JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Tangu kutokea kwa ugojwa wa #COVID19 unaosababishwa na Virusi vya Corona watu na taasisi nyingi zimehamasika kuweka Vitakasa Mikono katika malango ya kuingia katika nyumba au ofisi za taasisi husika
Hata hivyo kundi la Watu wenye ulemavu wamekuwa wakishindwa kufikia huduma hiyo kutokana na kufungwa au kuwekwa sehemu ambayo si rahisi wao kufikia
Jamii Forums inakukumbusha kulizingatia kundi hili (watu wenye ulemavu) ili na wao waweza kijilinda dhidi ya #CoronaVirus pindi wanapoingia au kutoka katika taasisi au nyumba
Upvote
0