Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
HIvi nyie Watu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) hapa Tabora huwa mnachukuliaje Wananchi? Tangu wiki iliyopita Kata ya Mwinyi hakuna huduma za maji na hata yanapotoka yanakuwa machafu na yanatoka kwa muda mfupi, mnataka Watu tuishije!
Mwinyi iko Manispaa ya Tabora inakuwaje Manispaa tunakosa maji na hawa watu wapo? Mamlaka au viongozi mnaohusika angalieni hili suala, linatuumiza Wananchi, tunapata wakati mgumu kupata huduma hii na tukiipata tunalazimika kutumia gharama kubw aya usafiri na hata kununua sehemu tofauti.