenyekevu. Ni ni wazi kabisa, kwani kuna viongozi au watumishi mbalimbali ambao wanatumia mamlaka zao kinyume na utaratibu, huu ni ukosefu wa unyenyekevu na badala yake ni ubinafsi wenye uadui ndani yake.
Kuna wanateolojia mbalimbali wameelezea kuhusu nguvu na fadhila hii ya unyenyekevu;
Ukirejelea hata katika vitabu vya kimungu (Biblia Takatifu) kuna baadhi ya wafalme hawakuomba utajiri kwa Mungu, bali hekima. Mfano mfalme Sulemani alipotokewa na Mungu alimuuliza unataka nikutendee nini? Mfalme akasema, naomba nijalie hekima na busara ili niweze kuliongoza kundi lako kubwa la watu ulilonikabidhi. Na Mungu akamjalia. Je, ingelikuwa wewe umetokewa katika hali yako ya ubinadamu basi ungeomba magari, mali nyingi na pengine kutaka hata fulani atoke kwenye nafasi ili wewe ukae, huo siyo unyenyekevu ndugu zangu.
Ukisoma kitabu cha Nabii Yoshua Bin Sira 3:18, anasema “ kadri ulivyo mkuu uzidi kujinyenyekesha” pia kitabu hicho hicho sura ya 10:1 anasema “ kadhi aliye na Hekima atawafundisha watu wake; na utawala wa mwenye ufahamu utakuwa na utaratibu”
Tujiulize hapa, je katika nafasi yako uliyonayo katika nyanja yoyote ile unajinyenyekeza au unawatumikia wengine kwa unyenyekevu? Huna uchu wa madaraka na tamaa ya mali? hupangi mipango ya taasisi kwa ubinafsi wako? Kama hayo hatutendi basi kuna unyenyekevu sana. Pendeni haki enyi waamuzi wa dunia. YESU alijishusha pamoja ya kuwa alikuwa mkubwa na mwenye mamlaka lakini aliwatumikiwa mitume wake kwa kuwaosha miguu yao.
Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE yeye alitambua kuwa kukaa Ikulu siyo kitu cha kung’ang’ania na hakihitaji mtu utumie nguvu, bali yeye aliamua kujenga nyumba yake Msasani, alipunguza wingi wa magari ya kumsindikiza katika misafara yake kwa nia ya kupunguza gharama na kutopenda sifa. Lakini alionyesha unyenyekevu kwa kuombwa kuachia madaraka na akakubali hii ni Zaidi ya unyenyekevu, kwani kwa karne hizi tazama viongozi wanavyobadilisha katiba ili kuzidi kuwapa nguvu za kubaki madarakani, wakati mwingine humwaga mpaka damu za watu kisa kung’ang’ania madaraka, tazama kiongozi hata akitoka Temeke kwenda Pugu mfuatano wa magari mpaka unatia hofu kwa raia. Baba wa Taifa letu la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere aliwatumikia watu wake kwa unyenyekevu mkubwa sana, hii ndiyo sababu hata ulimwengu mzima ulizizima.
Kutokana na maelezo hayo, je wewe unajionaje au watu wanawezaje kusema kuwa wewe ni mnyenyekevu?
TUTATAMBUAJE UNYENYEKEVU KATIKA UWAJIBIKAJI WETU?
Viashiria vifuatavyo vitatuwezesha kutambua unyenyekevu alionao mtu;
HITIMISHO
Kuna mambo kadha wa kadha ya kuzingatia baada ya kusoma Makala hii. Jambo ka msingi hapa ni kuwa yatupasa kuwa wanyenyekevu lakini haina maana kuwa mtu ajiweke nyuma kwa vipaji alivyonavyo. Mtu anapaswa aheshimu mambo mazuri ya wengine ambayo yeye hana, na atambue udahifu uliopo ndanimwe. Zingatia, “Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu- Yakobo 4: 6.
video: mtandaoni (youtube)

- Mtakatifu Augustino alisema “ kiburi kiliwabadili malaika kuwa mashetani na unyenyekevu unawabadili watu kuwa malaika”
- Mtakatifu Philipo Neri alisema “ bila unyenyekevu hakuna ukamilifu”
- Tom wa Kempis alsema “ namna ya kuwa mnyenyekevu ni kuwa na lengo katika kipimo yaani kiasi au thamani”
Ukirejelea hata katika vitabu vya kimungu (Biblia Takatifu) kuna baadhi ya wafalme hawakuomba utajiri kwa Mungu, bali hekima. Mfano mfalme Sulemani alipotokewa na Mungu alimuuliza unataka nikutendee nini? Mfalme akasema, naomba nijalie hekima na busara ili niweze kuliongoza kundi lako kubwa la watu ulilonikabidhi. Na Mungu akamjalia. Je, ingelikuwa wewe umetokewa katika hali yako ya ubinadamu basi ungeomba magari, mali nyingi na pengine kutaka hata fulani atoke kwenye nafasi ili wewe ukae, huo siyo unyenyekevu ndugu zangu.
Ukisoma kitabu cha Nabii Yoshua Bin Sira 3:18, anasema “ kadri ulivyo mkuu uzidi kujinyenyekesha” pia kitabu hicho hicho sura ya 10:1 anasema “ kadhi aliye na Hekima atawafundisha watu wake; na utawala wa mwenye ufahamu utakuwa na utaratibu”
Tujiulize hapa, je katika nafasi yako uliyonayo katika nyanja yoyote ile unajinyenyekeza au unawatumikia wengine kwa unyenyekevu? Huna uchu wa madaraka na tamaa ya mali? hupangi mipango ya taasisi kwa ubinafsi wako? Kama hayo hatutendi basi kuna unyenyekevu sana. Pendeni haki enyi waamuzi wa dunia. YESU alijishusha pamoja ya kuwa alikuwa mkubwa na mwenye mamlaka lakini aliwatumikiwa mitume wake kwa kuwaosha miguu yao.
Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE yeye alitambua kuwa kukaa Ikulu siyo kitu cha kung’ang’ania na hakihitaji mtu utumie nguvu, bali yeye aliamua kujenga nyumba yake Msasani, alipunguza wingi wa magari ya kumsindikiza katika misafara yake kwa nia ya kupunguza gharama na kutopenda sifa. Lakini alionyesha unyenyekevu kwa kuombwa kuachia madaraka na akakubali hii ni Zaidi ya unyenyekevu, kwani kwa karne hizi tazama viongozi wanavyobadilisha katiba ili kuzidi kuwapa nguvu za kubaki madarakani, wakati mwingine humwaga mpaka damu za watu kisa kung’ang’ania madaraka, tazama kiongozi hata akitoka Temeke kwenda Pugu mfuatano wa magari mpaka unatia hofu kwa raia. Baba wa Taifa letu la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere aliwatumikia watu wake kwa unyenyekevu mkubwa sana, hii ndiyo sababu hata ulimwengu mzima ulizizima.
Kutokana na maelezo hayo, je wewe unajionaje au watu wanawezaje kusema kuwa wewe ni mnyenyekevu?
TUTATAMBUAJE UNYENYEKEVU KATIKA UWAJIBIKAJI WETU?
Viashiria vifuatavyo vitatuwezesha kutambua unyenyekevu alionao mtu;
- Kusikiliza shida za wengine na kuzitatua pasipokuweka maslahi mbele
- Kujijua, kukubali makosa na kuomba msamaha
- Kuwa mkweli na muwazi na busara
- Kuwa na heshima kwa watu wote na ibada kwa Mungu
- Kutoa huduma kwa watu bila majivuno
- Kukubali sifa kwa huduma nzuri na bors unayotoa
- Kukubali kuteseka kwa ajili ya makossa yaw engine
- Kuwasifu wanaostahili.

Upvote
86