MKAKA WA CHUO 2
Member
- Aug 15, 2022
- 5
- 0
Maisha ya mwanadamu ni mfumo au mzunguko unaohusisha hatua mbalimbali hadi kukamilika kwake. Hatua za Maisha ya binadamu zinajumuisha utoto, ujana, utu uzima na uzee. Katika Maisha ya kawaida kila mwanadamu anapokuwa mtoto anahitaji uangalizi mkubwa na wa karibu Zaidi kutoka kwa wazazi au walezi wake. Uangalizi huu unajumuisha kuhakikisha mtoto anapata mazingira salama ya kuishi, chakula na mavazi ya kuvaa.
Katika hatua zote ambazo mwanadamu anapitia huhitaji msaada kulingana na mazingira ambayo yanamzunguka katika wakati husika, kwa hali ya kawaida na uhalisia baada ya kutegemea msada kuto kwa mungu ambaye tunaamini ndiye aliyetuumba sisi wanadamu, wazazi wetu pia ni nguzo muhimu ambayo sisi kama wanadamu tunaitegemea pindi tunapokuwa Watoto, tunapokuwa vijna na wakati mwingine hata tunapokuwa watu wazima pia huwa tunawategemea wazazi wetu katika harakati tofauti za kimaisha.
Kwa kila mwanadamu aliyezaliwa mpaka akafikia umri wa utu uzima na uzee, basi lazima atakuwa amepitia katika hatua mbalimbali za Maisha kama tulivyoziainisha hapo juu, katika Maisha haya ili mwanadamu atoke katika hatua ya utotoni hadi hatua nyingine, yaani ujana na kadhalika, ni lazima apewe malezi na uangalizi wa karibu kuanzia siku anazaliwa mpaka atakapofikia umri wa kuweza kupambanua mambo na kujitegemea, takribani mara zote wengi katika wanadamu tunapata malezi kutoka kwa wazazi wetu waliotuzaa na mara nyingine Watoto hulelewa na walezi kama vile bibi, shangazi na watu wengine, watu hawa wanaweza kuwa na uhusiano wa kifamilia na mtoto wanaemlea au wanaweza kuwa hawana uhusiano wa kifamilia.
Hivyo basi kila kijana anaepambana ili kufanikiwa katika maisha na kila kijana ambaye amefanikiwa kimaisha, ni muhimu akumbuke kwamba yeye ni mwanadamu na amepitia katika hatua tofauti ambazo alihitaji uangalizi wa hali ya juu kutoka kwa wazazi au walezi wake, miongoni mwa vitu ambavyo vijana wengi hutusaidia kutoka kwa wazazi wetu ni kutusimamia na kutuongoza ni katika suala la kusoma, kutupatia mitaji katika biashara zetu na vilevile wazazi wetu hutushauri katika mambo mbalimbali yakimaisha ili tuweze kufika mbali na tuwe na Maisha mazuri.
Hivyo tukiachana na mchango mkumbwa wa wazazi au walezi wetu wakati tulipokuwa hatuna uwezo wowote wakati wa utotoni ambapo tuliwategemea wao katika kutupatia chakula, mavazi, matibabu na kutulinda na kutuhakikishia usalama, tumekuwa tukiwategemea wazazi au walezi wetu katika masuala mbalimbali kama vile kutusomesha katika shule mbalimbali, vilevile vyuo na maeneo mengine ambapo wazazi au walezi wetu huwa ndio tuna wategemea katika kutulipia ada za shule na michango mingine.
Wazazi au walezi wetu hupitia katika changamoto mbalimbali wakati wa kuhakikisha wanatutimizia mahitaji yetu sisi kama Watoto wao, lakini wengi katika wazazi wetu huwa hawakati tamaa japo kwa kuhakikisha Watoto wao tunapata chakula cha kila siku.
Wapo wazazi au walezi ambao hupambana Zaidi na kwa muda mrefu ili kuhakikisha vijana wao wanafanikiwa kusoma katika shule mbalimbali na vyuo mbalimbali, lengo la wazazi au walezi hawa ni kuhakikisha kwamba Watoto wao wanafanikiwa katika haya Maisha yao wanayoishi hapa duniani, wazazi wengi husema “sipendi Watoto wangu wapate shida kama mimi” hapo ndipo panakuwa chanzo kikubwa cha hawa wazazi wetu kuwa wapambanaji na kuhakikisha wanapatupatia Watoto wao mahitaji yote ya msingi ambayo yatatuwezesha watoto wao kufikia malengo yao, kwa mfano mtoto akitaka kuwa muhandisi au daktari wazazi au walezi wengi hupambana ili kuhakikisha mtoto wao anafikia malengo yake.
Ukijaribu kutafakari kwa undani Zaidi utagundua ni kwa namna gani wengi katika wazazi au walezi wetu wanapambana ili kuhakikisha Watoto wao tunaishi katika mazingira mazuri ukilinganisha na yale mazingira ambayo wao wanaishi, kiukweli wengi katika wazazi au walezi wanapenda Watoto wao wafanikiwe Zaidi katika Maisha ndio maana takribani mara zote wazazi na walezi wetu hupambana sana ili kuhakikisha sisi kama vijana na Watoto wao tunafanikiwa.
Mara nyingine wazazi au walezi wetu hutumia hadi nguvu kutulazimisha tufanye mambo ambayo yanatunufaisha sisi wenyewe, kwa mfano wazazi huwalazimisha watoto wao waende shule katika wakati ambao wao walikua hawajui umuhimu wa kwenda shuleni, vilevile wazazi huwalazimisha Watoto wao kumeza dawa wakati wanapoumwa ili wawe na afya njema, na wakati mwingine wazazi au walezi wetu hutulazimisha tufanye kazi kwa bidi ili tuzoee kazi na tuwe wapambanaji.
Kwa masikitiko makubwa, licha ya jitihada zote ambazo wazazi au walezi wetu huzifanya ili kuhakikisha Watoto wao tunafanikiwa, baada ya kufananikiwa sisi Watoto hatukumbuki kurudisha fadhila kwa wazazi wetu. Ni jambo la kusikitisha sana katika jamii zetu vijana wengi waliofanikiwa kuto kuwajali na kuto kuwatunza wazazi wao, jambo hili linaendelea kuota mizizi katika jamii zetu siku hadi siku.
Malalamiko ya wazazi wetu huko vijijini yanaongezeka kutokana na wao kutokuweza tena kujitafutia mahitaji yao kwasababu hawana nguvu tena za kujitafutia mahitaji yao ya muhimu kama vile chakula, mavazi na vitu vingine. Sio jambo la sawa kwa mtu aliyefanikiwa kimaisha kuishi mjini na familiya yake wakati huo wazazi au walezi wake amewaacha kijijini na wanaishi katika mazingira magumu sana.
Huko vijijini kuna wazee wengi amboa wanaishi Maisha mugumu sana, lakini Watoto wao wapo mijini wanafurahia ujana na mafanikio ambayo kwa kiasi kikubwa yameletwa na wale wazee walioko vijijini ambao hawaijui chai Ya sukari miezi sita, chapati ndio wanakaribia kuzisahau kabisa hata zilivyo, wazazi wanakuwa ombaomba, wakati Watoto wao wapo mijini wakishindana kulewa pombe nyingi na kutafuta sifa katika mambo mbalimbali kama vile wanawake wengi, magari makubwa, majumba na vitu vingine.
Kumbuka, kama wewe ulivyo na nguvu hivyo na wazazi wako walikuwa na nguvu hivyohivyo, lakini sasa hivi zimewaishia, hivyo huu ni muda wako sasa kuwalea na kuwarudishia fadhila kama walivyo kutunza wewe japo kwa kuhakikisha ulipata chakula japo mara moja kwa siku na sehemu ya kulala, na huo ndio ulikuwa uwezo wao, hivyo basi tukiwaacha wazazi wetu vijiji bila kuwajali, basi na MUNGU hatatubariki katika shuguli zetu, familia na kazi zetu pia hazita barikiwa kutokana na vinyongo na malalamiko ya wazazi wetu, lakini pia tuache kuwasimanga,kuwatukana na kuwabuguzi wazee wetu kwa sababu hao ni wazazi wetu na tuwatumie kama marafiki zetu wakaribu na MUNGU atatubariki sana.
BY : MKAKA WA CHUO.

Upvote
2