Tanzania ni nchi moja katika zinazoangukia kwenye ule ukanda ambao wananchi wake hawana furaha katika nchi zao wenyewe.
Pamoja na sisi ni Uganda, Rwanda, Burundi na Zimbabwe.
Hawa wengine si wenzetu tena: Kenya, Zambia, Malawi au Afrika Kusini.
Itoke wapi furaha kwetu wakati pasipo na uhalali wowote watu wamepotezwa, wameuwawa, wameteswa, wamejeruhiwa, wamebambikiwa kesi, wamebambikiwa hukumu, wako magerezani, wamefilisiwa nk wakati kidole kwa watesi kikielekezwa kwa utawala ulio madarakani?
Ikumbukwe wahanga hao wana ndugu, jamaa na marafiki ambao nao wana ndugu, jamaa na marafiki zao pia.
Siyo siri kuwa miito ya kuitishwa kwa maridhiano haijapokelewa vyema na walio wachawi wetu. Hii ikiwamo hata ile miito ya kutokea kwa Mheshimiwa Rais Samia:
Ama kwa hakika mchawi wetu siyo Samia, JK wala CCM. Kwa maslahi gani CCM, Samia au JK wawe sehemu ya uhuni wa kijinga namna hii? Ili iweje?
Kama CCM siyo adui -- mchawi wetu ni nani?
Sote tunapokuwa tunaugulia maumivu ya faulo hizi za wazi, kwa mustakabala wa nchi yetu ni muhimu kuunganisha nguvu kupambana na adui yetu huyu wa pamoja.
Adui amedhamiria kuendelea kuwepo milele. Yuko tayari kuuwa, kutesa, kufunga na hata kupoteza.
Zaidi sana yuko tayari kupotosha adui ni nani kwa lengo la kutengeneza utengano wowote baina yetu.
Uzuri ni kuwa alipo sasa ni kama paka mwenye kengele.
Kwa hakika nyambizi na asimpate mtu.