RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara wa 19:
Pole na hongera kwa kazi dereva wa Bodaboda. Kuzunguka salama na chombo cha moto kila siku ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Naomba leo nikuume sikio mambo ambayo yanapendwa na wateja (abiria) ambapo wewe bodaboda unapaswa kuyafahamu na kuyazingatia. Ili wewe bodaboda uweze kunufaika zaidi kwenye kazi yako, fuatilia mambo ambayo wateja (abiria) wengi wanapenda.
👁️ USAFI
Kuwa msafi wa mwili kama vile nywele, kuoga na kuswaka kinywa kila mara. Lakini pia usafi wa mavazi na chombo chako cha usafiri (pikipiki).
👁️ UAMINIFU
Uwe mwaminifu kwenye kazi yako, kwa ufupi uridhike na kipato chako. Kwa mfano kufikisha salama mzigo, pesa au mtoto wa mteja wako. Mfanye mteja wako akuamini.
👁️ UKWELI
Kuwa mkweli. Upigiwapo simu na mteja wako fika haraka, au mpe location yako ya ukweli ili aamue mwenyewe kukusubiri au kutafuta bodaboda mwingine. Usimdanganye mteja wako ili tu akusubiri wewe.
👁️ KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
Ni abiria wachache sana wanapenda kukimbizwa kasi, abiria wengi hawapendi mwendokasi. Pia abiria wengi hawapendi kukamatwa ovyo njiani kwa makosa ya kutokuwa na leseni na kutovaa helmet, kwasababu abiria anahisi yeye pia atahaibika kwa kuambiwa na askari kuwa unapandaje bodaboda asiyekuwa na Leseni. Hivyo wewe bodaboda unapaswa kuzingatia sheria za usalama barabarani na ukamilike kwenye hayo mahitaji.
👁️ KABA (USIRI)
Usiri kwenye kazi ya Bodaboda ni jambo muhimu sana. Usiwe Lopolopo kwenye siri za kawaida za wateja wako. Hata hivyo zingatia sio siri zote ni za kuficha, bali zipo siri ambazo hutakiwi kuficha kwasababu ya maslahi mapana ya jamii na usalama wa watu wengine.
Mambo mengine utaambiwa na wadau wa JF kwenye comments. Fuatilia comments.
Right Marker
Dar es salaam.