Tuwe na Shukrani kwa Rais Samia, sio mawe tu kwa sintofahamu ya Mishahara

Tuwe na Shukrani kwa Rais Samia, sio mawe tu kwa sintofahamu ya Mishahara

Mr_Teacher

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2021
Posts
362
Reaction score
343
Najua mtanipinga, lakini tusaidiane kuelewa kidogo. Kwanza asieshukuru kwa kidogo hawezi kuwa na shukrani kwa makubwa. Watumishi tulkua na matarajio makubwa sana juu ya 23%, lakini imetokea ilivyotokea. Ila, kwa mapato ya Nchi yetu na idadi ya watumishi hiyo 23% ingepigwa hivo kwa kila mtu Nchi ingeenda hii?

Roughly 60% ya Makusanyo ya TRA hutumika kuwalipa watumishi.
Tunasahau pia kuwa Mama tangu mwaka jana ameajiri sana, na sasa anaendelea kuajiri sana, kila siku Tume ya Ajira Serikalini matangazo ya kazi maelfu kwa maelfu achilia mbali zile za Afya na Elimu kule TAMISEMI, hilo ongezeko kubwa na ongezeko hili la Watumishi mlitaka Nchi isijiendeshe?

Haya kuna watu mwaka jana na mwaka huu wamepanda Mishahara kupitia kupanda Madaraja, yote haya hatuyaoni tumekalia kulaumu tu?

Mkopo umelegezwa malipo Bodies ya Mikopo hii imeongeza amount ya Take Home bado hatuthamini? La msingi ni kweli maisha magumu Serikali iendelee kuboresha mifumo ikiwemo kuthibiti mfumuko wa bei ili tuweze kumudu maisha.

Kama ni lawama apewe aliyezuia mishahara kupanda 6 years na kuzuia Ajira mda wote huo. Mama apige kazi, tumuunge mkoni, with time tutakuja kumuelewa
 
Nitasalia mwenyewe nikipaza SAUTI KABISA kwamba;-

""Samiah jiuzulu Sasa nchi imeshakushinda, ulambaji asali umekuponza"!

""Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!
 
Mwanzo nilikuwa na Imani nae japo kidogo lakini alipo mteua Kingai kuwa mkurugenzi wa mashitaka na upelelezi yaani tumepigwa vibaya Sana.

Ni afadhali hata Magufuli alikuwa anawatumia watu wasio julikana kutuua na kuteka kuliko huyu mama yenu anaye watumia watu mnao wafahamu kuwa ni wauaji na watekaji
 
Tusuburi, muda ni mwalimu mzuri
 
Kama mshahara ni mdogo acha kazi ukajiajiri kwani lazima ufanye kazi mpaka ustafu? Maana nyie wafanyakazi wengi wa Tanzakiza ni Nyumbu msio jitambua na viongozi wenu sijui tak*tk* gani Tucta
 
Back
Top Bottom