ItsMi
Member
- Sep 13, 2021
- 66
- 31
Kwanza niseme kutoka moyoni kwamba sisi vijana tumekuwa ni tegemezi kubwa sana kwa jamii lakini kwa bahati mbaya wengi wetu hatuthamini ukubwa huu tuliopewa na jamii zetu.
Sasa lengo ni kwamba sisi tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kulipinga hili na sio vinginevyo
Tunapoona vijana wenzetu wametumbukia kwenye janga hili tusiwasifu kwa hilo ila tuwakanye kwamba madawa ya kulevya yanadidimiza nguvu kazi ya taifa na uchumi wetu kwa ujumla
Kwa kuwa tukishindwa kumshauri huyo mmoja aliye athirika na janga hili itakuaje kama ikatokea ataendelea kushawishi hata watu wengine wengi waliopo karibu yako.
basi kama ni hivyo utajikuta hata wewe umeanza kushawishika na kuziharibu ndoto zako ulizokua umejiwekea katika maisha yako
sasa tunatakiwa tutambue kwamba kila mmoja anayo ndoto ya kufika mbali kama vile ilivyo kwako kwa sababu huenda yeye pia aliteleza kwa bahati mbaya mara baada ya vishawishi vya makundi mbalimbali alivyokuwa akikutana navyo mara kadhaa
Kila mmoja ndoto yake ni kupambana dhidi ya umasikini na kama unavyojua huwezi kupambana vizuri ukishakuwa mraibu wa madawa ya kulevya tambua umri na miaka vinakimbia kwa kasi sana hivyo kama utaendekeza hali hii ni kwamba mafanikio yatakuacha mbali sana,
Hivyo ishi ndoto zako epuka vishawishi, ongeza juhudi, ongeza marafiki wanaofaa, katika kuhakikisha huishii hapo ulipo bali ufike mbali pia epuka tabia zisizofaa, na umtangulize mungu katika kila jukumu lako la kila siku kwa kuwa mungu hamtupi mja wake.
Na siku zote ishi katika fikra chanya kwa hakika utafika mbali katika kulijenga taifa.
Asante.