Tuwe wakweli: Diploma vs Degree kwenye ualimu

Mimi Nina Diploma na Degree.Teaching method Coverage iko poa.Behavior yao na nidhamu ni Safi.Degree unasoma Content nyingi sana.Degree ni degree tu.Mbuzi ni mbuzi na N'gombe atabaki kua N'gombe
 
Ok.. ndio wameachwa mbali lakini twende ktk uwezo wao! pia kumbuka diploma na degree wote wameishia form six!! na ujue siku hizi dip na degree wote wanakuja kwenye shule za olevel ni baadhi wanaoenda a level...jiulize why..
Unajua kwamba Kuna diploma ambao wameishia form four?
 
Utakuwa umesoma diploma?
 
Diploma!
 
Kimaadili wapo vizuri pia katika kuandaa(lesson plan lesson notes scheme work) ila kwenye uwasilishaji darasani ni wanaweza ila sio sana compared na kwenye degree. Ila wote ni waalimu
 
Teaching is an art, kuna vitu viwili lazma tuviangalie kwenye ufundishaji, cha kwanza ni contents ya kile ambacho unakifundisha, pili ni uwezo wa kudeliver kile ambacho unakifundisha, Hivyo competency ya mwalimu mzuri wa diploma au degree inategemea na hivyo vitu viwili, unaweza ukawa unajua vitu yaan una contents lakin hujui jinsi ya kudeliver, unaonekana hujui kufundisha. kwa kumaliza mwl wa degree husoma mambo mengi sana hivyo ana content kubwa ukilinganisha na mwl wa diploma,lkn mwl wa diploma yupo vizur zaidi kwenye mbinu za kufundisha lakin ana contents ndogo ukilinganisha na mwl wa degree
 
Jomon npo hapa nawaza kla mtu anatetea upande wake nachojua wengi wanaoenda diploma wanalack qualification za kwenda bachelor ukiacha wale wenye sababu za msing kama kukosa mkopo na vingine turud kwenye mada ishu ya kudeliver content inategemea na mtu mwenyewe anaeza ziwemo kichwan ila hajui kushusha vtu verse vesa is true ko bachelor hama dip haimat
Nakushaur we mwenye dip jtahd uongeze degree maana degree nazo zinazoeleka sasa
 
Kabla sijasoma bachelor nilipokuwa na diploma niliamini hivyo kwa kuona walimu wengi wa bachelor kutokumudu vitu vidogo kama lesson plan but when I joined at university education ndo nimegundua kuwa mwl wa bachelor huandaliwa kwa content kubwa sana ili akawasaidie watu kuanzia kuwaongoza kuwafundisha wanafunzi wa diploma hadi darasa LA awali duniani kote na masuala ya lesson plan na scheme of work mkazo siyo MKUBWA sana kama diploma. Kwa sababu unaweza soma course zaidi ya 60 kwa miaka 3+ ambayo ni sawa na masomo ya diploma wakati diploma kwa miaka 2+ unasoma masomo 10+ tu yanayo jirudia rudia kwa miaka yote . hiyo humfanya mwalimu kuwa vuzuri kwa hicho kichache. Kama hutojali mwl wa diploma nenda bachelor ninacho zungumza utakifahamu.
 
Naam, kwa hapa ni kama umefunga mjadala
 
Nikisema neno hapa ntaonekana nawasimanga walimu wenye diploma.
Mimi sio mwalimu ngoja niendelee kusoma comments
 
MHhhh uliona mbali

 
Mi Nina Diploma na Degree.Diploma unaiva sana kwenye teaching methodology na Ethics+Professional Codes of Conduct.Bachelor unakua deep sana kwenye content.Na unapokua deep kwenye content confidence inakua juu sana.Wakati nafanya kazi nikiwa na Diploma mtu wa Degree akinikosoa Mara nyingi nilimwona na kuhisi inferiority complex kua anafanya hivyo kwa kua kanizidi.Jambo hilo la kudharaulika lilinifanya nikasome.Na dawa ni kusoma tu,Degree ni degree tu mana Ada ya Diploma kwa mwaka haizidi 200,000 ila Baed ni zaid ya 800,000.
 
Kuwa muwazi mkuu sifa huna.
 
kaka ulisha soma hiyo degree au unaisikia? Unaposema degree na diploma hamna tofauti nakuwa na wasi wasi na uelewa wako na wanafunzi unao wafundisha! Kasome degree kisha ulete uzi hapa ukihitimu.
Mkuu achana nae,walimu wengi wa diploma ni arrogant sana.alafu wananidhamu ya uoga kwa mkuu wa shule mno. Kuna mmoja alisema hivyo hivyo kwamba haoni tofauti ya degree na diploma kumbe hana sifa za kusoma degree, alienda ku reasit akachemka vibaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…