Tuupime weledi wa NDUGAI kwa vigezo viwili vifuatavyo:

Tuupime weledi wa NDUGAI kwa vigezo viwili vifuatavyo:

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
3,626
Reaction score
3,869
Ndugai ameonekana kuhoji mkopo wa serikali wa Tril.1.3,ni sawa lakini tukumbuke mambo mawili yafuatayo:
1.Mbona hakumuunga mkono CAG prof.Assad kipindi ambacho palikuwa na matumizi mabaya kupindukia ya fedha za umma?
NB: Trilioni 1.5 aliyohoji Zitto nayo je?

2.Kama lengo ni uwazi wa mkopo,
Mbona wapinzani waliteswa enzi za Magufuli (kuliko kipindi chochote)
ambao,wengi wao walihoji matumizi ya fedha za umma?
Na kwa nini katika kipindi hiki tu cha
mh.SSH ndicho anaonekana kuhoji na kukosoa?

Tuupime weledi wa NDUGAI kwa vigezo viwili hivi.
 
Hakuna muda maalum wa mtu kutakiwa kuhoji, muhimu ni kujibu hoja yake tu bora hajavunja sheria yoyote ya nchi. Unaonesha ulivyoathirika kiakili na mfumo wa hovyo unaotawala mihimili yetu.

Kwako kama makosa yamewahi kufanyika, basi yaachwe yaendelee kufanyika tu kwasababu ndio kawaida yenu, akitokea mtu wa kuhoji tofauti miongoni mwenu unamuona wa ajabu, amka usingizini, usiiangamize Tanzania yetu kwa upeo wako mdogo.
 
Back
Top Bottom