Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Nchi ya Uzberkistan inaanza kuibadili Gesi Asilia kuwa petroli, dizeli, mafuta ya ndege, mafuta ya taa, na Gesi ya LPG ya kupikia.
Nchi ya Uzberkistan ina mpango wa kuanza uzalishaji katika kiwanda chake za kwanza cha kubadili Gesi asilia kuwa mafuta ya magari na ndege (GTL).
Kiwanda hicho chenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 3.6 ambacho kipo katika wilaya ya Guzar katika mkoa wa Kashkadarya kitasaidia nchi hiyo kupunguza utegemezi wa mafuta yanayoagizwa kutoka mataifa ya nje.
Kiwanda hicho kinamilikiwa na kampuni ya serikali ya mafuta na gesi Uzbekneftegaz kwa kushirikiana na Sasol ya Afrika Kusini.
Kiwanda hicho kitakua kina chakata gesi asilia ili kuzalisha mafuta safi ya magari na ndege. Kuanza kwa hicho kiwanda kutaipunguzia Uzberkistan kuagiza dizeli na mafuta ya ndege (Jet fuel) kutoka mataifa ya nje.
Kiwanda kinauwezo wa kuchakata kyubiki mita bilioni 3.6 za gesi asilia kila mwaka. Kitakua kinazalisha tani milioni 1.5 za mafuta ya magari na ndege yenye ubora.
Kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani laki tatu na elfu saba za mafuta ya taa (307,000t of kerosene), tani laki saba elfu ishirini na nne za dizeli (724,000t of diesel), tani laki nne elfu thelathini na saba za naphtha (437,000t of naphtha), na tani elfu hamsini na tatu za LPG (inayofanana na gesi za akina Oryx, Mihani na Lake). Naphtha itatumika kuzalisha mafuta ya petroli yenye ubora wa hali ya juu.
Bidhaa hizo za mafuta zitasambazwa nchini ili kufikia mahitaji ya ndani and pia zitasafirishwa kwenye mataifa ya nje.
Kiwanda hiki cha kubadili gesi asilia kuwa mafuta kina key production facilities nne ambazo ni:
1.Utilities supply plant,
2.Synthesis gas production plant,
3.Synthesis liquid production plant, and
4.Product work-up plant.
View attachment 1850375
Process nzima inaitwa GAS TO LIQUIDS (GTL). Unaweza kuiangali kwenye hizi video hapa chini kisha ukatoa maoni yako.