Ndugu Wananchi:
Hatukuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa ili kujenga chuki miongoni mwa Watanzania. Hivyo, tuwaogope sana wanaohubiri chuki kwa kisingizio cha ushindani wa kisiasa.Ushindani tunaoutaka sisi ni wa hoja, ni wa fikra, ni wa mikakati na mipango ya maendeleo. Tunashindanisha Ilani za Uchaguzi za Vyama. Ningependa vyama vyote vya siasa viwe na malengo makuu yanayofanana–umoja, amani, upendo,maendeleo na ustawi wa taifa na wananchi. Kinachotutofautisha na tunachoshindania kiwe mipango na mikakati ya kufikia malengo hayo. Tunapoingia kwenye mwaka wa uchaguzi, napenda vyama vyote, na wananchi wote, turejee kwenye maadili haya na malengo haya.
Nasema maneno haya kwa uchungu wa nchi yetu, na sijui nitumie lugha gani tuelewane. Tushindane kwa sera na mikakati; tusishindane kwa ubabe na vitisho. Na sera haiwezi kuwa KUINGIA IKULU. Sera ya kuingia IKULU ni sera ya ubinafsi; tena ubinafsi wa hali ya juu. Maana, hoja si kwenda IKULU; hata tausi wanaishi IKULU. Hoja ni unakwenda IKULU kuwafanyia nini Watanzania. Atafutaye kuongoza Watanzania lazima awe mnyenyekevu, anayejua anatafuta kutumwa, hatafuti kutumikiwa. Hayo ndiyo maadili ya Taifa waliyotuachia waasisi wetu.
Nataka mwaka wa 2005 tujikumbushe maadili hayo, na tukubaliane miongoni mwa vyama vyote vya siasa kuyazingatia na kuyafuata. Tarehe 28 Juni 1962, wakati akiwasilisha Bungeni mswada wa kuifanyailiyokuwa Tanganyika kuwa Jamhuri, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alizungumzia kwa kina umuhimu wa kuwa na maadili ya kitaifa, yanayozingatiwa na kila raia mwema na kila kiongozi.Alisema:
Hoja lazima ijengwe kwamba hatimaye kinga madhubuti ya haki za raia,uhuru wa raia, na mambo yote wanayoyathamini, hatimaye yatahifadhiwa na maadili ya kitaifa.
Taifa linapokuwa halina maadili yanayowezesha Serikali kusema. Hatuwezi kufanya hivi, huu si U-Tanganyika Au watu kusema: Hili hatuwezi kulivumilia, huu si U-Tanganyika. Iwapo watu hawana maadili ya aina hiyo, haisaidii sana hata kama wangekuwa na Katiba iliyoandikwa vizuri sana. Bado raia wanaweza kukandamizwa.
Tunachopaswa kukifanya ni kujenga maadili ya taifa hili, kila mara kuimarisha maadili ya taifa hili, maadili yatakayomfanya Rais yeyote yule kusema, Ninayo madaraka ya kufanya jambo hili chini ya Katiba, lakini sitalifanya, maana huu si U- Tanganyika. Au kwa watu wa Tanganyika, iwapo wamekosea na kumchagua mwenda wazimu kuwa Rais, mwenye madaraka ndani ya Katiba ya kufanya XYZ, akijaribu kufanya hivyo, watu wa Tanganyika waseme, Hatutakubali hili lifanyike, hata alitake Rais au Rais maradufu, hatulikubali, maana huu si U-Tanganyika.‘ ‖
Ndugu Wananchi:
Nimenukuu kwa kirefu maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kwa sababu naamini hapa tulipofika kwenye mageuzi ya kisiasa tunaanza kutetereka na hivyo tunahitaji sana kuzingatia busara zake. Naomba wananchi mniunge mkono kuwa mwaka 2005 uwe wa kurejea kwenye maadili ya kitaifa — maadili ya kutetea kwa nguvu zote uhuru, umoja, amani, utulivu, upendo na mshikamano. Huu ndio uwe U -Tanzania.
Tuwe na maadili yanayotusukuma kupinga kwa nguvu zote ubaguzi,udini, ukabila, chuki na visasi. Mwaka 2005 tukatae kiongozi wa dini kutuchagulia chama au mgombea. Tuseme hapana, huu si U-Tanzania. Tukatae chama au kiongozi wa chama anayetumia udini, ukabila au umajimbo kutafuta madaraka.Tuseme, hapana! Huo si U- Tanzania.Tumkatae kiongozi wa siasa, au hata raia mwenzetu, ahubiriye chuki, uhasama na ubaguzi wa aina yo yote ile.Tuseme hapana!Huo si U-Tanzania.
Wananchi mkiamua, na kukubaliana nami, nchi yetu itang‘oa mbegu zote zinazopandwa za chuki, ubaguzi na fujo, na kuturejesha kwenye maadili ya ki-Tanzania. Hiyo ndiyo changamoto kubwa kuliko zote mwaka wa 2005. La sivyo,katika miaka michache ijayo, Tanzania haitakuwa tofauti na nchi nyingine za Kiafrika wanakouana wenyewe kwa wenyewe. Na vurugu za kisiasa ni kama yule jini kwenye hadithi za Alfu Lela Ulela; akishatoka kwenye chupa ni vigumusana kumrejesha.
Tumwombe Mungu apishie mbali, lakini pi kila raia mwema adai kwa bidii zote kuheshimiwa kwa maadili yetu ya kitaifa. Tunapoelekea kwenye uchaguzi watakuja wengi kwa kivuli cha Asasi Zisizokuwa za Serikali ati kutuelimisha kuhusu demokrasia. Wanaoijua Tanzania, na raia wake, wanajua sisi si mbumbumbu wa siasa wala demokrasia.
Sisi ni mfano kwa wengine, mfano wa uhamasishaji wa kisiasa na kimaendeleo. Sisi pia ni waumini wa uhuru, usawa na kujitegemea.
Na SISI WENYEWE NDIYO WAJUZI NA WATETEZI WA U-TANZANIA!