Tuwe wakweli: Diploma vs Degree kwenye ualimu


Naungana na wewe kabisa hivi vi fm6 haviwezi kulitambua hilo sababu havijui hata nini kinafundishwa diploma vimekalia ushabiki kwa kushabikia bi degree vyao hewa visivyo kuwa hata na ubora,, mwl wa degree aliye pitia diploma ni mzuri zaid lakini kwa huyu wa fm 6 + degree ni matatizo matupu hata hapa shuleni kwangu nimeajiri hao walimu wenye sifa zote wenye dip na wenye degree kutoka fm6 na mwenye degree kutoka diploma ,,wanatofauti kubwa sana hawa walimu wangu wengi ambao ni fm 6 to degree ndio wanao lalamikiwa sana na watoto hapa shulen hawana weledi,kufundisha hawajui hata ukiwapa utawala wanakiuka kanuni,nimebadilisha utaratibu na nawapunguza taratibu hawa fm6 to degree.
 

why ulipita DIPLOMA
 
Diploma teachers wapo vizuri, nidhamu A, kujituma A, na huwa wanajua mambo mengi sana
 

maana ukweli unauma.
 

kama upo chuo na una mawazo hayo jiandae kupata frustration.
 
Tujikite kwenye mada pia tukumbuke mimi nimelenga kwenye ualimu tu. Nb nimemsamehe yule aliyeniita pimbi maana diploma tunafundishwa maadili.
 

Ndio maana nikasema haya ni mambo ya kuhuzunika sio kujivunia
 
why ulipita DIPLOMA

kama hatajibu ngoja nimsaidie mimi kukupa option za majibu ambazo husababisha
Mtu anapomaliza form six wengi chaguo la kwanza huwa Chuo kikuu (Degree) lakini huenda diploma kwa ajili ya sababu zifuatazo (Mtazamo wangu)
1.Kutokuwa na Pass za kuingia chuo kikuu
2.Kuwa na Pass za kuingia chuo kikuu lakini kutochaguliwa kulingana na nafasi.
3.Kutopata mkopo hivyo kushindwa kujilipia ada ya chuo kikuu na kuamua kuingia diploma
Kwa mtizamo wangu hizo ni sababu nilizoziona
Tuje kwenye mada
Mwalimu aliyepitia diploma huwa yupo vizuri kwenye methodolgy kwa kiwango fulani japo na wa degree naye yupo vizuri.Ila kwenye Content nadhani wa degree yupo juu.Lakini pia kwenye methodology yule aliyesoma Bed yupo juu kuliko hao wengine wote.

Mwisho tuache zana za kufikirika ukienda kazini ukiwa umejaa kiburi kichwani utapata shida tu,uende kazini ukiwa unajua kuwa unaenda kufanya kazi,kama unajua vitu basi onesha kwa kumwaga kwa wanafunzi sio kuja kujisifia jamiiforums
 
kuweka sawa mimi nimefaulu vizuri form six na diploma . nimemaliza chuo mwaka jana nipo nasubiri ajira hapa
 
Toka serikali ianze kutoa walimu wengi wa diploma na degree ndio matokeo ya wanafunzi yanazidi kuwa mabaya yaani vitu ni inversely proportion,sijui hao wazuri wanafanya nini maana zero kama kawa zinaongezeka mara dufu
 

Wewe umemamliza Form Six halafu umekwenda Chuoni kufundishwa namna ya kufundisha. Jee, unadhani elimu uliyonayo inatosha kumfundisha mwanafunzi wa Form Six? Siyo unataka kuturidisha kwenye ualimu wa UPE?

Unasema elimu yako uliyonayo ya F6 na Diploma inatosha, hivyo ndivyo unawaeleza wanafunzi wako? Bado huamini kuwa elimu haina mwisho?
 
kuweka sawa mimi nimefaulu vizuri form six na diploma . nimemaliza chuo mwaka jana nipo nasubiri ajira hapa

hukufaulu vizuri wewe sema ulifaulu kwa kiwango gani,scan matokeo weka hapa,ww upate one au 2 ya art uwende diploma,me nna wanafunz wangu wana two na baadhi III wapo university leo hii
 

Kweli vijana hamna adabu! Diploma holder ni mwanafunzi wa degree holder na hata paper zenu zinatungwa na kusahihishwa na degree holders. Sasa unaweza kumfundisha mwenye degree na kadiploma kako ka necta? Hivi darasa la saba anaweza kusema anamzidi mwl wake alie na form four content? A
 
Uwapunguze wewe kama nani? Nenda kasome acha kujifariji na maneno ya kiswahil
 
Ntaanza kuuliza maswali ya KOZI MLIZOSOMA HUMU NYIE DIPLOMA TUONE WELEDI WENU,HAYA MKO TAYARI? Tuondoe ubishi maana mmezidisha DHARAU,kuwa na degree si mchezo nyie sio mnafikiri ni DIP zenu hizo,Yaani ukiwa na DIP then unajisifu wewe ni mjinga wa mwisho kabisa.
 
hukufaulu vizuri wewe sema ulifaulu kwa kiwango gani,scan matokeo weka hapa,ww upate one au 2 ya art uwende diploma,me nna wanafunz wangu wana two na baadhi III wapo university leo hii

nikifanya hivyo nitakuwa nimetoka nje ya mada kama wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…