MoR 91
Member
- Mar 19, 2017
- 84
- 132
Kwa miaka takriban 60+ sasa tangu tumepata Uhuru wetu mwaka 1961 bado nchi yetu imeshindwa kutuonesha inasimamia malengo gani na inakwenda wapi ?
Hii kwa kiasi kikubwa inachangiwa na nchi kukosa vipaumbele binafsi ambavyo mtawala kwa asilimia Fulani Ni lazima avitekeleze kwa maana ya vipaumbele vya kitaifa, Na sio kila kiongozi kuja na vipaumbele vyake binafsi ambavyo vitaanzishwa na kuendelezwa pindi tu mtawala awapo madarakani lakini pindi atakapomaliza muda wake na nchi kumpata mtawala mpya miradi na Sera zake havitaangaliwa Tena na kupoteza tija na uzalishaji na kwa muktadha huo nchi inakuwa imepoteza pesa zake nyingi sana katika ujenzi na uanzishwaji wa miradi Ile na wakati inapaswa kuanza kuleta faida ndo wakati itakapotelekezwa bila sababu za msingi
Nalizungumzia hili nikiwa na maana kwamba tukijaribu kuzitazama Sera na maono ya viongozi wetu tangu Uhuru Hadi leo hazifanani Wala kuelekeana kwa maana nyepesi tu kwamba mfano,
Mwl J K Nyerere aliamini katika Ujamaa na kujitegemea na aliamini katika uchumi wa viwanda pia alianzisha viwanda vingi sana nchini kwa kuamini kwamba vingelisaidia sana taifa kupiga hatua kwa haraka lakini pindi tu alipopatikana mtawala wa awamu ya pili hakuona kile kilichofanywa na mtangulizi wake kwa miaka zaidi ya 20 kama kina tija hivyo akaleta Sera yake ya ubinafsishaji hivyo kazi iliyofanywa na mtangulizi wake kwa muda wote huo ikawa na matokeo hasi, na kupelekea taifa kuanza upya.
Baada ya utawala wa awamu yapili wenye Sera ya ubinafsishaji kufika mwisho taifa likampata mtawala wa awamu ya tatu nayeye aliamini kuwa kulikuwa na mapungufu katika mifumo ya mtangulizi wake hivyo akaamua kupambana Sana kurudisha Mali za serikali zilizobinafsishwa zirudi kuwa Mali za umma kwa mantiki hiyo ni kama hapo pia Ni kama nchi ikaanza upya nahivyo kuwa na miaka takribani 30+ iliyopotea bila kuwa na natija kwa wananchi na Hali imeendelelea kuwa hivyo Hadi kufika Leo ambapo nchi imefikia awamu sita za kiuongozi bado Mambo Ni yaleyale
Hasara za mfumo huu Ni kubwa Sana lakini kubwa zaidi Ni kwamba Mara nyingi miradi mikubwa mingi inayoanzishwa nchini huwa Ni pesa zinazotokana na mikopo Tena yenye riba. sasa mradi unaposhindwa kuleta faida deni la taifa linakuwa limeongezeka hivyo wananchi hubebeshwa mzigo usio na tija na hiyo ndiyo sababu deni la taifa linazidi kujua siku Hadi siku na kupelekea Kodi zisizoisha katika nchi ili kufidia madeni ambayo hayakulisaidia taifa.
Nb Kiongozi sio malaika anakosea pia hivyo Ni vyema hata viongozi wetu wakawa na vyombo vitavyowapa miongozo kwamba kwa wakati huu taifa linahitaji hiki na hiki na Sio Kiongozi kujiamulia atakavyo kwa utashi wake binafsi
Naomba kuwasilisha na Niko tayari kusahihishwa
Ahsanteni sana

Upvote
2