kingjohn255
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 400
- 513
Nianze uzi huu kwa kutambua uwepo wa watu mbalimbali na wenye ufundi na ujuzi wa kila aina. Kuna kitu bado wamiliki wa magari wanashindwa kukielewa pale ambapo wamekuwa wakipeleka gari zao kwa mafundi kubadilishiwa oil na baadhi ya vipuri lakini katika utafiti wangu mdogo kwenye swala la oil na vipuri nimegundua wamiliki wanapigwa sana.
Maana unakuta wewe umemwamini fundi umemwachia gari akubadilishie oil na unamwambia kabisa niwekee oil Fulani lakini atakachokifanya kwa vile oil ile bei yake imesimama kidogo atamuwekea oil hizi maarufu za kupima ambazo bei yake kwa dumu la litre 5 linauzwa 25,000 na hazina ubora wa kuaminika na ile inayobakia anachukua.
Wewe ukija ukitumia wiki moja tu unaanza kusikia gari inaunguruma kivingine baadae unaanza kulaum oil hii mbona nimeweka juzi lakini hadi saa hii sioni muungurumo ule wa gari! Itoshe kusema ukimpelekea fundi hasa kubadilisha oil na oil filter naomba usimamie gari yako na oil nenda mwenyewe dukani ununue umpelekee na sio kununuliwa na mafundi naona wengi wanavyopigwa hivyo nimekosa uvumilivu nimeona niwasemee but naomba mafundi mnaofanya hivyo mnisamehe.