Tuwatambue wafanyabiashara wakubwa wa mafuta nchini

Tuwatambue wafanyabiashara wakubwa wa mafuta nchini

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Toka mwaka 2011 tunahangaika sana na suala la nishati ,hivi ni wafanyabiashara gani wenye kuhodhi biashara hii Tanzania?

Kama unawafahamu wataje humu jamvini.

Rais Kikwete aliwahi kunukuliwa kuwa hawa jamaa huwa hawagusiki ukiwagusa tu unapata shida.
 
Matatizo yenu hayasababishwi na wafanyabiashara wakubwa, acha chuki na ujinga
Mjinga ni wewe unayedhani Oilcom baba zako na kwayo watakuonea huruma kuliko wao kutaka faida maradufu
 
Toka mwaka 2011 tunahangaika sana na suala la nishati ,hivi ni wafanyabiashara gani wenye kuhodhi biashara hii Tanzania?Kama unawafahamu wataje humu jamvini.
Rais Kikwete aliwahi kunukuliwa kuwa hawa jamaa huwa hawagusiki ukiwagusa tu unapata shida.
Kikwete si mtu wa kumsikiliza hata siku moja, yeye mwenyewe hajielewi.
 
Sukuma gang mmejipanga kweli kutishia nyau, mtu wenu Ikulu hayupo tena,

Na Samia bado yupo sana, mpaka 2030, na ikifika 2030 tutaandamana tumuongezee mingine kumi inamhusu mpaka 2040, hutaki kanywe sumu,
 
Mjinga ni wewe unayedhani Oilcom baba zako na kwayo watakuonea huruma kuliko wao kutaka faida maradufu
Ni mpumbavu pekee na mwenye roho mbaya ya kishetani atawalaumu wafanyabiashara kwa lolote badala ya kulaumu mamlaka husika za kuwadhibiti (hasa serikali).

Mfanyabiashara yeyote lengo lake ni kupata faida. Kama anaona mianya ya kupata faida mara dufu au mara milioni,atahakikisha anaipata hiyo faida.

Msituletee upumbavu wenu sisi wafanyabiashara. Wekeni sera nzuri,mazingira mazuri,utaratibu mzuri,udhibiti mzuri,kodi rafiki,muone kama kuna mfanyabiashara atafanya figisu.

Serikali na taasisi zake zimefeli mnasingizia wengine.
 
Ni mpumbavu pekee na mwenye roho mbaya ya kishetani atawalaumu wafanyabiashara kwa lolote badala ya kulaumu mamlaka husika za kuwadhibiti (hasa serikali)...
LOooh, hili jibu limenitoa jasho mkuu 'residentura'.

Umesema vyema kwa upande mmoja, lakini nadhani unasahau pia kwamba kati yenu (wafanyabiashara) kuna mapapa yasiyo amini kama unavyoamini kama wewe. Wao kazi kubwa ni kushindana na serikali kwa njia yoyote ile, ikiwemo kuwatumia waliomo serikalini kwa manufaa yao, bila kujali manufaa ya nchi.
 
Waswahili husema, "nia njema hailogwi" serikali inakosa dhamira njema katika kushughulikia ustawi na usawa nchini, kwa ufupi serikali imewekwa mfukoni na wagiriki wachache
 
LOooh, hili jibu limenitoa jasho mkuu 'residentura'.

Umesema vyema kwa upande mmoja, lakini nadhani unasahau pia kwamba kati yenu (wafanyabiashara) kuna mapapa yasiyo amini kama unavyoamini kama wewe. Wao kazi kubwa ni kushindana na serikali kwa njia yoyote ile, ikiwemo kuwatumia waliomo serikalini kwa manufaa yao, bila kujali manufaa ya nchi.
Ndio maana nikaandika kuwa serikali na vyombo vyake vinatakiwa kuwa makini.

Kama ilivyo binadamu wote hatufanani. Wapo binadamu wana roho na mioyo ya kishetani,ndivyo ilivyo kwa wafanyabiashara.

Kikubwq ni kwa serikali makini kuweka usimamizi makini ili wafanyabiashara tusitengeneze "cartels" na kulala kitanda kimoja na serikali.
 
Mafuta, vijana huita mkojo wa Muarabu..

Kwa nini nchi za kiarabu na waarabu ni matajiri sana kwa biashara hii? kwanini kila anayechimba na kufanya biashara hii na akaisimamia vizuri anakuwa tajiri..?..

Kwanini tunasema bei ya Mafuta Tanzania ni kubwa? Nchi gani ambayo haina na haichimbi mafuta bei ya mafuta ni ndogo?....
 
Back
Top Bottom