Vyuo vikuu hawafundishwi sijui mambo ya zana kwa vitendo. Vyuoni wanakula mapindi tu
Ama kweli ukistaajabu ya degree utayaona ya diploma! Chuo kikuu gani hakifundishi kutumia nyenzo? Kuna kozi inaitwa subject teaching methods, kuna educational media and technology sasa wewe unajua zina elekezwaje kwa wanafunzi? Usiseme kitu ambacho huja jionea! Fika, soma, fanya practice
bado mechi ngumu!! ningekuwa na uwezo niwalete hapa waliomaliza kidato cha nne waseme...walimu wepi walikuwa wanawakubali zaidi kiutendaji na kimaadili...
Na bado,utawapigia saluti vijana wenye shahada zao hadi ukome,mpo wengi mnaojipa moyo kuwa chekechea ni zaidi ya darasa la saba.
Hapa naona kama kuna ligi kati ya walimu wa diploma na wale wa degree. Mkimaliza hii ligi muweke na matokeo basi.
hapo ndiyo umemaliza kila kitu .big upkaka ulisha soma hiyo degree au unaisikia? Unaposema degree na diploma hamna tofauti nakuwa na wasi wasi na uelewa wako na wanafunzi unao wafundisha! Kasome degree kisha ulete uzi hapa ukihitimu.
Kwani walimu wa diploma huandaliwa na walimu wa level gani?
bado hujajitambua mwl!Mkuu kweli nina diploma na kutokana na nilivyoona uwezo wa wale degree holder nimeona sina haja ya kuchukua degree maana hakuna walichonizidi ! pia kuhusu sifa kuanzia za form 6 hadi matokeo yangu ya dip yananiruhusu kuchukua degree...sasa nifuate nini huko? kuongeza mshahara au? maana maujuzi...hahaha!
Hakuna ligi kaka hapa tatizo watu hawaelewi nini wanachozungumza. Mie nimesoma diploma na hiyo digrii pia hakika walimu wa diploma wako vizuri zaidi kitaaluma na kiutendaji.
Elimu kubwa inasaidia katika uzalishaji zaidi lakini kama haizalishi zaidi haina maana (human capital theory)
Shule za kata zina walimu wa kutosha wenye shahada lakini ukiangalia jinsi shule hizi zinavyoenda hazilingani na juhudi za serikali za kupandisha uzalishaji(matokeo) Organization as a system of flow.
Tukiwa tunatamba na digrii zetu tuonyeshe tofauti ya kiutendaji, kitaaluma, kinidhamu na kiuzalishaji.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Ukihitimu au ukipewa?