Tuwashauri hawa Form Four graduates sasa wachukue hatua za haraka

Tuwashauri hawa Form Four graduates sasa wachukue hatua za haraka

melech

Member
Joined
May 29, 2013
Posts
62
Reaction score
25
Amani kwenu!

Tunafahamu kuwa matokeo (version 2) ya hawa Form Four yametoka. Nashauri popote pale tutakapowaona tuwahimize sasa wachangamke na hatua zinazofuata bila kupoteza muda.
Ninamaanisha wale ambao matokeo yao yanaruhusu, wachangamkie suala la shule kwa Form Five, manake nimesikia wataanza mwezi wa saba, just one month ahead. Najua kuwa serikali itawapangia shule, lakini tunajua sio wote. Hivyo tuwashauri wale wa kuweza kutafuta private schools wafanye hivyo mapema, tumeshayaongea matokeo sana.

Tufanye wema pia kuwashauri na kuwaelekeza options nyingine kama certificate courses mbalimbali zilizopo, kwa kadri ya upeo wetu.

Tukimwona aliyefeli kabisa pia, hebu tuangalie tunaweza kumshauri nini cha kumsaidia.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom