Tuwahurumie Graduates, Hakuna Mwanasiasa wa kuwatetea Vijana waliomaliza Chuo

Acha blah! blah! vijana wanasoma vizuri na wanafaulu, nyie kwa siasa zenu uchwara mmeshindwa kujenga mazingira ya kuwatumia hawa vijana wanaohitimu kuleta tija kwenye taifa, hamna ajenda za kueleweka za maendeleo..............ni mwendo wa kudemka tu asubuhi hadi jioni.........
 
Story of change
 
Badilisha kigezo cha elimu ya mtu kugombea ubunge. Kujua kusoma na kuandika tu haitoshi, lazima mbunge awe na digrii
Hao waliosoma na PHds huko bungeni ndio wapuuzi na wezi kuliko fisi, na kuna watu wazuri na wachapa kazi na hawana degree
 
Hii idea ya kuwanunulia maofisa wa serikali VXR,GXR, V8 kwa nchi maskini kama Tanzania nimeshindwa kuielewa kabisa, dadeki ningekuwa mimi wote wakurugenzi,wakuu wa wilaya etc ingekuwa ni bodaboda tuu na anayetaka V8 akakope bank la kwake
 
Kuwa na maaskari wote graduates itakuwa mzigo mkubwa sana kwa serikali kifedha, watadai kulipwa kwa ngazi ya graduate.
Kulinda na kukamata watu kunahitaji akili kidogo tu..
 
Kuwa na maaskari wote graduates itakuwa mzigo mkubwa sana kwa serikali kifedha, watadai kulipwa kwa ngazi ya graduate.
Kulinda na kukamata watu kunahitaji akili kidogo tu..
By simba
 
Duh! we jamaa noma!
 
Hii idea ya kuwanunulia maofisa wa serikali VXR,GXR, V8 kwa nchi maskini kama Tanzania nimeshindwa kuielewa kabisa, dadeki ningekuwa mimi wote wakurugenzi,wakuu wa wilaya etc ingekuwa ni bodaboda tuu na anayetaka V8 akakope bank la kwake
Boda boda? you can't be serious Bora ungesema IST au vits
 
Shida ya watanzania ni kutokuwa wabunifu hata wakitoka vyuoni malengo ni kuajiriwa tu, unatakiwa ufikiri zaidi na kubuni kazi zipo nyingi tu tatizo tunataka kazi za ofisini tu
Siyo kazi za ofisini tu bali kazi iwe mjini tena mjini kweli, Mimi naona Tanzania kazi bado ni nyingi sana tatizo lipo kwa wananchi wenyewe kutokujua nini wanataka ila wachache tu ndo wanajielewa imagine uwekezaji mkubwa upo mjini sehemu zilizoendelea lakini ikitokea Serikali inataka kuwekeza vijijini watu hawataki na wanabeza kweli tena sana Sasa hizo ajira zilizotosha watu wa zamani tena mjini zisipoongezwa vijijini zitatoka wapi? Vijijini Sasa ndo kupelekwe maendeleo kwa wingi kiasi cha kuwa na umeme, maji, shule, vyuo vya Veta na Vikuu, barabara, hospital kubwa yaani hizo huduma tu zitaajili watu wengi Sasa hizo huduma serikali iombe na mashirika ya Dini na wale taasisi za misaada wajenge vijijini huduma hizo hayo yote yanatakiwa wananchi waweke msisitizo kwa serikali Ili wale wanahitaji kazi wapate kazi wafanye maana Kuna wengine hata iweje hawataki kazi wanapenda tu kulaumu na kupiga kelele bila kujishughulisha kwa kisingizio cha kukosa ajira, kingine wananchi waombe serikali mikopo ya riba ndogo Ili wale wanaohitaji mitaji wakope wafungue ofisi zao imagine Raisi alisema BOT wapunguze mikopo lakini watu wamekaa kimya hata hawaulizi hiyo ajenda itafanyiwa kazi lini? tena wengine wanapinga watu wasikope kwa riba ndogo Ili watu waendelee kukosa mitaji na meetings watu wapate ajenda za kupiga kelele huku umri wa kufanya kazi wakiwa na nguvu unawatupa mkono, hivyo watu tuamuke kuomba vijiji vigeuzwe mjini na viwanda na huduma zote kubwa na ndogo ziwe vijijini na watu wote watapata kazi iwe za kusajiliwa au za kujiajili.
 
Wajitetee wenyewe pamoja na mama zao. Kwa nini usubiri mwanasiasa akutetee kama unaona kuna jambo halipo sawa,huo ni ujinga. Ndio maana hata harakati za katiba hazisogei pakubwa kwa sababu tunasubiri wanasiasa waipiganie
 
Viongozi wana raha sana, na hapo Pole Pole hajazungumzia posho na mishahara.

Sijui kwa nini wasiongeze nafasi za Viongozi ili Watu wengi tupate hizi fursa, ni wengi tunapenda jamani.
 
Mwanachuo kwa sasa atajibana matumizi sana na nawapongeza kwa hilo, Lakini lengo la kujibana matumizi ni apate simu ya toleo jipya na la kisasa kwa ajili ya kuangalia picha na kuonyesha watu, Hawajui kazi zingine za simu
Hapa upo sahihi, na hili ni janga kubwa mnoπŸ€”
 
My services include, but are not limited to:

  • Web designing
  • Logo designing
  • Online business or company registration (BRELA,TIN)
  • Airline and Bus ticketing (Domestic & International)
  • Passport and Visa Registration
  • Studying abroad programs (China, Germany, Malaysia, India and etc.)
  • Online imports and export services (India, China, Malaysia and etc.)
  • And any other I.T support/consultant services.

 
Umefanya self praise.

Ulichoandika ni completely out of Content, out of proportional...πŸ€£πŸ€£πŸ˜πŸ˜πŸ™„πŸ™„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…