Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
TUWE MAKINI NA HILA ZA MABEBERU, TUSIJEINGIA KINGI
Na, Robert Heriel
Jana nimekumbuka habari za mabeberu na hila zao, nikashtuka sana, nilikaribia kuwa na hofu, Sikujua hofu ile ilisababishwa na nini. Lakini nikiri kusema, akili yangu inaniambia kuwa Mabeberu wapo inchaji mpaka sasa.
Kitabia Mabeberu hawapendi watu wanaogusa maslahi yao. Hiyo ndio tabia yao na wapo hivyo mara zote na kwa uzoefu wangu wa kufuatilia historia na vyombo vya habari vya kimataifa. Mabeberu wapo tayari kupambana na yeyote atakayegusa maslahi yao.
Kwa namna hiyo, sidhani kama Mabeberu wamekuwa na furaha chini ya Utawala wa Magufuli, sidhani kuwa wamefurahia jinsi Magufuli alivyowabana kwenye sekta ya Madini kuanzia kule kwenye Mikataba ya Makinikia, na jinsi biashara ya madini kwa sasa inavyofanyika. Mabeberu wameguswa na kawaida yao hawawezi kukaa kimya bila kujibu mapigo.
Nampongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuweza kutetea rasilimali za nchi hii. Hilo lipo wazi, Magufuli amejitahidi na amekaribia kuweza kukabiliana na majizi wa Rasilimali ya nchi hii. Magufuli ninamsapoti kwenye hili, na mara zote ninasemaga hivyo, kwani ukweli ni ukweli siku zote.
Sasa Watanzania lazima tuelewe kuwa Mhe. Rais Magufuli alichokoza nyuki wabaya wasio na haya kutoka nchi za Barafu. Sifikirii kama wanamfurahia Mzee wetu huyu Magufuli. Huenda watamchekea tuu usoni, lakini kwa tabia za mabeberu ni watu wa hila, njama na kila aina ya uovu. Beberu ukimpiga, wanatabia ya kujifanya wanajichekesha kumbe wanakutafutia nafasi, wanatumia kanuni isemayo; " Pose as a Friend, Work as a Spy" kisha hutumia kanuni nyingine isemayo "Use the Surrender Tactic: Transform Weakness into Power"
Kanuni hizo wamezitumia na kuangusha waliowengi, Mathalaani Hayati Muammar Gadhafi ambaye Miaka ya themanini alikuwa moto, baadaye mabeberu wakaona watumie mbinu ya "kujifanya marafiki kumbe wanampeleleza"
Gadhafi aliwakaba kooni sana mabeberu kwenye ishu ya Nishati ya mafuta, aliwasumbua vile atakavyo. Beberu kuona Gadafi anamsimamo; ndio akatumia mbinu ya 'Kujifanya amesalimu amri, na kuugeuza udhaifu mpaka kuwa mamlakani"
Unapopambana na Mabeberu usije ukadhani ugomvi wao unaisha, ukiamua uwe umeamua kweli. Kwani ukidhani umewashinda kumbe wenzako wanatafuta ukaribu na wewe ili wakujue zaidi au wanatafuta mbinu zingine ambazo nitazieleza hapo chini.
Mhe. Rais Magufuli, lazima ajue kuwa hawa watu mapambano yao hayaishi, unapoingia field na hawa watu uwe umejitoa kikamilifu. Nafikiri Magufuli anajua jambo hili, na waliokaribu yake wanalijua hili.
Mataifa ya Iran, Korea Kaskazini,, China na Urusi yameamua moja kwa moja, na bila shaka yanamuelewa adui yao hulka yake ilivyo. Hii ndio inawasaidia. Tofauti na hapo nao wangetetereshwa mapema sana.
Mabeberu pia hupenda kutukuzwa, kusifiwa, na kuabudiwa. Mataifa yanayoyatukuza mabeberu hupewa sapoti kwa kiasi kikubwa na mabeberu licha ya kuwa rasilimali zao zinachukuliwa zaidi na hao mabeberu.
Mataifa yasiyoyaabudu, kusifia, na kutukuza mabeberu huonja joto ya jiwe. Mataifa yote yanayotukana mabeberu huingia kwenye migogoro mikubwa na mabeberu.
Tulimuona Sadamu Hussein wa Iraq alivyokuwa akiwatukana mabeberu, tulimuona, Gadafi, Tulimuona Solomon wa Iran, Tunaona Kwa Bashad Alasady wa Syria, tuliona kwa Robert Mugabe, huko kote Mabeberu wameonyesha vurugu zao kwa njia nyingi.
Mabeberu wametumia mbinu za kuangusha uchumi kwa nchi hizo, wametumia njia ya vikwazo vya kiuchumi, wametumia njia ya propaganda kwa kuwapa majina yasiyofaa viongozi wote wasiowaabudu. Wameanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya nchi hizo kwa kutumia vikundi vya kidini, kisiasa, au hata maandamano ya haki za binadamu.
Mhe. Rais Magufuli ni moja ya viongozi wa sasa barani Afrika ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwa jasiri kuwasema na kuwatukana mabeberu. Usidhani mabeberu hawamsikii, usidhani mabeberu ni watu wakuchekea watu dizaini ya Magufuli. Mabeberu hawajawahi kuwa na huruma na ushahidi huo upo.
Inafahamika kuwa Hakuna serikali yoyote duniani inayofanya mambo yake kwa asilimia mia moja 100%. Ni lazima yawepo mapungufu tuu. Na kupitia mapungufu hayo ndio Mabeberu huyatumia kama mwanya wa kuleta vuruga zao.
Kikawaida demokrasia ni moja ya dhana za mabeberu kuzichapa nchi masikini. Kama hawatatumia chama tawala basi watatumia chama cha upinzani.
Kikawaida Diini ni moja ya nyenzo za mabeberu kuzichapa nchi masikini. Kama hawatatumia Ukristo basi watatumia uislamu
Mambo hayo mawili ndio fimbo muhimu za kuzichapa nchi masikini hasa kwa bara la Afrika.
Ni kawaida kwa Mabeberu kuwatumia wapigania haki kutimiza vurugu zao. Unajua wakati mwingine mtu anaweza kuwa mpigania haki lakini asiwe na akili za kutambua hila, njama na ulaghai wa mabeberu hivyo unaweza kukuta mpigania haki akawa anatumika pasipokujua anatumika. Yeye dhamira yake ni kutetea haki na kifanya jamii yake iwe jamii bora lakini kumbe wenzake yaani mabeberu wao wana-agenda nyingine ya siri.
Nawashauri wananchi, tuwe makini hasa kipindi hiki cha Uchaguzi. Watu pigeni kura kuchagua kiongozi mnayemtaka. Atakayepita hewala, atakayeshindwa basi asiumie ilimradi awe ameshindwa halali.
Pia naishauri serikali na vyombo vinavyohusika na Uchaguzi, NEC na ZEC pamoja na vyombo vya dola, tendeni haki, anayeshinda apewe ushindi asiyeshinda apewe pole tumalize uchaguzi maisha yaendelee.
Nafahamu kuwa mabeberu wanaweza kupenyeza watu wasiowaaminifu ili wasitoe haki kwa walioshinda, kisha mabeberu hao hao wakawatumia waliodhulumiwa haki zao kudai haki, mwishowe kukawa na vurugu.
Tusihujumiwe, mara nyingi vipindi hivi ndio huwa na mambo mengi.
Pia serikali itayoingia madarakani ihakikishe yale masuala ya msingi ikiwa ni pamoja na kutenda haki na uadilifu yanazingatiwa ili mabeberu wasijepata mwanya wa kujimwambafai.
Kuna kanuni inasema; "playing people against one another, making them pursue you".
Mabeberu ndio tabia zao, wanaweza kuchezesha watu akili, upande huu na upande huu ili kuchochea vurugu.
Hatutakuwa tayari kutumiwa na mabeberu kuuana wenyewe kwa wenyewe. Amani ilindwe kwa mgongo wa haki.
Ndugu zangu, nimalize kwa kusema usikubali mtu akakutumia kudhulumu haki za wengine, mtu huyo anakuhujumu ili kuhatarisha amani ya nchi hii. Pia usikubali mtu akuingize barabarani ikiwa unajua ameshindwa katika uchaguzi.
Piga Kura, Linda kura, usiibe kura. Usifanya vurugu.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
kwa sasa Dodoma