Izack Mwanahapa
JF-Expert Member
- Apr 21, 2011
- 497
- 236
Ndugu wazalendo wananchi wa Tanzania, tumelalamika sana kuhusu mapungufu na uchakachuaji ambao umejitokeza kwenye uundaji wa mabaraza ya katiba kiasi cha kuonesha kukosa imani na mabaraza hayo. Tutumie fursa hii maridhaya ya kuendesha mabaraza huru ya katiba kutumia Asasi, Taasisi na Makundi ya watu wenye malengo yanayofanana kutoa maoni yetu kwa ufasaha.
Naamini nguvu ya makundi haya ni kubwa kuliko nguvu ya mabaraza halisi ya katiba kwani asasi na taasisi zinaweza kupata watoa maoni wengi zaidi kuliko wale waliomo kwenye mabaraza ya katiba kwani asasi zipo kila kona ya nchi hii. Ni muda wa kuungana na kulipigania taifa letu, nchi inahitaji misingi bila kujali ni nani anategemewa kuchukua nchi 2015.
Naamini waliokuwa wakisukumwa na uzalendo kulalamikia Mabaraza ya katiba wataitumia fursa hii, samahani sana kwa wale ndugu waliokuwa wakisukumwa na posho kwasababu ni wazi kwamba mabaraza haya ya asasi na taasisi yapo kiharakati zaidi posho kidogo au hamna kabisa. Weka Taifa kwanza mengine baadae.
Nimeatach muongozo wa kuendesha mabaraza hayo ya makundi mbalimbali, humo mpaka vikundi vya wakulima vipo na vinaruhusiwa kutoa maoni yao kwa uhuru.