Watanzania tumefikia wakati sisi wenyewe kwa wenyewe hatuwezi kusikilizana au kuheshimiana. Watanzani wengi siku hizi wamekuwa wakiangaliwa kibinafsi wakitoa hoja kuliko kusikiliza hoja za wanaotoa.
Mara nyingi sana tumekuwa hata hatusikilizani kwa sababu ya woga au kujijengea fikra za uongo. Hili linaturudisha nyuma sana mifano hii hapa
1. Kumezuka kutofahamu kwa Watanzania siku hizi kwa kupewa barua za kukemea mambo tofauti nchini. Pamoja na mazuri kuna mambo ambayo yanakiuka haki za binadamu nchi nyingine zinaona lakini sio nchi zote.
Mabalozi wetu wanajua yote haya lakini wametawaliwa na woga hivyo hawawezi kuwaambia waziri wa mambo ya nje ukweli wa mambo kiwazi na badala yake wamekuwa wepesi wa kurembesha maneno.
Kinachotokea waziri anafikiri mambo sio makubwa mpaka inafikia tunawekewa vikwazo tofauti bila waziri kujua vizuri. Hii inatokana na utamaduni wa kuogopana na vilevile utamaduni wa kutokusikilizana.
Tungeweka uwazi mapema mambo mengi sana sana tungeweza kurekebishana kabla hayajawa majanga
2. Kama mna kumbuka tukienda miaka sita tu nyuma tulikuwa hatusikilizani wapinzani walikuwa hawasikilizi CCM na CCM walikuwa hawasikilizi wapinzani.
Sasa watu walewale wameona kumbe zile rushwa, pesa za madini na mambo mengi ambayo walikuwa wanasema yalikuwa ya kweli.
Tumejua hivyo baada ya kuona wenyewe laini vilevile wana CCM wenyewe ndiyo wanasema hivyo. Kumbe mambo mengi yangeweza kufanyika mapema lakini tumeweka utamaduni wa kutokusikilizana na ukiongea kitu wanaangalia wewe ni nani.
3. Tushukuru mitandao bila mitandao tusingeweza kujadili kitu maana ungemuona huyu Mtanzania mwenzako wengi wangeanza kusema huyu mpinzani tu ataongea nini, huyu diaspora au huyu ni CCM tu.
Tuna utamaduni wa kuangalia watu zaidi kuliko kusikiliza hoja na ndiyo maana angalau mitandao ndiyo sehemu pekee ya mijadala. Yaani hatuna mijadala hata level ya ubunge Tanzania.
Kwanini tujiulize mtu anagombea wasikutane wakaulizwa maswali moja kwa moja na wananchi kuhusu mikakakti yao bila kukaa nyuma ya ilani ambazo huwezi kusema mamtatizo yote ya sehemu yanafanana.
Tanzania sasa hivi kuna vijana wengi sana 67% ni chini ya miaka 25 wengi hawana kazi. Hakuna mtu mpaka leo hii anajua hawa vijana watafanya kazi gani, wataishi vipi kwa ushindani wa siku hizi.
Kama hatuna plan na tukaacha tu kazi zitaendelea kuwa ngumu kupatikana. Hivyo tusikilizane wakati watu tofauti wanatoa mawazo yao kuhusu uchumi na kazi badala ya kukimbilia kupinga kila kitu kwasababu mawazo yametolewa na mtu ambaye wewe hukubaliani naye mara nyingi.
Kama nchi yetu ilivyo sasa tunahitaji mbinu sana. Watu wengi hawajui serikali haiogopi upinzania kama vyama serikali inaogopa vijana. Lazima tujikite kutatua swala hili la kazi kabla hatujaanza kuogopana zaidi.
Nimeshangazwa na fensi kubwa na mbwa wengi ambao tunaweka kwenye nyumba zetu wakati hata silaha haziruhusiwi Tanzania kiholela. Watanzania tunaogopana na badala ya kuogopana tusikilizane