Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Kama taifa, ninashauri tutengeneze mkakati mzuri wenye tija tuwauze Wamachinga nje ya nchi kama #nguvukazirahisi (wakafanye kazi zile ambazo ni labour intensive/mitulinga lakini wanaretain uraia wao wa Tz) ikiwa hatuna mpango maalum wa kuwatumia hapa nyumbani. Mbona Wachezaji wanauzwa! Korea Kusini Nannies alone walioko Middle East wanaiingizia nchi yao 30% ya GDP, Kenya diaspora wanaliingizia taifa 16% ya GDP kabla ya Corona kulipuka, Tz diaspora wanachangia kiasi gani cha GDP? Siyo kwamba diaspora ya Tz ni sawa na Wamachinga walio nje ya Tz? Kwasababu hatuna takwimu zao, hatujui wanachangia kiasi gani kwa pato la taifa ili tuzidi kuwafungulia wengine wapya waende nje? Taifa lije na mpango kabambe salama wa kuwauza Wamachinga (rasilimaliwatu) nje ya nchi kwa tija ya taifa. Naamini baadhi yetu walioko humu walio na white-colar occupations wataziacha na kukimbilia kuuzwa nje ya Tz kama Wamachinga pia (ikumbukwe kuna graduates wengi sana ni Wamachinga wakiwemo Masters Holders ambayo hii ni sawa na INTELLECTUAL ASSASSINATION), pia kuna baadhi yetu humu huenda tumewaajiri Wamachinga lakini tumekataa ku-declare interest kwenye mjadala huu. Kwenye dunia hii hii zipo nchi ambazo Commercial Sex is legalized, is it death sin tukicommercialize Umachinga ama ndani au nje ya nchi? Kuna wakati Tz diaspora walimuomba JPM wafadhili ujenzi wa Muungano Bridge kati ya bara na visiwani kama sehemu ya fadhila zao kwa taifa JPM hakuwakubalia, swali je, wangekuwa Wamachinga au hata Wafanyabiashara na Wafanyakazi hapa nyumbani wangekuwa na fedha za kujenga hilo daraja? What if kama tukizidisha kupeleka watu/Wamachinga officially kwenye diaspora si faida itaongezeka kwa taifa? Massive population pressure kwa nchi ambayo haina mpango jadidifu wa ku-utilize rasilimaliwatu ni hatari kwa nchi husika. (usichanganye hii na biashara ya utumwa bali zaidi ni labour-migration-protocol sort of) . Take this homework and bring the solutions for assessment.