Elections 2010 Tuwafanyeje wasanii wetu waongezeke ktk game la ukombozi?

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2010
Posts
1,399
Reaction score
255
Kazi ya msanii ni kuburudisha na kufundisha. Hivi tukiwaangalia wasanii wetu wanayatimiza vipi mambo haya mawili na mhimu? Ukiachilia Mpoto, Wagosi wa kaya, Mr. 2, Roma (huyu anatisha kwa maana kuwa amekuja kwa kasi katika kuamasisha vijana) na wenginewamekuwa, waliowengi wamekuwa wakiimba mapenzi na mambo yasiyohusu maisha ya watanzania walio wengi hasa masikini na wakulima.

Ikumbukwe hapa naongelea wasanii wa mziki wa kizazi kipya. wapo wale waliodiliki KUJIKOMBA kwa magamba hawa ni pamoja na akina A-Y, Marrow, Wanaume makundi yote (kina Nature, Mh. Temba, Chege) na hawa comedy original ( hawa si wanamziki) Mimi hawa nawaita MISUKULE/ WASALITI au WANAOJIKOMBA.

Hoja yangu ni kwa nini hawa jamaa wanaendelea kuwa hivyo hivyo bila kubadilika? Hivi hawajui nchi ina matatizo au wanajikomba wapewe viti maalum bunge lijalo?

Ebu tujadili maana tukiwapata hawa tutapata wapunge huru ambao watusaidia kufichua movu na kuiamsha jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…