Tuwe makini- mafataki ( pedofiles) wengi tunao majumbani mwetu.


hahahaha! Cheusie hata kama mimi nitalala chumbani kiukweli nitaumia sana kuona watoto wanalala sebuleni kwasababu mimi ndio nitakuwa nimeharibu utaratibu. Inawezekana nikang'ang'ania kulala nao au mimi ndio nikalala sebleni. Baada ya hapo nitakuwa nikija kwako silali. Lol.
 
Unataka kutest kina kwa mguu wako?
Hadi akiwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo
Lakini kama kuna nafasi sitataka kumuweka mwanagu majaribuni
 
Unataka kutest kina kwa mguu wako?
Hadi akiwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo
Lakini kama kuna nafasi sitataka kumuweka mwanagu majaribuni

hakuna anaependa kumweka mwanae majaribuni ni mazingira tu yanafanya wazazi wanaweka watoto wao majaribuni bila kukusudia. Mlinde mwanao kadri uwezavyo na wakati unamlinda ajue unamlinda dhidi ya nini.
 

thanx kwa huu ufafanuzi,kuna umri watoto bado ni wadogo hata kama ukiwafundisha bado mtu mzima,anaweza kuwarubudi,mfano mdogo tu ni kwamba,mtoto anaweza kuwa amefanya kosa analojua ni kubwa mama au baba akijua,huyu pedofile(ndugu) anaweza kutumia hiyo kumtisha mtoto kuwa ukikataa nakusemea,so hapo hata mafundisho yako yanaweza yasisaidie.
pia nimesema wageni wakuja na kuondoka kesho keshokutwa huwezi kuwalaza sebuleni ila wale ndugu waliokuja kuishi kwako kabisa kila siku wapo hao,sasa sio wageni,ni sehemu ya familia yako na hao ndio nitakaowalaza sebuleni au jikoni ili wanangu walale wenyewe vyumbani mwao.
ila sikusema wageni walale jikoni.
 
Mi Avatal yako imenifanya niondoke nirudi nyumbani kusalimia kidogo...
 

hata ukilala nao chumbani kama unawaza kuvuruga utaratibu basi hata huko chumbani bado utakuwa umewavugia wanangu utaratibu maana labda walikua wanalala wawili kitandani leo aunty Hus amekuja inabidi walale watatu kwa kujibana.Hutjisikia vibaya,hata ukikangania kulala nao nitatafuta sababu yakukudanganya na ukarimu nilionao wala hutajisikia vibaya,nitakudanganya,wanajikojolea,au wanalala vibaya,au vyovyote tu lkn hutajisikia vibaya na nitahakikisha ukiondoka unamiss kuja kututembelea tena.
 
Unataka kutest kina kwa mguu wako?
Hadi akiwa na uwezo wa kufanya maamuzi hayo
Lakini kama kuna nafasi sitataka kumuweka mwanagu majaribuni

si ndio hapo sasa,hatari zipo nyingi lkn zinazoepukika na tuziepushe.
 

hahaha! Umenipa funzo kuwa natakiwa kujenga nyumba ya vyumba vitano minimum vya kulala tu. Sitotaka kutesa watoto wala wageni watakaokuwa wanakuja kunitembelea na kulala. Ahsante.
 
hakuna anaependa kumweka mwanae majaribuni ni mazingira tu yanafanya wazazi wanaweka watoto wao majaribuni bila kukusudia. Mlinde mwanao kadri uwezavyo na wakati unamlinda ajue unamlinda dhidi ya nini.

nimependa ulichoandika Hus,mazingira hayo tunayoyaweka watoto majaribuni bila kukusudia ndio hayo niliyoyaongelea,unasema watoto kadri ya tuwezavyo,sasa ugumu wa kuwalinda watoto dhidi ya pedofiles ambao wanaweza kuwa ni ndugu wanaoishi majumbani kwetu uko wapi,ikiwa inawezekana kuwatenga watoto wakalala peke yao na ndugu zetu wakalala peke yao.
 
Ndio maana nadhani ni busara usiruhusu watoto wajenge hofu juu yako kiasi kwamba wakisikia "ntamwambia mama/baba yako" mkojo unachuruzika.
Binafsi style yangu ya malezi nikiwa na mtoto mkubwa mkubwa itakua kuNEGOTIATE nae. Badala ya kumcharaza tu mboko mpaka tuogopane ntamkanya kwa maneno, ntajitahidi kumweleza madhara ya kosa lake kwa namna ambayo ataacha mwenyewe bila hata kuhisi ameshurutishwa. Kwa style hiyo hata akiambiwa "ntamwambia mama yako" anajibu "utajiju". . Lolzz. . .
 
hahaha! Umenipa funzo kuwa natakiwa kujenga nyumba ya vyumba vitano minimum vya kulala tu. Sitotaka kutesa watoto wala wageni watakaokuwa wanakuja kunitembelea na kulala. Ahsante.

kama uwezo upo hivi ndivyo inavyopasa iwe,ila kama nyumba ni ndogo inabidi ufuate ushauri wangu.ahsante kwa kushukuru.
 

kuna wazazi ni wakali kiasi kwamba mtoto akifanya kosa,anapata homa maana hapati picha itakuaje baba akirudi,ila tuseme ukweli wababa wengi ni wakali sana aisee,yaani huwezi hata kumtania baba yako,au siku akikutania kidogo huwezi hata kuendeleza utani ,unabakia tu kucheka unatamani lkn kicheko hakiji sbb umezoea kumuogopa.
 
kama uwezo upo hivi ndivyo inavyopasa iwe,ila kama nyumba ni ndogo inabidi ufuate ushauri wangu.ahsante kwa kushukuru.

dah! Ushauri wako siwezi kufata bora niwaambie wakija kwangu hakuna kulala. Waje na kuondoka au nilale na watoto na wao walale chumbani.
 

Nashukuru Mungu niliobahatika kuishi nao pamoja na kwamba walikua wanasimama kidete tuwe na discipline bado tulikua tunakaa wote sebleni na kucheka mida ya jioni na weekend. Hii ni zawadi nzuri sana kumpa mtoto. . . Kumfundisha adabu sio lazima umfanye akuogope.Sema wengine wanachanganya WOGA na ADABU. Matokeo yake mtoto akitoka nje tu ajirusha huko mpaka anadondoka.
 

kweli kulea ni kazi,mim nataka wageni,nafurahia sana,na hata nikiwa na watoto nitapenda wageni waendelee kuja,na nitawakirimu wageni wangu vizuri ili wanangu wajifunze siku wakiwa na makwao jinsi ya kukirimu wageni,ila ndio kama hivyo,wanangu is my first priority,lazima niwalinde,kwani kuna shida gani wanangu wakilala sebuleni,mgeni alale chumbani bila kubughuthiwa na watoto ambao wengi labda ni vikojozi.
 
dah! Ushauri wako siwezi kufata bora niwaambie wakija kwangu hakuna kulala. Waje na kuondoka au nilale na watoto na wao walale chumbani.

pouwa,
ila ningefurahi kama utanieleza kwa kifupi jinsi ulivyonielewa,labda kunaweza tokea nafasi yakueleweshana zaidi tukaelewana.
 
pouwa,
ila ningefurahi kama utanieleza kwa kifupi jinsi ulivyonielewa,labda kunaweza tokea nafasi yakueleweshana zaidi tukaelewana.

hahahahahaha! Cheusi bana, utafikiri tupo darasani. Ticha na denti. Lol. Nimekuelewa vizuri mamii. Nimekuelewa namna unavyotaka kuwalinda watoto na ndugu ambao unahisi wataharibu watoto hasa nyakati za kulala. Lol. Kifupi nimekuelewa kuhusu ulinzi na malezi yako kwa watoto yatakavyokuwa.
 

ofcoz tupo darasani,au unadhani ile siku ulivyograduu ndo umelikimbia darasa,
okay,bado sijaridhika na summary yako,nilidhan ungegusia jikon na sebulen ktk huu ufupisho,sawa naomba nisikuchoshe,ila naomba nihitimishe kwa kuweka mkazo kuwa,wageni wangu sitawalaza jikon ktk harakati za kuwalinda watoto mpenzi wangu,watu watakaolala sebuleni au hata ikibidi jikoni LOL,ni wale ndugu ambao wanaishi home kwangu na hawatarajiwi kuondoka karibun,yaani hao sio wageni,nadhani umenielewa wale ambao wamekuja kwako ili uwasaidie nao siku moja wawe na maisha yao,hao kwa kweli sion aibu kusema nitawalaza sebuleni au hata jikon,ili wanangu walale peke yao sbb kwanza kama nina nyumba ni kwamba ilijengwa ili wanangu waishi kwa raha,hivyo sitawabananisha na kuwahatarisha kufundiswa mitabia ya ajabu wkt kuna sebule na jiko.Ila mgeni wa siku moja anaondoka keshokutwa atalala chumbani watoto ndio watalala sebuleni hadi mgeni akiondoka.Natumai hii meseji itakufikia ikiwa na maana iliyokusudiwa,hichi ndicho ninachomaanisha.
 
Cheusi hizo pande unazoishi ni zipi, maana kuwa shuhuda wa huu uchafu wote ulioelezea hapa ni ngumu kidogo katika mazingira ya kawaida. Naomba nieleweke kuwa sio kwamba nasema haya mambo hayatokei ila napata shida kidogo kuelewa mazingira yanayokuwezesha wewe kushuhudia mambo yote haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…