Tuwaombee sana vijana wetu

Tuwaombee sana vijana wetu

Joined
Feb 13, 2024
Posts
80
Reaction score
204
Kama Kuna vijana wanapitia hali ngumu ya kimaisha basi ni pamoja na vijana wa kitanzania.

Just imagine kijana hanakwambia hana mpango wa kuoa kama ni upwiru atachukua buku Tano anakwenda kumalizia kwa dada poa na maisha yanaendelea.

Vijana wengi wa kitanzania hawana vyanzo vya kimapato zaidi ya kutegemea michezo ya kubahatisha daily vijana mifukoni wamejaza mikeka wanatembea na ndoto ya kumiliki mamilioni kwa kubahatisha.

Matajiri wa nchi hii wamewageuza vijana wengi kama mitaji yao badala ya kuwasaidia wao wamewageuza mateja wa vinywaji vichafu, vijana wengi ni mateja wa pombe chafu visungura, double kick, k vant na energy drink.

Tunaitaji maombi ya kitaifa ili kuwanusuru vijana wetu.
 
Nawashauri pia wasin'gan'ganie mjini, mjini unaitaji connection kubwa sana ili utoboe sio km vijijini na miji midogo.

Wengine wamekimbia fursa ndogondogo vijijini/miji midogo zinazoweza kumpa ela ya kujikimu wakakimbilia mjini kwenye mrundikano wa watu wengi sana wanaoitaji fursa. Kuna mwingine hajasoma kabisa,hakuna ajira yoyote anayoitegrmea siku za usoni ila yupo mjini amekaa tu anakwambia "one day yes" hakuna utajiri wa miujiza,

Hakuna issue unayoifanya Dar, unalala njaa, unapata ela ya pango kwa shida lakn umepan'gan'gania. Wakat kuna miji midogo zinazokuwa km Kahama na nk utaishi chumba bei chee, vyakula bei rahisi, na vibarua kibao. Ukikaa miaka kwa miaka ulizopoteza mjini utatengeneza mtaji wako utarudi dar ufungue ka kibanda cha Mpesa km unapenda uishi huko.
 
Nimesoma huku machozi yakiwa yananilenga kimsingi sisi vijana tunapitia hali ngumu sana kimaisha usilaumu vijana kukataa kuoa washafanya tathmini kama kula yake mpaka mkeka utiki atahudumia vipi familia ya mke na watoto.
 
Kuna mahala nilienda kwa jamaa yangu nilikaa kama week aisee ni hatari. Nilichogundua wale vijana kwanza ni wale wanaopiga simu kujifanya wahudumu wa mitandao wanawatapeli watu ila wakupata pesa kuna duka hapo jirani ndiyo wanakuja kujiburudisha baada ya kazi ni mwendo wa hivyo vinywaji ulivyotaja na mixing na energy drink kuanzia asubuhi mpaka jioni wengi wao si kama wanapenda ila aijra hakuna.
 
Na 80% ya vijana hao asubuhi wanajadili Simba na Yanga
 
elimu dunia ndio itakuwa ukombozi kwa vijana siyo kuegemea kwenye maombi tuu
kuwa na seminar ambazo zitakuwa rafiki kwa vijana kuzifikia kuna mengi sana ya kimaisha vijana tunayakosa angalau ile elimu ya jando ilikuwa inawasaidia vijana wa nyuma (wazee waleo)
baada ya kuiyacha ile na kukumbatia ya mzungu mtaani hali imekuwa mbaya
 
Back
Top Bottom