Tuungane na Kala Pinna

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
2,026
Reaction score
3,107
Nimeangalia kipindi cha harakati cha kala pina kinachorushwa na television ya kilauzi (japo siipendi), nimekuta waungwana wanaangalia mahali nikajikuta na mm nimekodolea macho.

Alikuwa anamhoji mama mmoja aliyeathirika na madawa ila kwa sasa ameacha.... La msingi sio huyo mama Bali ni mtoto wake Keneth Lwakatare aliyemaliza form six akapata division two na kupangiwa kwenda mzumbe university.

Mama Hana msaada kwa kijana, kijana amekosa mkopo, na hawezi kuendelea tena na masomo kwa sababu Hana mkopo.

Mama analia akiomba mkopo toka kwa wadau na kijana anaongea kwa machungu akiamini kusoma kwake kusoma kwake kungekuja kuikomboa familia yake.

Hebu Tuungane, kumsaidia huyu kijana kutimizza ndoto zake. Kwa Hali na Mali..... Watu wa bodi ya mkopo mliopo humu Hebu fanyeni namna jamani... Na kwa watanzania wa kawaida ukiguswa fanya kitu.

Imenigusa, inaanza na wewe.
 
Kuna mtu anahusika na mikopo
sio sisi

Hebu mfuate yeye ofisini


Unadhani sisi tuna la kuamua wakati hata ****** anaangaliaga colouzi tovii kila siku
 
Kuna mtu anahusika na mikopo
sio sisi

Hebu mfuate yeye ofisini


Unadhani sisi tuna la kuamua wakati hata ****** anaangaliaga colouzi tovii kila siku
Acha jazba mkuu, kuwa na moyo wa kusaidia.
 
Mi nina moyo wa kusaidia hadi huwa najishangaa

niliwahi kusaidia hadi Kagera

Sema kwa sasa moyo huo niliachana nao kwa muda

Acha tujifunze kufanya maamuzi sahihi kwanza!
Umenikumbusha machungu sana, ila tudumishe utanzania ndugu yangu.
 
Ivi hatuna serikali?mbona wadogo zetu karibu wote wameshindwa kwenda shule.
 
Umenikumbusha machungu sana, ila tudumishe utanzania ndugu yangu.

Tatizo sio sisi
Tatizo ni system

Na ukienda kinyume na system si muda utabadilishiwa jina

System inatutaka tushtuke kabla ya kuchangia

So natimiza matakwa ya system!!!

Utanzania ni bora, na ndio jukumu letu

Lakini huwa vinafika kwa walengwa?

Tena umesema colouzi midiya?

Hata sitoi!!

Sorry
 
Moja ya watu wanaofanya kazi kubwa ktk kuirekebisha jamii ni KALAPINA lkn watu hawamuoni, kipindi chake kizuri lkn hakina wadhamini ila bado hajakata tamaa, huyo dogo nilimuona yy na mama yake ambaye alikuwa mwathirika wa madawa ila sasa anatumia methadone, inatia huruma sana pamoja na mazingira magumu aliyokulia huyu dogo bado form six kapiga II - 11 PCB (kwa wanaoijua shughuli ya PCB advance nadhani lazima watatoa salute kwa huyu dogo) na amechaguliwa SUA (Bsc in industrial engineering and management) ila mkopo hana (sijui bodi wanaangalia vigezo gani). Huyu anahitaji msaada sana, mimi mwenyewe nimeguswa ila uwezo sina, anatia huruma kama ingewezekana bodi wasikilize rufaa ya huyu kijana. Big up brother pina usichoke, kupitia ww watu wanajifunza mengi
 
Watu mnajifanyaga kuiponda clouds ila ndo wa kwanza kuifatilia[emoji41] [emoji57]
 
lwakatare?? aende mlima wa moto kuna hela kibao
wahaya wana hela sana sidhani kama atakosa msaada tena aanze na ruge amtembeze kwa wahaya wenzake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…