Tuwe Wakweli: Kama Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalumu wasingeenda Bungeni ruzuku ingepungua sana chama kingeendeshwaje?

Viti maalum mali ya wanawake kivipi? Si wangeteuliwa hata wa chauma ama wale wasio na vyama.?
 
Ruzuku ya chama inatokana na kura katika uchaguzi mkuu siyo uwepo wa wabunge bungeni.
Faida ya ziada kwa CHADEMA kuwa na wabunge ni michango yao kwa chama
 
Ni wakati wananchi wa tanganyika waelewe kuwa hii nchi si ya kupiganiwa na chama fulani, bali watu wote. Hata kama huendi vitani, watie moyo waliopo vitani, sio unawaacha unaenda kula bata unategemea wafie huko kwa ajili yako. Wananchi mjifunze. Chama hakiwapiganii msipojipigania wenyewe

Acheni upumbavu bwana.
 
Unavyodai kuwa unawapongeza CHADEMA kwa kuwatendea haki Wanawake wa Tanzania,unaweza kuthibitisha ya kwamba wale wanawake 19 wamepelekwa bungeni kwa baraka zote za chadema na wala siyo kwa njia za panya kutoka kwa mamlaka?
 

Ama kwa kweli wajinga ndi waliwao!!!!!!😡😡😡
 
Unavyodai ya kwamba shughuli za uendeshaji wa chama zinahitaji fedha na wabunge 19 ni mtaji mzuri wa kutunisha mfuko wa ruzuku, kwani chadema walikuambia kuwa wanahitaji ruzuku kupitia uchaguzi haramu ambao haukuwa uchaguzi bali ni uchafuzi wa demokrasia?
 
sasa katibu mkuu Mnyika mbona anapiga kelele sana!? amenyimwa nini?!
 
Unavyodai kuwa unawapongeza CHADEMA kwa kuwatendea haki Wanawake wa Tanzania,unaweza kuthibitisha ya kwamba wale wanawake 19 wamepelekwa bungeni kwa baraka zote za chadema na wala siyo kwa njia za panya kutoka kwa mamlaka?
Kwani katika wale wabunge 19 kuna mwanamme pale?!
 
Huwezi kuitenganisha Chadema na fedha hata siku moja bwashee!
 
Huwezi kuitenganisha Chadema na fedha hata siku moja bwashee!
Wewe ni mwekahazina wa chadema hata usemee mambo yahusuyo fedha ya chadema?Unavijua vyanzo vyao vya mapato?What if vyanzo vyao vingine vya mapato vinajitosheleza?
 
Wewe ni mwekahazina wa chadema hata usemee mambo yahusuyo fedha ya chadema?Unavijua vyanzo vyao vya mapato?What if vyanzo vyao vingine vya mapato vinajitosheleza?
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG wale Chadema wanategemea ruzuku na misaada kutoka kwa wazungu.

Hawana miradi kama wenzao CCM!
 
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG wale Chadema wanategemea ruzuku na misaada kutoka kwa wazungu.

Hawana miradi kama wenzao CCM!
Unavyojinasibu kuwa hawana miradi kama CCM, Kwani vyanzo vya fedha ni lazima viwe miradi?
 
Naomba kufahamu utaratibu wa viti Maalumu kwenye Chama ukoje? Maana nionavyofahamu
Wanaomba na kupigiwa kura kabla hata ya uchaguzi sasa imekuwaje hawa tena au ndiyo waliopita mwanzoni kabla ya kukosa kwenye majimbo?
Utaratibu wa viti maalum unapaswa kuwa hivi.

1. Uchaguzi mkuu ukishafanyika, tume ya uchaguzi inatangaza nafasi za viti maalum kulingana na kila chama kilivyopata kura.

2. Chama husika kinafanya mchakato wake wa ndani kupendekeza majina ya wanawake kutoka chama chao. (Kila chama kina utaratibu wake wa ndani kulingana na katiba ya chama husika, na mchakato huo unaweza kuanza hata kabla ya uchaguzi, lakini hauwezi kukamilika mpaka uchaguzi uishe. Kwanini? Huwezi kujua chama kitapata nafasi ngapi kabla ya uchaguzi)

3. Chama husika kinaweka orodha ya majina iliyoyapendekeza kwa umma.

4. Katibu mkuu wa chama husika anawasilisha orodha ya majina yaliyopendekezwa na chama chake kwenda NEC.

5. NEC inaweka wazi kwa umma orodha ya majina ya wanawake waliopendekezwa kupewa hivyo viti maalum.

6. NEC inawasilisha rasmi hiyo orodha kwa spika wa bunge.

7. Spika wa bunge anaweka wazi kwa umma orodha ya majina ya wanawake wa chama husika walioteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum.

8. Wabunge walioteuliwa wanaampa ndani ya bunge mbele ya spika siku ya kikao cha bunge.
 
Walioteuliwa ni wabunge wanawake haijalishi wamepatikanaje bwashee!
Kwa nini haijalishi wamepatikanaje?Kwani hawawezi kupatikana kwa njia haramu na ambazo ziko nje ya kanuni pamoja na sheria kitu ambacho ni cha kujali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…