Hakuna pesa iliyorudishwa! sana sana hizi ni propaganda kupitia vyombo vya habari kujaribu kupoza hii ishu baada ya kuona moto wa Richmod ulivyowapukutisha wanasiasa.
Wengi wa wamiliki wa yale makampuni hewa ni "maboya" tu na pesa ilichukuliwa na wanasiasa ambao wasingependa kuanikwa hadharani.
Hii EPA siyo mara ya kwanza; ziliwahi kuliwa pesa kwa mtindo huu huu miaka ya '80 mwishoni katika kile kilichoitwa OGL na DCP na hakuna senti iliyorudishwa! La kushangaza, hawa mafisadi wa sasa hivi, baadhi yao ni walewale waliokula pesa za OGL na DCP na wamekuwa wafadhili wakubwa wa chama tawala.