Terrible Teen
JF-Expert Member
- May 1, 2017
- 1,009
- 2,934
Naomba niandike kwa kifupi sana . Katika Nchi yeyote ya kidemokrasia vyombo vya kiuchunguzi wa jinai na utoaji haki hutakiwa kuwa huru na hivyo vionekane kutenda haki. Kwa siku za karibuni hapa kwetu kumekuwa na udhaifu na dosari kadhaa hivyo kupunguza kuaminika kwa vyombo hivyo.
Natoa mifano michache hapa.
1. Bila ya kuathiri hukumu ya mbowe na wenzio, ila DPP alitakiwa kuwashtaki Msimamizi wa uchaguzi Kinondoni na askari waliokamatwa awali lakini wakaachiwa. Double standard ikajielekeza kwa upande mmoja.
2. Mashtaka ya uchochezi yamekuwa ya upande mmoja tu. Mwenyekiti UVCCM Taifa ameongea hayo hayo hakukamatwa wala kuhojiwa, mwingine wa UVCCM Iringa katishia kuua hata jalada halikufunguliwa.
Kwa mifano hii , na mengine mengi ikiwa ni pamoja na hata aina ya hukumu ya mbowe ya leo ni dhahiri tunalipasua Taifa. Madaraka ni ya muda tu. Kutafakari Vizazi vyetu vya baadae kuepuka uwezekano wa genocide. Kule Rwanda wale wahutu walio wengi walikumbuka madhira ya zamani sana ambayo babu zao walifanyiwa na Watusi wachache, yaliyotokea tunajua.
Tujifunze kuvumiliana na kufanya siasa safi. Demokrasia itamalaki , tusiwe na roho ya kisasi . Mungu atuongoze hima. Nafikiria familia ya mtu kama Mbowe, siasa imemfirisi watoto wake wanawaaangaliaje watoto wa viongozi wa juu wa CCM leo ambao wanaamini mateso yao yametokana na viongozi husika.
Dunia tunapita , sote tu mavumbi, na mavumbini tutarudi tena kwa kuwekwa bila idhini yetu wala Ulinzi wa bunduki.