Tuwekane wazi kilimo chenye tija ni cha umwagiliaji

Mausingizii

Member
Joined
Jul 14, 2022
Posts
90
Reaction score
74
Wasalamu ndugu zangu, km ambavyo kichwa cha uzi kinajieleza miaka ya nyuma kabisa nilikua mpenzi wa kufuatilia nyuzi mbalimbali zinahusu kilimo katika jukwaa hili.

Nyuzi nyingi zimeandikwa katika upande wa mafanikio tu na kusahau changamoto ambazo ndizo zinamfanya mkulima aamue vyema.

Baada ya kupitia nyuzi mbali mbali katika mitandao nami nikaona nijitose katika kilimo hiki pendwa cha makaratasi au cha kwenye madaftari ambapo nilianza na kilimo cha mahindi KWA KUTEGEMEA MVUA ,mwaka 2019 na katika kilimo hicho mavuno hayakuendana na nguvu niliyoiweka shambani hapo.

Baada ya hapo nikajitosa katika kilimo cha maharagwe kwa mwaka huu na kama mnavyoona hali halisi mazao yamekauka na tumeishia kuunguza mitaji, kama wasemavyo wahenga kwamba hasara hutokea katika biashara yoyote ile na ndio hukupa uzoefu na mimi nikiri kwamba kutoka katika kazi hii nimegundua kwamba kilimo cha uhakika KILIMO CHA UMWAGILIAJi.

1: Kilimo hiki kinampa mkulima uhakika tofauti na kilimo cha msimu ambacho mkulima hucheza pata potea.

Pili, kilimo cha umwagiliaji kinatoa fursa kwa mkulima kucheza vizuri na soko Lake, Hii ni kwasababu anauwezo wa kuivisha zao lake muda wowote kulingana na uhitaji wa soko tofauti na kilimo cha misimu ambacho kinasababisha mafuriko ya bidhaa sokoni kipindi cha mavuno na kusababisha bei ya bidhaa kushuka.

Mwisho, Nitoe rai kwa serikali kuwa isiishie kuwa na mikakati ya kwenye makaratasi kwaajili ya kusomwa bungeni, tupeni mitaji ya kilimo vijana, pembejeo zimepanda bei sawa, huenda liko nje ya uwezo wenu lakini vipi kuhusu masoko?

Yametawaliwa na madalali wanyonyaji, njiani tunapopitisha bidhaa vibali kibao, kwan mnashindwa kurasimisha masoko hata kuweka mifumo mizuri kwa sisi ambao tunapigika mashambani ili angalau na wakulima wafaidike.

Mmewahi kujiuliza kuwa Licha ya kilimo kuwa uti wa mgongo ni kwanini asilimia kubwa ya watanzania ambao ni wakulima ni maskini?

Mbona kenya yenyewe imeweza? Kwann kilimo kisiwe ajira ya kukimbiliwa na badala yake vijana tumeishia kukesha na CV mikononi na kuilalamikia serikali, kilimo kinaonekana kama kazi ya watu duni na wajinga.

Mtaala wa elimu hautoi elimu tosha kuhusu kilimo, taasisi zinazojinadi kuhusika na kilimo tunaziona mitandaoni tu kama linked in, na kufanya zoom Conferences ambacho huishia kujadili kwa kiingereza kuseti goals ikiwa sisi vijijini huku hatuwaoni. Wekeni strategies kuorganize vijana na kuwapa mikopo ya kilimo na wakaufunzi au mabwana shamba wa kutosha .

Mwisho nitoe rai kwa jamii niko katika mchakato wa kukamilisha idea ya kuunda katiba, kushare mitaji ili tutengeneze partnership nzuri ya kilimo, tulime kilimo chenye tija.
 
Mkuuu sisi tulio toka mikononi mwa wakulima tuna kauli mojà ...JEMBE HALIMTUPI MTU...mkuu endelea kukomaa hata km umeanza na changamoto .Pia kwa kweli serikali haitujali wakulima cha msingi ni kukomaa tu mkuu tukisema tusubiri serikali ndo kuukaribisha umasikini.
 
Mikopo Wanatoa SEMA ugumu wake hadi uweke reheni hati ya nyumba Sasa kwa kijana anaeanza anaitoa wapi
Ila komaa taratibu Ndugu yangu
 
Wasalamu ndugu zangu, km ambavyo kichwa cha uzi kinajieleza miaka ya nyuma kabisa nilikua mpenzi wa kufuatilia nyuzi mbalimbali zinahusu kilimo katika jukwaa hili.

Nyuzi nyingi zimeandikwa katika upande wa mafanikio tu na kusahau changamoto ambazo ndizo zinamfanya mkulima aamue vyema.

Baada ya kupitia nyuzi mbali mbali katika mitandao nami nikaona nijitose katika kilimo hiki pendwa cha makaratasi au cha kwenye madaftari ambapo nilianza na kilimo cha mahindi KWA KUTEGEMEA MVUA ,mwaka 2019 na katika kilimo hicho mavuno hayakuendana na nguvu niliyoiweka shambani hapo.

Baada ya hapo nikajitosa katika kilimo cha maharagwe kwa mwaka huu na kama mnavyoona hali halisi mazao yamekauka na tumeishia kuunguza mitaji, kama wasemavyo wahenga kwamba hasara hutokea katika biashara yoyote ile na ndio hukupa uzoefu na mimi nikiri kwamba kutoka katika kazi hii nimegundua kwamba kilimo cha uhakika KILIMO CHA UMWAGILIAJi.

1: Kilimo hiki kinampa mkulima uhakika tofauti na kilimo cha msimu ambacho mkulima hucheza pata potea.

Pili, kilimo cha umwagiliaji kinatoa fursa kwa mkulima kucheza vizuri na soko Lake, Hii ni kwasababu anauwezo wa kuivisha zao lake muda wowote kulingana na uhitaji wa soko tofauti na kilimo cha misimu ambacho kinasababisha mafuriko ya bidhaa sokoni kipindi cha mavuno na kusababisha bei ya bidhaa kushuka.

Mwisho, Nitoe rai kwa serikali kuwa isiishie kuwa na mikakati ya kwenye makaratasi kwaajili ya kusomwa bungeni, tupeni mitaji ya kilimo vijana, pembejeo zimepanda bei sawa, huenda liko nje ya uwezo wenu lakini vipi kuhusu masoko?

Yametawaliwa na madalali wanyonyaji, njiani tunapopitisha bidhaa vibali kibao, kwan mnashindwa kurasimisha masoko hata kuweka mifumo mizuri kwa sisi ambao tunapigika mashambani ili angalau na wakulima wafaidike.

Mmewahi kujiuliza kuwa Licha ya kilimo kuwa uti wa mgongo ni kwanini asilimia kubwa ya watanzania ambao ni wakulima ni maskini?

Mbona kenya yenyewe imeweza? Kwann kilimo kisiwe ajira ya kukimbiliwa na badala yake vijana tumeishia kukesha na CV mikononi na kuilalamikia serikali, kilimo kinaonekana kama kazi ya watu duni na wajinga.

Mtaala wa elimu hautoi elimu tosha kuhusu kilimo, taasisi zinazojinadi kuhusika na kilimo tunaziona mitandaoni tu kama linked in, na kufanya zoom Conferences ambacho huishia kujadili kwa kiingereza kuseti goals ikiwa sisi vijijini huku hatuwaoni. Wekeni strategies kuorganize vijana na kuwapa mikopo ya kilimo na wakaufunzi au mabwana shamba wa kutosha .

Mwisho nitoe rai kwa jamii niko katika mchakato wa kukamilisha idea ya kuunda katiba, kushare mitaji ili tutengeneze partnership nzuri ya kilimo, tulime kilimo chenye tija.
Nimesoma andiko lako mkuu,nimekuelewa vizuri sana,naomba serikali ifanye juu chini tuna ardhi ya kutosha,Dodoma mahindi yalikuja vizuri sana!mvua zimekata hakuna tena matumaini!
 
Ninasiku kadhaa hapa Dodoma ,imenyesha Jana na Leo naona vimanyunyu huku maeneo ya zuzu
 
Back
Top Bottom