tabu kuishi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 353
- 43
Unajua ndg yangu shida inabaki na ukweli kwamba mawaziri wote ni CCM na isotoshe wana vita vya wenyewe kwa wenyewe ili kuendelea kupotezeana dira katikta masuala ya kisiasa hulazimika kufanya mambo ndivyo sivyo hata jama anajua kua kuna kasoro katika hicho anachokubaliana nacho.Mfano mzur ni Mh. Sitta huyu ni waziri lakini si waziri mwaminifu hata kidogo katika baraza la mawaziri lililopo,amekwenda kwenye mandamano kule Mbeya akiwa anaongea na wanafunzi wa chuo kikuu akawambia serikali iwaombe radhi kwa tatizo la mgao wa umeme na kuongea hadharani kua tatizo ni mafisadi wachache wanaolingiza taifa katika tatizo la umeme kwa kusaini mikataba mibovu yenye maslahi binafsi.Sitta hakuona kwamba tatizo ni la mda mrefu tangu yeye yupo madarakani kama spika wa bunge je!Alishauri nini serikalini juu ya hilo,lakini tena je!Akiwa yeye ni mmoja wa mawaziri amewezaje kuipitisha bajeti hiyo katika vikao vyao vya mawaziri vya kupitia bajeti mbalimbali?Leo hii anatoa kauli na mambo ya siri ndani ya baraza la mawazari!CCM ijiandae kung'olewa madarakani.Tulichokisikia na kukiona ni muendelezo wa ujinga na umbumbu la baraza letu la mawaziri yaliyote yaliokosolewa na kurudishwakwa bajeti ya wizarani ya nishati na madini yalipita mbele ya baraza la mawaziri. Ina maana hawajaona upungufu na kasoro za bajeti ya hiyo wizara hadi kufika bungeni na kurudishwa tena.