Lugano Edom
Senior Member
- Dec 2, 2021
- 122
- 186
Ndugu zangu,
Kwa wale mnaonunua gesi ya kupikia kwa kutumia njia ya usafiri wa bodaboda,kuweni makini sana hasa pale mtungi wa gesi unaposhushwa kwenye pikipiki.
Inashauriwa tuacheni dakika chache ili gesi itulie kabla ya kuikonekti kwenye jiko na kutumia. Ni kama chupa iliyojaa soda halafu unaitikisa kabla ya kuifungua.
Ni siku mbili zilizopita jamaa yangu alipatwa na mkasa mbaya wa mkewe kuungua na gesi kwa kiwango cha asilimia 25 na baadae kupoteza maisha baada ya kuagiza gesi na kuletewa kwa bodaboda na kuikonekti hapo kwa hapo na kuwasha jiko ili atumie. Ilimlipukia usoni mwake na kuungua. Alikuja kufia hospitalini baadae.
Jaribu kuisambaza taarifa hii kwa uwapendao, unaweza kuokoa maisha ya watu wengi na ukabarikiwa👏🏼👏🏼