Watatapanya mali za familia hovyo.
Sadaka inatoka kwenye jasho la mtu.
Watafute hela kwa jasho lao ndiyo wazitoe
Fundisha nadharia tu.
DNA = Imebeba taarifa za chanzo, chimbuko na njia za kiumbe husika.
DAMU = Imebeba chembe chembe za uhai zitokanazo na muingiliano wa mbegu yenye uhai kutoka kwa kiumbe Me kuingia katika ‘yai’ lenye uhai ndani ya via vya uzazi (uumbaji??) vya kiumbe Ke.
Watoto wetu ni sehemu yetu iliyotokana na kielelezo cha Hisia zetu juu ya Uhai wetu (chembe hai ndani yetu??)
Watoto wetu ni muendelezo wetu. Ni muendelezo wa chanzo chetu. Ni muendelezo wa kule tulikotoka. Ni waendeleza njia ya kule tunakotarajia kwenda.
Watoto wetu ni nafasi yetu (chembe hai yetu??) kuendelea pale tutakapo ishia sisi ili kukamilisha dhamira ya uumbwaji wetu.
Watoto wetu ni wawakilishi wetu wafuatao hapa duniani baada ya kuondoka kwetu Kama ambavyo sisi tunawakilisha wazazi wetu (watangulizi wetu) waliopita.
Watoto wetu ni nafasi yetu ya pili katika maisha yetu katika kujifunza na kuyarekebisha makosa yetu yaliyopita na ya watangulizi wetu.
Watoto wetu ni sisi wenyewe katika nyakati zijazo. Wazazi wetu ni sisi hapa katika kizazi hiki.
Watangulizi wetu ni wazazi (waumbaji??) wetu katika nyakati zilizotangulia.
Watoto wetu ni kila sababu ya mapambano yetu ya kusonga mbele na kuamka tena kila kukicha.
Ni haki yao kulindwa, kuongozwa na kuandaliwa kuendelea mbele bila kushindwa wala kuchoka wala kukata tamaa kwa kuhakikisha wanazo nyenzo sahihi za kufanya hivyo (Elimu + Mali??).
Watoto wetu ni jukumu letu Kama ambavyo sisi ni jukumu la wazazi wetu na wao la wazazi wao (waumbaji??)
Ahsante.