Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Ilikuwa mwaka 2006 majira ya Jumamosi nipo zangu nyuma ya bweni nikishua shuka zangu mbili na sare za shule, pembeni nipo na redio yangu niliyopewa na Babu. Hapo ni kidato cha pili, kidogo swahiba wangu mkubwa sana alikuja mbio na kunipa taarifa kuwa Mwalimu Mkuu ananiita kwake, sio mbali ilikuwa ni pembeni ya shule tu, kiukweli tuliishi vizuri na Mkuu hivyo nilimwambia Rafiki yangu kuwa ngoja nimalizie kufua nguo kabsa ili nikienda niende nikiwa sina kazi yoyote tena.
Nilimaliza kwenye majira ya saa 6 mchana na baada ya kumaliza nilivaa nguo na kanda mbili na kuelekea kwa Mkuu, nilipofika niliona ananichangamkia ila hakuwa kwenye uchangamfu wake wa kawaida (Kuna Wakati alikuwa ni zaidi ya Mlezi ni kama alikuwa Mshua wa pili), alinikaribia kisha tukakaa na kuanza kuongea. Aliniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni, kuhusu Maisha ya shule na vingine vingi.
Nilimaliza kwenye majira ya saa 6 mchana na baada ya kumaliza nilivaa nguo na kanda mbili na kuelekea kwa Mkuu, nilipofika niliona ananichangamkia ila hakuwa kwenye uchangamfu wake wa kawaida (Kuna Wakati alikuwa ni zaidi ya Mlezi ni kama alikuwa Mshua wa pili), alinikaribia kisha tukakaa na kuanza kuongea. Aliniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni, kuhusu Maisha ya shule na vingine vingi.
Katika stori mbili tatu, alinipa taarifa kuwa Mzee wangu yupo hospitali na anaumwa sana, hivyo ninatakiwa kwenda kumtazama Bugando, kwa namna alivyoongea ni kama Jambo la kawaida ila macho yake yalikuwa yakiongea kitu tofauti kabsa. Nilimuuliza, Baba anaumwa nini? Mkuu alitabasamu tu na kuniambia “Baba yako atakuwa salama wala usijali.
Miaka ya 80 mwanzoni mwanzoni, mzee pamoja na Rafiki zake walikuwa wanapiga sana maji kiasi kwamba walikuwa wakilala vilabuni, mara kadhaa aligombana sana bibi, na kuna picha moja amepiga na Bibi akiwa amelewa chakari. Kwa mujibu wa Bibi, Mzee wangu akiwa na Miaka 28 hali yake ilikuwa mbaya sana na alipopelekwa hospitali ilionekana kuwa Ini lake limeharibika vibaya sana, na kutokana na gharama za matibabu kuwa kubwa ilimbidi mzee arudi nyumbani (Wakati huo walikuwa wakiishi Igumbilo, Iringa), ingawa geto la Mzee lilikuwa huko Madibira, Mbeya kabsa.
Mzee alikaa maskani kwao kwa muda wa mwezi mmoja na hali ikawa ni mbaya kila siku kiasi kwamba wakaanza kutafuta wataalamu wa jadi (madaktari) kutazama namna ya kuokoa uhai wa mzee, walikwenda sehemu mbalimbali, Ilole milimani huko lakini wengi walidai kuwa hiyo hali haina tiba. Siku moja, Dada zake na Bibi ambao ni dada wakubwa walimtembelea kumtazama mzee, na mmoja wa Dada yake na Bibi alikuwa anaitwa Nyamsenga alikwenda kumtafuta Daktari wa Jadi huko Ubaruku kama unaelekea Makambako, na yule mtaalamu alipomutazama Mzee akasema kuwa tiba inawezekana ila inatakiwa aende naye huko Ubaruku ili yeye pamoja na wenzake wamfanyie ustaarabu wa kumtibu Ini, Mbalali wilaya iliopo Mkoa wa Mbeya.
Kwa mujibu wa Bibi walipofika walitengwa wanawake sehemu yao na wanaume sehemu yao, kulikuwa na sehemu ambazo mwanamke hakuruhusiwa kabsa kufika, vivyo hivyo kulikuwa na sehemu ambazo mwanaume hapaswi kabsa kutia mguu wake. Mzee aliweka kwenye nyumba ya nyasi na walichanganya dawa za asili na kufunga mlango wa nyumba hiyo ya nyasi na kuanza kuimba nyimbo za kihehe huku wakirusha maji kwenye kijumba hicho, kiasi kidogo cha dawa kilibaki kwa kazi nyingine ya kitabibu.
Ilipofika usiku wa manane, walikwenda kilingeni na kuchinja Mbuzi mweupe, alikuwa mweupe asiye na doa, mbuzi dume (Beberu), Moyo, Ini, Korodani na Mzuzu viliwekwa ndani ya mtungi, na ile dawa kiasi iliyobaki, kila mtaalamu aliweka mate na damu na kuchanganya kisha walipandisha juu ya kijuba cha nyasi. Walimpa maelekezo Mzee asije kuamka hata kitokee nini, yeye alale mpaka asubuhi wakija kumtazama. Nyama pamoja na vingine vilivyobaki katika mbuzi vilifukiwa hakuruhusiwa mtu kula chochote.
Usiku ulikuwa mrefu sana kwa Mzee kwani alidai kuwa hakuwa peke yake, alikuwa na uhakika kuwa walikuwepo watu au viumbe wengine zaidi ya watano, kuna Wakati pumzi ilikata na mbavu zake zikawa ni zinavutwa kutoka nje. Mzee alitamani kupiga kelele za msaada ila ni kama sauti ilikuwa haitoki. Mpaka inafika asubuhi, mzee alikuwa amelowa jasho mwili mzima. Na wanawake walipewa maelekezo kuwa watamtazama Mzee au mtoto wao majira ya mchana. Asubuhi nzima wazee walikuwa wakiimba nyimbo, na baadaye walikwenda kwenye mbuyu mkubwa abapo ilikuwa ni sehemu ya ibada kwao. Walishukuru miungu na kukaa kwa ukimya kwa zaidi ya lisaa na baadaye kurejea nyumbani.
Mzee alipona Ini lake ila alipewa masharti na wataalamu, mosi asije kula nyama ya Mbuzi (Asile kiumbe ambaye ndio amempa tiba), pili asije kunywa pombe Maisha yake yote, tatu, kila mwezi apeleke sadaka ya kuchinja (mbuzi mweupe) na mwisho akianza safari ya kuondoka Ubaruku asingeuke nyuma.
Mzee wangu alifariki mwaka 2007 kwa baada ya Ini lake kushindwa kufanya kazi, Marehemu Bibi alifariki mwaka 2020 aliniambia kuwa Mzee wangu alikuwa akipikiwa nyama ya Mbuzi na moja ya Mke wake ambaye hakuwahi kuifahamu historia kamili ya mzee, kifupi Mzee alikuwa na wake tisa na watoto tupo 28. Pumzika Mzee wangu! Tumekumis sana Mwamba!
ILA USICHEZE NA TAMADUNI ZA WAAFRIKA! SHIKAMOO WAAFRIKA!