Inategemea na situation, atleast unajua uko na mtu wa namna gani na hujiachii asilimia zote, na kama kumkatalia kamahumtaki pia inakuwa ni uamuzi wako, kwa vie ukweli unakuwa nao
Mtumeeeee! keshaibiwa mtu mume, sasa huyo mume alidhani akikudanganya ndio ataonekana bora ama?
endelea na maisha kuliko kukubali kuwa mke wa pili kwa jamaa muongo hivo
Hus ni kweli. Ni rahisi sana kumchunguza mpenzi wako pale mnapoanza mapenzi kwani huwezi kupenda na kumzimikia mtu ghafla kwa maana ya kuingia kichwa kichwa. Muda wa mwanzo mwanzo wa uhusiano kila mtu anakuwa amekaa kimachale machale.
Ila ndio hivyo kuna watu hawawezi kujifunza mpaka wakosee (learners through mistakes) na kuna wengine wanajifunza kutokana na makosa ya wenzao (learners through other's mistakes) which is a best way to learn.
badilisha msimamo.kaa chini muyamalize na mmeo.yaani kuoa tu ndo usahau fadhira zote.ongea na moyo wako kumbuka penzi lenu lilivyokuwa moto moto.piga moyo konde.kijana kaonyesha nia na katubu.huwezi jua kwanini kaoa.maisha ni mzunguko.kama siku hiyo alikuambia na bado alivyorudi jioni ukalala nae,unafikiri kuna nini tena?inawezekana wewe ni wapili kwenye ndoa lakini wa kwanza moyoni.mia
Jitu kama hili litakuwa smart sana huwezi kulikamata, mweeee maumivu nahisi
Mia, fadhila gan sasa wakati jamaa hakuwa mkweli, this means hata walichokuwa nacho wakadhani ni penzi ni uongo mtupu
Nafikiri mazingira pia yalinifanya nimwamini, sababu alikuwa free chuoni na yuko mdogo yaani huwezi fikiria sana, na mapenzi ya dhati yalionekana machoni kabisa, labda ndio fake enyewe ila nahisi kama alikuwa real ,inakuwa raahisi kugundua kama family yake ingekuwa around

pole mpenzi, ushajua mbivu na mbichi., mwache aendelee na familia yake na wewe utapata mwingine.
Nimeipenda hii.
Naona toka mwanzo wa uumbaji wa dunia!
Ilianza kwa Mama yetu Hawa.
Akamzawadia udanganyifu Adam. Udanganyifu wa Hawa kwa Adamu ndo ulitumaliza kabisa, hadi sasa kero tu.
Achana na mawazo ya kuwa mke wa pili, hata kama utaona umri wako unaenda.
Natamani niku-pm
uhuru wa chuo ni wa muda tu, lakini muhimu kama kweli unahitaji uwe na mwenza ni vyema ukawa naye huru zaidi wakati wa likizo

pole mpenzi, ushajua mbivu na mbichi., mwache aendelee na familia yake na wewe utapata mwingine.

ni sahihi kabisa, tena huwa namwambia unanidanganya kimoyo moyo. Nikihisi unanidanganya muda si mrefu napata evidence kuwa ulinidanganya. Ni ngumu kuniamini ila habari ndio hiyo.
Pole. Fungua ukurasa mpya kwenye maisha na mapenzi kwa ujumla. Ukisikia ukubwa dawa ndio huo sasa. Yaani ndio umeshakuwa mkubwa sasa. Ila namwonea huruma huyo atayefuata baada ya hapo. Moyo ukishajeruhiwa huachiwa vidonda, vidonga vikipona huacha makovu. Sasa kwenye kovu mara nyingi huwa hakuna hisia halisi kama zile zilizopo kwenye sehemu ambayo haina kovu.
Ndio umeshakomaa hivyo Sara. Songa mbele, picha la maisha ndio kwanza limeanza!
Uwe mke wa pili? Huna wivu weye?
Yaani nina wivu wa hatari mwanajamii, nilipenda hasa
Hapana, mwache aendelee na maisha yake na wewe Mungu atakusaidia utampata wako peke yako.
pole achana nae
Pole dada kwa yaliokukuta muombe mungu akupe ujasiri utafanikiwa uatapata mwanaumwe wa kweli mwenye mapenzi ya kweli huyo uliekuwa naye hakuwa na mapenzi ya kweli kwako alitaka kukuchezea na kukupotezea tu....
wasichana wengi hawapendi kusema ukweli wanapenda kuongopewa tu ..... maana anapenda vitu vya mpito kuliko halisia
Ahsante sana kwa kweli huwezi jua ila ukiwa mchunguzi sana unaweza jua mapema, maana kunasimu zingine maybe ningekuwa mpekuzipekuzi ningegundua mapema