Tuungane na Burundi tuifaidi Congo

Tuungane na Burundi tuifaidi Congo

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Baada ya taarifa za kuwepo harakati za muungano wa Tanzania na Burundi. Ni wakati Sasa jambo hili lipewe nafasi na lifanyike Kwa haraka.

Jamii ya warundi ni tiifu Kwa Tanzania na miaka yote kuanzia raia mpaka serikali ya Burundi wamejiona salama chini ya Tanzania mpaka kufikia kuwa na kura ya pamoja katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Katika Kila jambo Burundi itasubiri kuona Tanzania imeamua nini na huo ndio itakua msimamo wao pia.

Hii ni utii wa halo ya juu. Muungano huanzia moyoni, muungano huanzia katika kuheshimiana.

Tuanahitaji kutawala eneo kubwa la ziwa Tanganyika lenye mafuta na gesi pia na usafiri wa maji. Kupitia Tanganyika, eneo lote la kivu kusini litayuhitaji Kwa Kila namna.

Biashara ya mabilioni ya Dola zitamilikiwa na WA Tanzania. Baada ya muungano, Sasa Bujumbura otakuwa kama Kariakoo. Biashara zote Toka nje zitafanyika pale.

Nchi za Congo, Angola na Jamihuri ya kati watakija Bujumbura Kwa mahitaji ya kibiashara. Congo itaondoa utegemezi Kwa mipaka ya Kisenyi na Bunagana na hivyo biashara zote zitapitia Bujumbura.

Miji ya Uvira, Bukavu, Goma, Ituri, Kisangani na Mpaka Kabinda na Bangui wote watakuja Bujumbura.

Biashara ya Madini Toka Congo itafanyika Bujumbura Kwa amani, Tanzania wa kawaida watajazana kwenye machimbo ya Congo na kujipatia Ajira .

Wakongo wengi wamejazana mijini na kuacha maeneo makubwa yenye ardhi nzuri yakiwa wazi. Hiyo ni fursa Kwa wakulima wa mazo ya Chai nankahawa kupata fursa.

Congo atafurahi kuwa karibu na rafiki wa kweli mwenye Nia njema. Kuna nchi zikisikia muungano huu lazima zipate kiwewe, kwakua fursa zote zitaelekea Tanzania. Lakini Jina la nchi libaki kuwa Tanzania, Burundi ijiunga kama mkoa.
Mwisho niseme.

Tuanahitaji Burundi ili tunufaike na Congo
 
Hakuna ulazima wa kuungana. Tunatakiwa kufanya yafuatayo kama tunataka kufaidika kibiashara kwenye nchi za maziwa makuu:

1. Kuimarisha usalama na kuhakikisha hakuna anayehatarisha interests zetu.

2. Kutengeneza mazingira mazuri ya mwingiliano wa kibiashara kati ya nchi zetu: kodi rafiki kwa biashara, njia za usafirishaji, uhamiaji usio na kona kona, uwazi ktk biashara, nk.

3. Kuwa tayari kusaidia na kuwezesha hizo nchi kujisimamia kiusalama na kibiashara. Kujenga meaningful friendship na hizo nchi. Kama ulivyosema kuwa Burundi ni loyal kwetu, in return tunapaswa kuwaonyesha kuwa we are trustworthy friends.

Tukifanya hayo tutakuwa hub ya kibiashara na maendeleo kwenye huu ukanda.

Angalizo: Ni lazima tuache ubabaishaji, rushwa, ufisadi, na porojo kwanza, ndipo hayo yanaweza kufanyika.
 
Baada ya taarifa za kuwepo harakati za muungano wa Tanzania na Burundi. Ni wakati Sasa jambo hili lipewe nafasi na lifanyike Kwa haraka. Jamii ya warundi ni tiifu Kwa Tanzania na miaka yote kuanzia raia mpaka serikali ya Burundi wamejiona salama chini ya Tanzania mpaka kufikia kuwa na kura ya pamoja katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa. Katika Kila jambo Burundi itasubiri kuona Tanzania imeamua nini na huo ndio itakua msimamo wao pia. Hii ni utii wa halo ya juu. Muungano huanzia moyoni, muungano huanzia katika kuheshimiana.
Tuanahitaji kutawala eneo kubwa la ziwa Tanganyika lenye mafuta na gesi pia na usafiri wa maji. Kupitia Tanganyika, eneo lote la kivu kusini litayuhitaji Kwa Kila namna. Biashara ya mabilioni ya Dola zitamilikiwa na WA Tanzania. Baada ya muungano, Sasa Bujumbura otakuwa kama Kariakoo. Biashara zote Toka nje zitafanyika pale. Nchi za Congo, Angola na Jamihuri ya kati watakija Bujumbura Kwa mahitaji ya kibiashara. Congo itaondoa utegemezi Kwa mipaka ya Kisenyi na Bunagana na hivyo biashara zote zitapitia Bujumbura. Miji ya Uvira, Bukavu, Goma, Ituri, Kisangani na Mpaka Kabinda na Bangui wote watakuja Bujumbura.
Biashara ya Madini Toka Congo itafanyika Bujumbura Kwa amani, Tanzania wa kawaida watajazana kwenye machimbo ya Congo na kujipatia Ajira .
Wakongo wengi wamejazana mijini na kuacha maeneo makubwa yenye ardhi nzuri yakiwa wazi. Hiyo ni fursa Kwa wakulima wa mazo ya Chai nankahawa kupata fursa. Congo atafurahi kuwa karibu na rafiki wa kweli mwenye Nia njema. Kuna nchi zikisikia muungano huu lazima zipate kiwewe, kwakua fursa zote zitaelekea Tanzania. Lakini Jina la nchi libaki kuwa Tanzania, Burundi ijiunga kama mkoa.
Mwisho niseme.
Tuanahitaji Burundi ili tunufaike na Congo
Baada ya kugeuzwa shamba la bibi la Zanzibar, sasa mnataka Tanganyika ipate mnyonyaji mwingine 🤔🙄

Kwani ushirikiano wenye tija hauwezekani mpaka kuwe na muungano wa nchi?!!!
 
Mkuu hii ndoto umeota,ushirikiano wa Afrika mashariki unatosha sababu watakuwa wategemezi kwetu tutawapa pesa zetu za mikipo ya world bank na IMF na kwingineko halafu mzigo wa deni utabaki kwetu lakini kikubwa kuna jirani zetu wanapenda sana kuja kuishi hapa nchini kwetu ikiwemo kuja kumiliki ardhi.
 
Mngejua wakazi wa kigoma wanachokipata toka kwa warundi msingekuwa na hamu na muungano huo hv why msipige kelele tuungane na Rwanda????
 
Hili jambo mbona lisambaa Sana? Nifafanulieni ndugu zangu, yaani Mimi natamani tuungane kwa kweli. Tkiungana Warundi hatagombana kwa sababu watakuta makabila zaidi ya 120 huku kwetu,sasa watashindwa wagombane na wangapi watatulia tulii.
 
Nilijua kuungana Kama walivyofanya Rwanda na Uganda huko mashariki ya Congo
Coltan ya Congo imeineemesha sana Rwanda na Uganda aisee.

1656837112839.png
 
Hiyo ilikuwa ni nia kwa kina Piere kwa miaka ile ya Mwalimu Julius na warundi walikuwa tayari kuwa sehemu ya Tanganyika ila baada ya Mwl. sidhani kama litawezekana, maana kila jambo na mtu wake.
 
Hiyo ilikuwa ni nia kwa kina Piere kwa miaka ile ya Mwalimu Julius na warundi walikuwa tayari kuwa sehemu ya Tanganyika ila baada ya Mwl. sidhani kama litawezekana, maana kila jambo na mtu wake.
Pierre liquid au buyoya?
 
[emoji74][emoji74][emoji74][emoji1][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2961]
 
Back
Top Bottom