Tuutafakari na Kuufanyia Kazi mfumo huu wa Elimu kwa mustakabari wa Taifa Letu

Tuutafakari na Kuufanyia Kazi mfumo huu wa Elimu kwa mustakabari wa Taifa Letu

Zinedine

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
1,187
Reaction score
694
Kumekuwa na sintofahamu na mambo kadhaa yanayoleta mijadala isiyoisha juu ya elimu yetu, mfumo wa elimu yetu na uwezo wake katika kulikomboa Taifa hili kutoka katika umaskini uliokithiri. Kwanza, nibainishe kwamba mimi si mtaalam katika fani ya elimu ila bila shaka naathiriwa na mfumo wa elimu kwa namna moja ama nyingine. Miongoni mwa mijadala inayotamalaki kwa siku au miaka ya hivi karibuni ni pamoja na ule wa kuyaweka masomo ya Physics na Chemistry pamoja uliobuniwa na Joseph Mungai (niko tayari kukosolewa kama niko wrong) aliyekuwa Waziri wa Elimu, lugha ya kufundishia kwa ngazi zote au baadhi katika mfumo wetu wa elimu pamoja na muundo wa kutahini au kutoa madaraja kwa wahitimu. Kama nilivyosema hapo juu, mimi si mtaalam hasa katika sekta hii, ila najua wapo manguli watakaokuja kutuweka sawa zaidi.

Kwa upande wangu, mimi nina hofu zaidi ya mambo mawili:- mfumo wa na usimamiaji wa elimu yetu. Katika Mfumo, ni wazi kwamba unawaacha wahitimu walio wengi katika ngazi mbalimbali pasipo na skills za aidha kuweza kujiajiri au kuweza kuajiriwa. Ni asilimia chache sana ya wahitimu wa Darasa la Saba wanaofanikiwa kwenda Sekondari, halikdhalika wengi pia wanaachwa kutoka Kidato cha 4 kuingia Cha tano na hivyo hivyo kutoka Kidato cha VI kuingia Chuo Kikuu. Chini ya Mfumo tulionao, mhitimu wa Darasa la saba, kiadato cha IV au VI aliyeshindwa kuendelea katika hatua ya juu yake, anakuwa amepoteza haki zote za Kielimu kwa maana hawezi kujua uelekeo wake. Hii ni kutokana na ukweli, elimu ya ufundi (Vocational) ni kama haijawa formalized nchini kwetu na badala yake kwa wanaoenda huko (eg VETA), sio tu ni suala la utashi wa mtu au kama "kutupa jongoo na mti wake" lakini ni ukweli kwamba kundi hili halina Jukwaa rasmi la kuajiriwa, kwani Binafsi sijawahi kuona Tangazo la kazi linalotoa sifa ya "aidha aliyemaliza kidato cha nne au elimu ya ufundi". Kutokana na ukweli huu, elimu ya ufundi imekosa utashi wa kuvutia vijana wengi hali iliyopelekea hata baadhi ya vyuo vya VETA kuanzisha madarasa ya fani ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na ufundi(amali); mafno Procurement, Business Administration au Accounting(zisizo na specialization ya ufundi wa amali).

Aidha, kwa upande mwingine, tunafahamu kwamba, tumesahau quality na kuzingatia sana quantity. Hali za Shule zetu ni mbaya sana, elimu inazidi kuwa "wakala" wa kuwagawa watanzania katika makundi tofauti-tofauti kutokana na kipato chao na uwezo wa kuwapatia elimu watoto wao. Imefikia hatua, matokeo ya kitaaluma ya mhitimu yanajulikana tangia akiwa Chekechea kutokana na shule anayepelekwa. Kwa mtoto atakayepelekwa katika English Medium au kwa Lugha rahisi shule binafsi(ingawa nazo zina matabaka), anakuwa na probability kubwa ya kufika hatua za juu za elimu hata kama uwezo wake halisi wa kichwani unazidiwa kwa mbali sana na yule wa "Manzese Uwanja wa Fisi). Hii ni hatari!

Kutokana na ukweli huu, napenda kuwasilisha mfumo huu wa Elimu unaotumika nchini Finland, ambao huenda hautakuwa mzuri kwetu kwa asilimia 100, lakini una hazina ya uzani-sawa kati ya elimu ya "kitaaluma" na ile ya kiufundi (vocational), na hivyo tunaweza ku-customize ili kuendana na mahitaji yetu. Aisha, suala la Lugha na mengineyo nayaacha kwa wanajamvi ili kila mmoja atoe mchango wake. Mfumo wenyewe ni huu hapa chini:

Magwiji wa uchambuzi na taaluma karibuni kwa kudadavua hili hususana Dkt. Kitila Mkumbo, Nguruvi3, MCHAmbuzi, Mwalimu @gfsowin, CHAMVIGA, Ritz, faizaFoxy, zumbemkuu, Zakumi, john Myika unahusika kwani ni mdau muhimu wa elimu na wengine wote.
 

Attachments

  • FINLAND education system.jpg
    FINLAND education system.jpg
    24.4 KB · Views: 237
Mkuu Zinedine;

Kuna mijadala mingi ya kuhusu mfumo wa elimu wa Tanzania. Na mijadala hii haikuanza leo. Lakini haitakuwa vibaya kuirudia.

Kwa upande wangu binafsi naona tunaolalamikia serikali kuhusu ubora wa elimu, haituitendei haki serikali. Hii ni kwa sababu mfumo mzima wa sasa ulianzishwa hii kuongeza idadi ya wanafunzi katika shule za msingi. Na hiki ndicho kitu kinachofanyika. Sasa tunailamu vipi serikali?

Kama tunataka mabadiliko ya elimu, mission statement ni lazima ibadilike na vidonge vichungu ni lazima vimezwe. Kwanza inabidi workforce linalofanya kazi ya kutoa elimu lifanyiwe mabadiliko makubwa. Kuna watu itabidi waambiwe kuwa hawafai kuwa waalimu. Vilevile serikali ikubali kuongeza maslahi ya wale wenye sifa za kuwa educators.
 
wakuu umeme wa mgao unaathiri kuonekana kwetu JF, nikipata wasaa ntakuja kutoa yangu mawazo kuhusu elimu yetu..

Poleni sana mlio Dar, tunasikitishwa sana na kinachoendelea kiasi kwamba tunashangaa hizi mbio za kufunga safari za Ulaya, Ameriaca na Asia kutafuta "investors" zinawezekanaje na power-outage hiyo inayoendelea.
 
Back
Top Bottom