Tuwe makini tunapoendesha gari kwenye barabara ya Mandela

Tuwe makini tunapoendesha gari kwenye barabara ya Mandela

M24 Headquarters-Kigali

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
8,199
Reaction score
8,186
Ewe dereva wa gari ndogo unayetumia Mandela Road. Chukua tahadhari Sana na malori mara kadhaa nimekoswa koswa na hayo malori pamoja na kuwa Nilikua kwenye 'lane' sahihi.

NB: ukiweza tumia njia mbadala wa Mandela Road.

Tuishi
 
Ya mwisho njia hiyo imenitokea kama week mbili zilizopita kwenye mataa ya Socota pale ilikua night. Natokea Tazara na elekea Chang'ombe police, kufika mataa ya Socota natakiwa kukunja kulia, nikakaa foleni ya wanaosubiri kukunja kulia nasubiri taa, mbele yangu kuna bajaji naye anasubiri.

Sasa taa kuwa zinaruhusu wanaonyoosha kwanza halafu baadae ndiyo nyie mnaokunja kulia mnaruhusiwa, zikaruhusu wanaonyoosha kwanza, zikawa nikakuja zile lorry zinazotoka Chang'ombe mataa zinaenda Tazara, chuma zilikua speed zikapita kama 3, sasa ile ya nne ndiyo ilikua ya mwisho ishaona green tokea ilipotoka hook ikanyoosha sana sasa pale kuna kuna fulani ndogo kutokea Chang'ombe mataa kuja kuvuka mataa ya Socota uende Veternary jana ile kona ikaanza kumshinda naiona ile gali inakuja upande wetu kabisa, dereva akaikunja ikarudi kwenye lane yake na alikua na trailer ya container sasa kichwa kikarudi ila ile trailer zile tairi za nyuma zikaja kupanda ile bustani ya katikati ya barabara kidogo yaani upande wa pili wa bustani niko mimi na bajaji kama mita 1 tu.

Ile trailer na container kwa nyuma zikapanda kwa kishindo kuruka juu halafu zikatua tena barabarani kwa kishindo, nikasikia na vyuma vinasugua, moshi wa vumbi la bustani, taharuki, halafu chuma ikatembea.

Tendo la kama sekunde 2 tu hizi, ila pamoja na kwamba tulisimama sehemu sahizi ila kifo kilitaka kupiga hodi.

Taa ziriporuhusu tukakunja, nikaona bajaji na abiria wake wameshuka wote pale kituo cha mafuta wamekaa Socota wanakaa kwanza kikao. 😀


Kuna siku pia ilinikuta njia hiyohiyo Lorry limewasha indictor linakunja kulia kumbe ile indicator ya mbele na ya nyuma zinapoint tofauti, ikakunja kushoto inaovertake kwenye lane yangu, aisee.
 
Back
Top Bottom