Ninaiomba Wizara ya Muungano na Mazingira ije na mpango madhubuti kabisa wa kupanda miti millioni 50 katika kipindi hiki cha mvua. Uhamasishaji ufanywe kuanzia uongozi wa Kaya, Mashule, Mitaa/Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya , Mikoa mpaka Taifa. Mpango huu usimamiwe kikamilifu na Waziri mwenye dhamana ya Mazingira Mhe. Jaffo na uzinduzi ufanywe na Mhe. Rais katika eneo atakalolichagua Mhe. Waziri. Ni vema tukatumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda miti millioni 50. Wenzetu jirani zetu nimeona Mhe. Rais wao ndo amekuwa msimamizi mkuu wa jambo hili. Mhe. Jaffo tunakuomba usimamie uhamasishaji wa jambo hili.