Kupigania ukombozi wa nchi ni harakati zote zenye lengo la kuitoa nchi katika mifumo ya dhuluma katika kipindi chochote. Huku kupo sawia na kupigania uhuru kwa kina Mandela, Nyerere, Samora, Museveni, Garang, au kina Kagame wa Rwanda huko.
Kwamba makwetu leo dhuluma zimetamalaki tena hadi kufikia kwenye uporaji wa maisha ya watu, kwa hakika kunahitajika ukombozi wa "caliber" zile zile za enzi za uhuru.
Jukumu la ukombozi haliwezi kuwa la mtu mmoja, kikundi au chama kimoja; bali wananchi wa matabaka yote wenye kuchukizwa na dhuluma au "status quo."
Humo hakuwezi kuwa na nafasi ya ubaguzi wa kivyama, kikabila, kikanda, kidini, kimkoa, nk.
Humo watakuwamo ma CCM, Chadema, ACT, CHAUSTA, CHAUMA, UDP, CUF nk.
Humo watakuwamo watanganyika kwa wazanzibari, wasukuma, wachaga, wahaya, wandengereko, nk.
Humo watakuwamo wamatumbi, waarabu, wahindi, nk.
Kwamba kinachotukutanisha sote pamoja ni kiu ya kupata haki au kiu ya ukombozi wa nchi yetu dhidi ya dhuluma, nani anaweza kujidhania kuwa bora au mpambanaji zaidi kuliko nani?
Kwamba kumbe tunaweza kuwa na chuki na nani baina yetu hata kama kaongoka juzi?
Kwani yuko wapi anayefurahishwa na tekaji za watanzania wenzetu? Ni CCM, Nchimbi, Tulia au Samia?
Tuwapelekee mialiko washirika wetu wote hawa katika haki, kokote waliko. Tukapate kuwakemea watesi wetu katika umoja wetu. Nani asingependa kuujua ukweli? Nani anaweza kupinga umuhimu wa uchunguzi huru?
Kwamba nani asiyeuona umuhimu wa Sep. 23?
Pamoja na yote, tujiangalie wandugu kama tuna chuki na awaye yote katika jitihada hizi za ukombozi; bila kujua:
"Tunaweza kuwa wapigania ukombozi mamboleo tusiokuwa na mchango wowote kwa taifa hili."