Tuujadili uchumi katika vitabu vitakatifu.

Tuujadili uchumi katika vitabu vitakatifu.

RAGNAR LOTH

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
698
Reaction score
1,589
Natumai nyote mu-buheri wa afya Enyi wana wa nuru.
Nimeona ni jambo la kheri tukageuza macho yetu katika vitabu vitakatifu tuone Mwenyezi Mungu anatuasa nini kuhusu swala zima la uchumi. Na zaidi kukujulisha tu Ewe mwana mwana wa Adamu ni kwamba maarifa yaliyomo katika vitabu vya kidunia msingi wake ni hivi vitabu vya Mungu.

Kwa kuwa mimi ni mfuasi wa Kristo nitajikita kuchambua Bibia Takatifu, lakini kama unatofautiana nami si vibaya ukaja na uchambuzi wako wa vitabu vya imani yako ukatuongezea maarifa. Lengo langu si kuanzisha kashfa,matusi na ubishi usio na msingi bali ni kuelimishana tu. Ukiona natofautiana na wewe ni vyema ukatumia staha kunijibu na si maneno makali.

Karibuni sana.
 
KITABU CHA MWANZO ( GENESIS )

1 : 2-3

" Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilkuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mwenyezi Mungu akasema, iwe nuru; ikawa nuru. ............."

SOMO I.
Hapa tunaona "Roho" ( spirit ) ndio muumbaji wa kwanza, na sio mwili. Kila binadamu ana Roho ( spirit ), kwa sababu binadamu wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Kama Mungu aliweza kuumba Mbingu na nchi kutoka kwenye "Hakuna", "out of nothing" kwa kutumia Roho yake basi hata sisi pia tuna uwezo wa kuumba ( create ) kitu chochote kisichokuwepo, kikawepo kama tu Roho zetu zitakuwa hai.

Ndani ya Roho kuna " imani ( belief / Faith )", kama roho yako haina imani, hiyo Roho imekufa, wazungu wanasema "If you have no belief / Faith in you then your spirit is dead".

Wengi tuna ndoto nyingi kama sio moja, lakini tunakosa imani ndani ya roho zetu ya kuumba, tunashindwa kuzileta ndoto kwenye uhalisia ( We fail in most cases to make our dreams into reality ). Wanasema ukiamini kitu kiwe kinakuwa, tunaamini kabla ya kuona na sio tuone kwanza ili tuamini.

Kama unatamani kuwa mfanyabiashara, unachotakiwa ni kuamini kwamba wewe tayari ni mfanyabiashara na nakwambia lazima utakuwa mfanyabiashara. Ukiamini nitazalisha na nitauza lazima utauza, Imani inaumba wakuu. Vitabu vya kidunia vimechota haya maarifa huku na kutengeneza kanuni inayoitwa " Law of attraction " mkaitafute kama mtapenda sitailezea hapa.

Imeelezwa vizuri kwenye kitabu cha Napoleon Hill " Think and grow rich ", kitabu kizima kinaelezea hii kanuni. Hakuna Tajiri yeyote katika hii dunia asiyelijua hili. Donald Trump katika vitabu vyake vyote " Art of the deal, Great again, How to get rich " hakosi kuitaja hii kanuni. Nimekuwekea na video yake hapo chini akithibitisha hayo kama tu usipoamini nikisemacho.


SOMO 1I.

Mstari wa tatu tunaona Roho ya Mungu inasema " Iwe nuru, inakuwa nuru. na vitu vyote vinaumbwa kwa neno la mdomo ( by the word of mouth ).

Wahenga wa kiswahili waliposema " Maneno yanaumba / Mdomo unaumba ", hawakudanganya. Hapo ni kwamba maneno na roho vinamawasiliano, ni two way process. Ni kwamba unachokiamini ndani mwako ndicho kinachotoka mdomoni ( in most cases but not all the cases) na unachokitoa mdomoni ndicho kinachojengeka ndani mwako.

Ukisema lazima nianguke utaanguka, ukisema lazima nifanye utafanya, ukisema lazima kiwe kitakuwa. Tunatakiwa tuwe chanya muda wote tunapoongea jamani, tusiwe hasi kwa maneno tunayoyatoa. Maneno yanaweza kuamsha imani ya roho lakini pia yanaweza kuua imani ya roho.

Kufaulu na kufeli katika uchumi inategemeana sana na unachokiongea pia mdomoni.


1 : 28
Moja ya vitu Mungu anayoviumba ni sisi wanadamu. Akatutuma akasema " Zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

SOMO I
Hapa kwa upande wangu maneno wawili yamenivuta kuyatafakari kama mchumi / Mfanyabiashara nayo ni " KUITIISHA na KITAWALA KILA KIUMBE ". Kila mfanyabiashara ni kiongozi, kila mfanyabiashara lazima aijue sanaa ya kuongoza watu ( Art of leadrship ). Bila hiyo huwezi kufika popote. Katika hiyo sanaa ya uongozi kuna kitu pia kinaitwa "ushawishi".

Tulipopewa agizo kwamba tutawale kila kiumbe Mungu hakumtoa kwenye hilo kundi la "viumbe" yeye mwenyewe binadamu. Kwa hiyo binadamu ni moja ya viumbe vinavyotakiwa vitawaliwe na kutiishwa na binadamu mwenzake.

Katika maisha kila mtu ni kiongozi, kwenye familia, kazini, na kwingineko. Na kama tujuavyo binadamu ana utashi wa kung'amua na kuamua atakacho, kimfaacho. Ukichagua kuwa mfanyabiashara hukwepi kuwa mwajiri na kuongoza watu chini yako, uwatawale na kuwatiisha.
Na ukiamua kuwa mwajiriwa ina maana umechagua kutawaliwa na kutiishwa na kiongozi wako.

Waajiri ni jukumu lenu kujifunza zaidi namna ya kutawala na kutiisha na
Waajiriwa ni jukumu lenu kutawaliwa na kutiishwa na waajiri wenu.
Kila mmoja ana utashi wa kuchagua na kuamua nafasi anayotaka acheze hukatazwi kutiisha na kutawala lakini pia hukatazwi kutii na kutawaliwa.


TUKUTANE SURA YA PILI KATIKA KITABU CHA MWANZO: GENESIS CHAPTER 2.
( Itategemea na mwamko wenu, kama mtakuwa tayari kwa haya majadiliano tutaendelea pamoja).
 
Mbona kama umebase sana kwenye uumbaji mkuu....au ndio mwanzo?haya ngoja nisubiri....
 
Back
Top Bottom