Tuwe makini na matumizi ya akili zetu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Mtu ambaye hawezi kuongoza mawazo yake vyema na kuwaza mawazo mema pekee bali akili zake zimejawa na mawazo mema na mabaya ni sawa sawa na gulio ambalo kila kitu kinauzwa humo, Humo utakuta maharage, unga, samaki, kunde, choroko katika soko hilo hilo moja ndivyo alivyo mtu anayeshindwa kuongoza jinsi anavyofikiri.
Bali akili yenye mpangilio ina utulivu na mawazo yake huongozwa kwenye mema. Akili zetu ndio kiongozi wetu. Hutuongoza kwenye mabaya au mema.
Dunia tuliyonayo ni zao la mawazo yetu na dhamira zetu ambazo huzaa matendo. Kama tunaiona ni nzuri au mbaya ni zao la matendo yetu.
We become good by doing good things and evil by doing evil things.
Akili iliumbwa kumsaidia binadamu sio kumuangamiza ikitumiwa vibaya ina madhara.
Tuwe makini na matumizi ya akili zetu. Tuzitumie vizuri kuleta manufaa kwa jamii sio maangamizi. Kuleta amani na sio mifarakano, kuleta umoja na sio utengano.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…